Rais Magufuli: Uchumi mzuri ni pamoja na kuwa hela ngumu kuipata; kizuri hakipatikani hovyo hovyo

pierre-plissonnier_3463867b.jpg

huyu ni CEO wa airfrance akila kichapo baada ya kutangaza redundancy. Hizi ni nchi zilizoendelea na zenye uchumi imara , hasira za wananchi, kupunguza wafanyakazi haizifanyi kuwa za hovyo au uchumi kupinda siku zote, inaweza kuwa season ya mud mfupi.
NMB sijui sababu lkn kama ni sehemu ya transition ktk kuupokea mfumo mpya ipo siku mambo yatakaa sawa.

Mkuu jamaa alisema 2018 ni mwisho wetu kuvaa mitumba, je hayo ni kweli au huwa anasema ili ww na wenzako mshangilie? Sasa unaposema uchumi utakuwa mzuri ni kuanzia mwaka kesho tutakapoacha kuvaa mitumba?
 
Mkuu jamaa alisema 2018 ni mwisho wetu kuvaa mitumba, je hayo ni kweli au huwa anasema ili ww na wenzako mshangilie? Sasa unaposema uchumi utakuwa mzuri ni kuanzia mwaka kesho tutakapoacha kuvaa mitumba?
nje ya wigo wa kinachojadiliwa
 
Tatizo wa Tanzania tunapenda kulalamika bila kuwa na sababu. Nani aliitoa hela ya Tanzania toka noti ya shs 100 mpaka noti ya shs 10,000
Je hapo uchumi ulipanda au ulishuka??
We hujui lolote! Hata sasa uchumi unakua kwa asilimia 7+,na hiyo hazijaanza kipindi hiki cha magufuli,ukuaji wa uchumi umetokea mbali sana! Tofauti ni kuwa kipindi cha mr dhaifu uchumi ulikuwa ukipanda kwa 7.1 % na mzunguko ulikuwa mzuri! Ila sasa ukuaji wake upo chini zaidi na mzunguko upo hoi!!kumbuka pia ukubwa au udogo wa sarafu si issue as long as ipo constant/certainity!! Kile tunachopata kutoka kwenye uchumi is all that matter!! Sasa kama hakuna unachokipata kwenye uchumi mkubwa na ambacho ulikuwa unakipata kwenye uchumi mdogo funga,usali na kumuuliza Mungu kosa lako nini!
 
“Ninapowaeleza kuwa uchumi wetu ni mzuri, ni mzuri kweli kuwa na uchumi mzuri hauna maana kuwa na mahela umeyajaza chumbani. Uchumi ni pamoja na kuwa na hela ngumu kuipata, kizuri hakipatikani hovyo hovyo, ni lazima utoe jasho. Nilikuwa nazungumza juzi pale Mwanza kuwa bajeti ya Afya imepanda kutoka bilioni 31 hadi bilioni 269 na Tanzania tukapewa nafasi ya kuuza madawa katika nchi zote za SADC.“amesema Rais Magufuli Tarehe 6 Novemba 2017 mkoani Kagera wakati wa ufunguzi wa mradi wa wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba, mkoani Kagera.

Chanzo: Bongo 5
Chizi wetu karogwa tena.
 
Kila nikikumbuka kale kagodoro alikokalia Magufuli kule kwao Chato hapa juzi kati. Sioni tena wepesi wa kupata pesa hata ipande thamani mara 50.
 
Jamani ukweli ni kwamba tufanye kazi ili zituletee kipato cha kuendana na mazingira.

Pia naishauri serikali iliangalie suala la kodi kwa raia wake. Jodi ziendane na upatikanaji wa pesa. Sio upatikanaji wa pesa ni mgumu, alafu ukiipata yote inaishia kwenye matumizi. Hii ni mbaya kwani kwa nijuavyo mimi, ni muhimu sana kujiwekea akiba.

Najua hakuna anayepata hela pasipo kufanya kazi. Ila zama zimebadilka. Kipindi hiki unafanya kazi ngumu alafu ujira kidogo. Wakati vipindi vilivyopita, unafanya kazi nyepesi alafu ujira wa kutosha. Ndio maana hela ilikua na mzunguko mzuri kiasi kwamba uliwanufaisha mpaka wauza mchicha
 
Uchumi wa nchi haupimwi kwa hela kuwa na thamani kubwa au ndogo.

Unapimwa kwa uzalishaji.

China ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi, lakini hela yao haina thamani sana. Na kwa kweli serikali yao inapigania hela yaoisiwe na thamani, kwa sababu hilo linavutia exports.

Nchi isiyo na exports ikiwa na hela yenye thamani sana ni vibaya, ikiwa na hela isiyo na thamani sana ni vibaya pia.

Uchumi haupimwi kwa thamani ya hela, thamani ya hela inaweza kupangwa na serikali tu, by "fiat".

Uchumi unapimwa kwa uzalishaji.
Ni kweli uchumi unapimwa kwa uzalishaji,ambapo huzalishaji huo hupelekea thamani ya hela ya nchi husika kupanda!kusema uchumi wa nchi haupimwi kwa thamani ya fedha sio kweli sababu mazingira ya nchi kwa nchi yanatofautiana mfano china ana export sana bidhaa hivyo ni wazi kutokana na nguvu za demand na supply ktk soko la dunia ni lazima sarafu yao itapanda zaidi ya sarafu zingine.kwa kuwa china unahitaji kuuza zaidi ndio maana anaingilia sarafu yake.
unaposema serikali inaweza kupanga thamani ya sarafu zao sio mara zote hilo nalo inategemeana na mazingira kama ilivyo kwa china.Je leo unaweza sema B.O.T wanawaza kusema dola moja ya USA iwe sawa na Shilingi 1 ya Tanzania
 
Ni kweli uchumi unapimwa kwa uzalishaji,ambapo huzalishaji huo hupelekea thamani ya hela ya nchi husika kupanda!kusema uchumi wa nchi haupimwi kwa thamani ya fedha sio kweli sababu mazingira ya nchi kwa nchi yanatofautiana mfano china ana export sana bidhaa hivyo ni wazi kutokana na nguvu za demand na supply ktk soko la dunia ni lazima sarafu yao itapanda zaidi ya sarafu zingine.kwa kuwa china unahitaji kuuza zaidi ndio maana anaingilia sarafu yake.
unaposema serikali inaweza kupanga thamani ya sarafu zao sio mara zote hilo nalo inategemeana na mazingira kama ilivyo kwa china.Je leo unaweza sema B.O.T wanawaza kusema dola moja ya USA iwe sawa na Shilingi 1 ya Tanzania
Mimi napenda kuangalia fundamentals.

Fundamentals za uchumi wa nchi zinaelezewa kwa uzalishaji,sio kwa thamani ya fedha.

Nchi yenye kichwa ngumu ambayo inataka kuendekeza pride inaweza kuwa na sarafu yenye thamani kubwa na uchumi mbaya, sarafu yake yenye thamani kubwa haimaanishi uchumi wa nchi hiyo ni mzuri.

Na nchi yenye uchumi mzuri sana inayotegemea exports inaweza kufanya makusudi kabisa sarafu yakeisiwe na nguvu sana, ili kuchochea exports.

Kwa hiyo mtu kukwambia tu thamani ya sarafua ya nchi ni ya juu sana au ya chini sana, bila kuweka context ya production, imports, exports etc, anakuwa hajakuambia kitu chenye maana yoyote.

BOT wanaweza kusema dola moja ya US iwe sawa na shilingi moja, Zimbabwe wameprint a quasi currency wakasema hivyo.

Lakinihilo halimaanishi kwamba kwa kufanya hivyo uchumiwa Zimbabwe umeimarika.

Kwa hiyo, tunapozungumzia uchumi wa nchi, kitu cha msingi cha kuzingatia ni uzalishaji namauzo,si thamani ya fedha.

Thamani ya fedha inaweza kupanda au kushuka kwa fiat tu, kwakauli ya serikali.

Kuna serikali nyingi ziliona inflation kubwa zikaondoa zero kadhaa kwenye fedha zao.

Hilo halimaanishi uchumi ulipanda mara moja.
 
Back
Top Bottom