Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,580
4,262
Namsikiliza Rais Ruto hapa Citizen TV tangu 19h00 (anahojiwa live na Radio/Tv).

Wenzetu wako vizuri kwenye Interview, Waandishi na wenye vyombo vya habari wanacha kujifunza hapa.
Pamoja na mambo mengi aliyo ongelea, mimi nimevutiwa na ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Kwa kuanzia wafanyakazi watachangia 3% ya mshahara na Serikali itaongezea 3% ya kiasi mtumishi alizotoa Jumla 6% ambazo zitakuwa za mfanyakazi.

Mfanyakazi ataruhisiwa kutumia hela hizo kama kianzio cha kupewa nyumba na kuendelea kulipia kidogo kidogo kwa mfumo wa kodi ya pango au kuzichukua kwa mkupuo akistaafu.

Amesema hili wazo likipita, litawapa vijana ajira nyingi sana wakati wa ujenzi kwani nyumba za kawaida zinazotarajiwa kujengwa ni laki tano nchini humo kwa kuanzia (maeneo ya mijini).

Na hii inaweza kusaidia sana kupanga miji na kusaidia maeneo mazuri ya kilimo na kazi zingine yasitumike kwa ujenzi..

Interview inaendelea.....
 
Ila Kenya kuna Waandishi bhana

Hayo mahojiano hayachoshi kusikiliza

Mtangazaji wangu wa Citizen tv kwenye hilo Jopo la Waandishi hajatuangusha!
 
Back
Top Bottom