Rais Museveni aapishwa kuongoza Uganda kwa miaka mitano

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
112
500
Rais Yoweri Museveni ameapishwa kwa mara ya sita mfululizo kuliongoza taifa hilo hadi mwaka 2026 katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Kololo nchini humo.

Museveni amekuwa kiongozi wa nchi hiyo tangu mwaka 1986. Sherehe za uapisho zimehudhuriiwa na viongozi takriban 11 wa mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwamo Samia Suluhu wa Tanzania, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Évariste Ndayishimiye wa Burundi, Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia na Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe.

Museveni alitangazwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2021 dhidi ya mpinzani wake Robert Kyagulanyi 'Bobi Wine' baada ya kujinyakulia kura milioni 5.85 au asilimia 58.64 ya kura zote.

museven.jpg
 

kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
2,458
2,000
Africa, kiongozi anabakia madarakani hadi kutamka neno katiba aliyoapa kuilinda ashindwe ndipo wakumbuke kumng'oa eg Mugabe namseveni nae itakua hivohivo. Jamani
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,725
2,000
Leo hii rais Yoweli Kaguta Museveni anapishwa kuwa rais nchini Uganda.

Katika mtazamo wa vyombo vya ulaya na hasa pale nchini Ujerumani
Dw wamekuja na kibonzo kuhusu kiapo cha rais Museveni.

Je kwa picha hii inaashiria nini kwenye uongozi au kwa viongozi wengi barani Afrika?

Screenshot_20210512-132551.jpg
 

diego's

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
293
250
Makamanda wa ufipa wanamsema museveni ni dikteta ila wamesahau wanae mwenyekit ambae hata wao hawajui atang'atuka lini,maana hukuna kama mwamba
 

kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
2,458
2,000
Kwasasa vyama mbadala hapo Uganda wachunge sana kanisa katolic rasivyo museveni ataenda tena kurubuni nakusema waliangalia vibaya mwaka wa kuzaliwa mseveni wa watu

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,207
2,000
Some stupid people are saying.... Museven must go.....Museveni must go.... GO WHERE? (By Yoweri Kaguta M7)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom