Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,869
Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma (82), amezuiwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini ili asigombea Ubunge wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 29 Mei 2024. Mh. Jacob Zuma alitaka kugombea kupitia uMkhontho weSizwe (MK), chama kipya kilichosajiliwa karibuni kikitumia jina la Jeshi la msituni la zamani la ANC wakati wa kupigania Uhuru. Juhudi za ANC kutumia mahakama ili kuzuia usajili wa MK zimegonga mwamba baada ya mahakama kutupilia mbali hoja zao.
Katika Uchaguzi wa Afrika Kusini, wapiga kura hawachagui Rais, bali huchagua Wabunge 400 ambao baada ya siku 30 hukutana kumchagua Rais. Kwa ujumla, kiongozi wa chama ambacho kitapata Wabunge wengi ndiye aliye na fursa ya kuchaguliwa kuwa Rais na kuunda Serikali.
Kitendo cha Jacob Zuma kukiunga mkono MK kinafanya wachambuzi wa masuala ya siasa za Afrika Kusini waone Zuma anaweza kupunguza kura za ANC hasa pia katika Jimbo la Kwazulu Natal anakotoka yeye na kuifanya ANC kukosa kufikisha kura 50% kwa mara ya kwanza katika historia ya Uchaguzi wa kidemokrasia kutoka mwaka 1994.
Hayo yakitokea, inaweza kupelekea pia vyama vingine kuungana dhidi ya ANC kuunda Serikali mseto ili kuiondoa ANC kutoka madarakani. Hata hivyo, hata ANC yenyewe inaweza kuunda umoja na vyama vidogo vidogo ili pia kufikisha idadi ya kura ya asilimia 50% ili kuunda serikali.
Jacob Zuma alifungwa jela miezi 15 kwa kosa la kudharau mahakama. Sheria za Afrika Kusini zinamzuia mtu yeyote kugombea nafasi ye yote katika Uchaguzi Mkuu kama aliwahi kupatikana na jinai ya kifungo cha miaka miezi 12. Jacob Zuma anayo nafasi ya kuukatia rufaa uamuzi wa kumzuia kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Mei 2024.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 28 Machi 2024; saa 3:24 usiku