Rais Magufuli: Uchumi mzuri ni pamoja na kuwa hela ngumu kuipata; kizuri hakipatikani hovyo hovyo

Jamani ukweli ni kwamba tufanye kazi ili zituletee kipato cha kuendana na mazingira.

Pia naishauri serikali iliangalie suala la kodi kwa raia wake. Jodi ziendane na upatikanaji wa pesa. Sio upatikanaji wa pesa ni mgumu, alafu ukiipata yote inaishia kwenye matumizi. Hii ni mbaya kwani kwa nijuavyo mimi, ni muhimu sana kujiwekea akiba.

Najua hakuna anayepata hela pasipo kufanya kazi. Ila zama zimebadilka. Kipindi hiki unafanya kazi ngumu alafu ujira kidogo. Wakati vipindi vilivyopita, unafanya kazi nyepesi alafu ujira wa kutosha. Ndio maana hela ilikua na mzunguko mzuri kiasi kwamba uliwanufaisha mpaka wauza mchicha
Job creation inafanywa na serikali kupitia sera ya chama husika,huwezi kulazimisha watu wafanye kazi ambazo hazipo! au wewe unadhani watu wote wanao graduate kila mwaka ni wavivu wa kutaka kufanya kazi?? la hasha ni sababu kazi hazipo.
swala la unemployment ni tatizo namba la kiuchumi ktk kila nchi iliyo chini ya dunia ila Tatizo huli limezidi kwa asilimia kubwa kwa Nchi za ulimwengu wa 3 kutokana na sera mbovu za watu tunao wapa dhamana ya kutupa mwanga wa kutatua matatizo yetu
 
Mimi napenda kuangalia fundamentals.

Fundamentals za uchumi wa nchi zinaelezewa kwa uzalishaji,siokwa thamani ya fedha.

Nchi yenye kichwa ngumu ambayoinatakakuendekeza pride inaweza kuwa na sarafu yenye thamani kubwa na uchumi mbaya, sarafu yake yenye thamani kubwa haimaanishi uchumi wa nchi hiyo ni mzuri.

Na nchi yenye uchumi mzuri sana inayotegemea exports inaweza kufanya makusudi kabisa sarafu yakeisiwe na nguvu sana, ili kuchochea exports.

Kwa hiyo mtu kukwambia tu thamani ya sarafua ya nchi ni ya juu sana au ya chini sana, bila kuweka context ya production, imports, exports etc, anakuwa hajakuambia kitu chenye maana yoyote.

BOT wanaweza kusema dola moja ya US iwe sawa na shilingi moja, Zimbabwe wameprint a quasi currency wakasema hivyo.
maelezo ya hapo juu yote nakubaliana nawe ila hapa kwenye rangi niulize kama BOT wanaweza fanya hivyo kwa nini wasifanye kwa hela yetu ili dola 1 iwe sawa na Tshs 1??
 
maelezo ya hapo juu yote nakubaliana nawe ila hapa kwenye rangi niulize kama BOT wanaweza fanya hivyo kwa nini wasifanye kwa hela yetu ili dola 1 iwe sawa na Tshs 1??
Kwa sababu hilo, ceteris paribus, halitasaidia chochote katika kukuza uchumi, zaidi, hata kisaikolojia tu, litafanya uchumi usinyae.

Ndiyo maana China,uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, wanapigana na Marekani sana ili hela yao Wachina iwe na thamani ndogo. Timothy Geithner aliwasema sana, Trump anawasema sana kuhusu hili.

Wamarekani wanataka sana hela ya China ipande kwa market forces, China wanakataa, wanaiwekea vizuizi vya kiserikali.

Trump mwenyewe alikuwa analalamika USD iko very high, alikuwa anataka ishuke, kuchochea trade. Na imeshuka sana tu.

Kwahiyo hela kuwa juu au chini, bila kuweka context ya uzalishaji, haina maana yoyote.

Uzalishaji ndio unatuelezakwamba uchumi ni mzuri au mbaya. Ukishaanza na habari za uzalishaji, sasa hapo ndipo hela kuwa juu au chini inaweza kuwa factor.
 
Wakulima wa mbaazi wamefanya kazi kwa bidii matokeo yake bei imeshuka kutoka 2,000 kwa Kilo 205hadi 199 means huu
 
Basi achapishe NOTI ZA 5000, 1000, 500, 20 NA 10 Tsh. Pili arudishe time ya bei ili kuondoa mkanganyiko
 
Yani tunavyo changia ni kama vile Tanzania ni Taifa jipya lililodondoka kutoka sehemu flani ,kila Uongozi utakao ingia nao utakuwa ukihitaji Miaka 10 kujipanga na kukuza Uchumi sio ?..
Kwa hiyo ulitaka ukiamka tu siku ya pili ukute kila kitu kimesha badilika?
Mimi binafsi sochagui chama, nachagua kiongozi na sera. Kabla ya Magufuli kuteuliwa nilikua upande wa chadema, lakini kilichotokea katika wateuliwa wa pande zote ccm na chadema nikaona heri ccm. Hatuwezi tukamchukia kiongozi mpya wa ccm basi kwa sababu watangulizi wake walikua dhaifu. Anachofanya ni kitu ambacho ni tofauti sana tena sana na viongozi wa awali, kuna badhi ya makosa anayo fanya lakini tukitoa maoni yetu, na tukapaza sauti bila kua na lugha chafu nina uhakika atatusikiliza. Leo hii ana maadui wengi tu, wale wote waliokua wakitegemea wizi na ufisadi, matajiri waliokua wakitafuna nchi, tena wanatafuna hela za watu wa hali ya chini, wakwepa kodi wote hao.
Miki binafsi ninacho omba kwake kwa sasa ni vitu viwili avifanyie kazi. Kuboresha huduma ya afya na ainue kipato cha chini. Hapo hela itarudi kwenye mzunguko.
 
Yuko sahihi! Mfano soda ilikuwa inakimbilia 1000, sasa hivi imeshuka imekuwa mia tano
Nauli za dala dala zamani zilikuwa zinapanda kiholela lakini sasa ivi kuna muda zinashuka.

Kingine sasa hivi kodi za nyumba na vyumba zimeshuka na hamna ile kutoa kodi ya mwaka au miezi kumi kwasasa unaweza kulipia miezi mitatu na uka bargain kupunguziwa kodi tofauti na zamani.

Naunga mkono hoja na pongezi kwa mheshimiwa rais.
 
Job creation inafanywa na serikali kupitia sera ya chama husika,huwezi kulazimisha watu wafanye kazi ambazo hazipo! au wewe unadhani watu wote wanao graduate kila mwaka ni wavivu wa kutaka kufanya kazi?? la hasha ni sababu kazi hazipo.
swala la unemployment ni tatizo namba la kiuchumi ktk kila nchi iliyo chini ya dunia ila Tatizo huli limezidi kwa asilimia kubwa kwa Nchi za ulimwengu wa 3 kutokana na sera mbovu za watu tunao wapa dhamana ya kutupa mwanga wa kutatua matatizo yetu
Mwambie huyu,watu wamelima mbaazi vya kufa mtu, being imekuja 200 kwa kilo,serikali inefanya nini. Watu hawafanyi kazi vipi hapo
 
We hujui lolote! Hata sasa uchumi unakua kwa asilimia 7+,na hiyo hazijaanza kipindi hiki cha magufuli,ukuaji wa uchumi umetokea mbali sana! Tofauti ni kuwa kipindi cha mr dhaifu uchumi ulikuwa ukipanda kwa 7.1 % na mzunguko ulikuwa mzuri! Ila sasa ukuaji wake upo chini zaidi na mzunguko upo hoi!!kumbuka pia ukubwa au udogo wa sarafu si issue as long as ipo constant/certainity!! Kile tunachopata kutoka kwenye uchumi is all that matter!! Sasa kama hakuna unachokipata kwenye uchumi mkubwa na ambacho ulikuwa unakipata kwenye uchumi mdogo funga,usali na kumuuliza Mungu kosa lako nini!
Hahaha bora mimi nisie jua ila weww naona umechanganyikiwa. Endelea kufunga na kusali Mkuu
 
Ehee! Amefungia pesa kwenye kabati anafaidi yeye, bashite na mtoto wa dada afu anakuja na ngonjera za uchumi umekua
 
Toka kipindi cha kikwete ilikua tsh 2500 sema magu kaifanya iwe stable aishuki wala kupanda ovyo
 
Back
Top Bottom