Rais Samia, achia pesa hali ni mbaya mtaani

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,945
2,000
Napenda kumkumbusha tu Mama akumbuke huku mtaani hali ni mbaya sana hakuna pesa mtaani tunarudi enzi za ujima za kibadiishana mchele na nguo au mafuta na unga n.k

Biashara hazifanyiki sababu watu hawana pesa(purchasing power) na wenye dhamana na uchumi wetu wameweka pamba masikioni.

Waziri wa fedha amkumbushe mama atoe kibali cha kuachia pesa kwenye mzunguko wa uchumi, kwa kutoa ajira, kulipa madeni ya ndani, serikali ifanye shughuli na sector binafsi, bank yashushe riba ili watu wakope kiurahisi zaidi na kwa riba ndogo n.k kuweza kusaidia pesa ingie kwenye mzunguko wa uchumi wetu.

Ninachokiona tukienda kwa mwenendo huu ndani ya mwaka mmoja mtu mmoja akaja akamobilize watu kuingia mtaani hakika mziki wake utakuwa mgumu kuuzima. Sababu kila mtu kwa sasa anaumia kwa aina yake mwenye kitu na asiye kuwa na kitu, vijana hadi wazee, wenye ajira na wasiokuwa na ajira, wagonjwa na wazima, maskini na matajiri, wenye dini na wasiokuwa na dini, wafanyabiashara na wasiokuwa na biashara, wakulima na wachuuzi, wavuvi na madalali n.k
 
Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,914
2,000
Tunajenga kwanza miradi ya kimkakati alisikika mpigiani legacy kutoka chattle.

Nikukumbushe tu kama kweli watumishi watapanda madaraja mwaka huu esp mwezi wa sita au wasaba kutakua na ingizo la bilioni zaidi ya 300 kwenye mzunguko.

Akimwaga hizo ajira ambazo vijana wanaomba sasa kutakuwa na ingizo jingine na mabilioni.

Achana na yule mgawa laki tano tano kwa wanyonge akidhani ndio njia sahihi ya kuwapigania.
 
Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
4,953
2,000
Kama fao la kujitoa hakuna hapo pesa mtaani tutaendelea kuichezea wachache tuliokaa mferejini.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,072
2,000
Tunajenga kwanza miradi ya kimkakati alisikika mpigiani legacy kutoka chattle.

Nikukumbushe tu kama kweli watumishi watapanda madaraja mwaka huu esp mwezi wa sita au wasaba kutakua na ingizo la bilioni zaidi ya 300 kwenye mzunguko.

Akimwaga hizo ajira ambazo vijana wanaomba sasa kutakuwa na ingizo jingine na mabilioni.

Achana na yule mgawa laki tano tano kwa wanyonge akidhani ndio njia sahihi ya kuwapigania.
kwani hizo 300b zinatoka jupiter!!!si ni hizo hizo zinazokusanywa na tra??
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,062
2,000
Chonde chonde wanawake wenzangu .tukimbizane na huyu mama mzunguko utarudi tu later..kama hukujenga kipindi cha Jk bas kipindi hiki jenga walau nyumba ya rooms 2!
Nna imani na mama la Mama SSH!
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,259
2,000
Chonde chonde wanawake wenzangu .tukimbizane na huyu mama mzunguko utarudi tu later..kama hukujenga kipindi cha Jk bas kipindi hiki jenga walau nyumba ya rooms 2!
Nna imani na mama la Mama SSH!
Wa mbili wa mbili tu watu tumejenga multiple houses wakati wa JPM....chapeni kazi hakuna mwanasiasa atakuwekea hela mfukoni labda awe mzazi wako.
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,042
2,000
Wa mbili wa mbili tu watu tumejenga multiple houses wakati wa JPM....chapeni kazi hakuna mwanasiasa atakuwekea hela mfukoni labda awe mzazi wako.
Ni Bora wewe uwaambie ukweli, hata kipindi Cha jk Kuna watu walishindwa kujenga.
Kujenga au kutojenga hii inategemea na wewe mwenyewe, na ndio ukweli wengi hawaupendi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom