lord atkin
Senior Member
- Sep 30, 2018
- 197
- 683
Ni nani ajitokeze awaambie ukweli hawa wanawake? Hali inatisha kila siku wanalilia kulipiwa mahari na harusi, yaani siku hizi mwanamke anahitaji harusi (sherehe) kuliko anavyohiyaji ndoa (kuishi na mume).
Wanawake wengine wapo radhi wamwache mwanaume wanayempenda kisa hana uwezo wa kuwalipia mahari na harusi ili waolewe na mwanaume mwenye pesa za mahari.
Wakati hayo yakiendelea wazazi nao wamepandisha mahari bei juu, bila milioni tatu nne au tano hupati mke. Utasikia mbona shangazi yangu aliolewa kwa mahari, jamani zamani kila mzazi alikuwa na ng'ombe na wazazi waliwalipia watoto wao mahari leo hii nani analipia mtoto mahari ya milioni tano? Huyu kijana asiye na ajira ndiyo akulipie mahari ya milioni tano kweli?
Ifike wakati sasa wanawake wabadilike hali ya kiuchumi ya vijana wengi wa kitanzania walio katika umri wa kuoa ni mbaya Sana waache kung'ang'ania mahari na maharusi ya kifahari.
Kijana amemaliza chuo mwaka wa tatu huu yupo mtaani hana ajira lakini binti unang'ang'ania aende kwenu akalipe mahari afunge harusi ndiyo mjenge familia ataweza wapi? Atapata wapi milioni nne za kwenda kulipa mahari na milioni 10 za Harusi? Kwanini usimkubalie muanze kuishi pamoja mjenge familia kwanza hayo mambo mengine ya mahari na harusi yafuate baadaye mkishajipanga?
Wanawake badilikeni kuweni waelewa kubalini sogea tuishi vijana hali ya kiuchumi ni ngumu Sana siku hizi.