jamii01
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 1,974
- 1,400
Napenda kumkumbusha tu Mama akumbuke huku mtaani hali ni mbaya sana hakuna pesa mtaani tunarudi enzi za ujima za kibadiishana mchele na nguo au mafuta na unga n.k
Biashara hazifanyiki sababu watu hawana pesa(purchasing power) na wenye dhamana na uchumi wetu wameweka pamba masikioni.
Waziri wa fedha amkumbushe mama atoe kibali cha kuachia pesa kwenye mzunguko wa uchumi, kwa kutoa ajira, kulipa madeni ya ndani, serikali ifanye shughuli na sector binafsi, bank yashushe riba ili watu wakope kiurahisi zaidi na kwa riba ndogo n.k kuweza kusaidia pesa ingie kwenye mzunguko wa uchumi wetu.
Ninachokiona tukienda kwa mwenendo huu ndani ya mwaka mmoja mtu mmoja akaja akamobilize watu kuingia mtaani hakika mziki wake utakuwa mgumu kuuzima. Sababu kila mtu kwa sasa anaumia kwa aina yake mwenye kitu na asiye kuwa na kitu, vijana hadi wazee, wenye ajira na wasiokuwa na ajira, wagonjwa na wazima, maskini na matajiri, wenye dini na wasiokuwa na dini, wafanyabiashara na wasiokuwa na biashara, wakulima na wachuuzi, wavuvi na madalali n.k