Kwa hali inayoendelea mtaani, Makonda ndio akiba pekee ya CCM upinzani imara ukitokea

Messenger RNA

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,103
3,023
Sio siri tena hali ya mtaani inazidi kuwa tete kwa wananchi na kama haitoshi hawaoni yeyote akiwatetea,zaidi ya kuwapendelea matajiri.Mifano wanayotoa ni:-

1. Bei za nauli zinapanda bila kujali maslahi ya wananchi kwa kisingizio cha kupanda mafuta,wanauliza mbona yakishuka bei hakuna anayeshughulika kushusha hata kidogo?

2. Sukari kwa sasa wanaotumia ni wenye uchumi tu maana bei haishikiki,hakuna mwanaccm wala chadema anayepaza sauti,zaidi ya wote kuendelea kulamba asali.

3. Ajira ni pungufu,vijana wakitaka kujiajiri kwenye mitandao wanakutana na bei zisizo rafiki za mabando na usumbufu mwingine,kwenye kilimo na biashara hali kadhalika na hakuna anayejali.

4. Mikopo ya halmashauri ili vijana wajikwamue nako lahaula vijana wengi wanajikuta wakikata tamaa kwa urasimu uliopo mwisho wa siku kama huna kadi basi umeumia,na hakuna anayeona akakemea kwakua hayawahusu.

5. Na mengine mengi sana wananchi wanakumbana nayo.

Kwanini makonda angalau?
Tangu kuteuliwa kwake anaonyesha uthubutu japo kupiga vijikelele(ambavyo hata hivyo havijazaa matinda), lakini huwezi amini wananchi ukiachana na hawa wa jamhuri ya mtandaoni wanaona kama anaweza kuwa mkombozi wao,huku wanaccm wengine wakiwa kama hakuna madhira yanaendelea kwa wananchi.

Ambacho kinaendelea kuibeba CCM ni uwepo wa upinzani dhaifu na uliogawanyika,siku upinzani ukijitambua kama wa 2015, CCM kutakuwa na kibarua kizito na turufu itakuwa ni Makonda na kidogo Bashe, wengine wote wameoza .
 
Anachofanya makonda ni drama za ccm tu. Wanakutenngenezea matatizo wao wenyewe. Wanayatafutia suluhu kwa kulaumiana.
Kwakuwa wengi wetu tuwajinga tunawaamini na kuwapa uongozi tena. Tangu lini kelele zikawa suluhisho ya matatizo
 
Anachofanya makonda ni drama za ccm tu. Wanakutenngenezea matatizo wao wenyewe. Wanayatafutia suluhu kwa kulaumiana.
Kwakuwa wengi wetu tuwajinga tunawaamini na kuwapa uongozi tena. Tangu lini kelele zikawa suluhisho ya matatizo
unachosema kina ukweli,lakini kina nafuu kuliko hao wengine ambao wamekauka kama hakuna kinachotokea kwa wananchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom