Kama hawafai hawafai tu hata wawe 1000.Tuko vyuoni tuliaminishwa Mwinyi hafai, tukapoteza tukafukuzwa vyuoni na vyuoni vikafungwa kwa mwaka mzima, akaja Mkapa tukaambiwa hakufai, akaja Kikwete tukaaminishwa hafai, akaja Magufuli tumeambiwa hakufaa. Na sasa yuko Samia tukaambiwa hivyo hivyo, na wote hawa wana staili tofauti ya Uongozi.
Jee nyinyi mnaona nani anafaa Lissu?, Mbowe? au nani?
Mnacho sahau hawa ni kuwa viongozi hawa wote ni wa Tanzania wenzetu tunaongea nao, tunakunywa não, tuna cheka não na tunasikitika não.
Tuna wafahamu uzuri, Ubaya na upungufu wao. Mnapo tushawishi kuwa wanafaa watu pumbavu pumbavu mnafanya kila mnae ona anafaa tumuangilie kwa jicho la tatu, na tunapogundua hafai hatuwasikilizi tena..
Watanzania tunapata viongozi kutoka miongoni mwetu na uwakilishi wa sisi tulivyo na sio kutoka mbinguni.