...kosa kubwa tulilofanya kama taifa ni kukubali sera za IMF na World Bank. Hapo ndipo palikuwa mwanzo wa kufungwa pingu na wazungu. Hili pia liliendana na sisi kukubali liberalism na democracy. Hizi zote ni constructs za wazungu; inamaanisha hapo ndipo tulifunga ndoa kabisa na wazungu.
...kuna njia mbili za kufanya ili kufaidika kama taifa. Moja, ni kutumia mbinu na mikakati ya kuona namna gani tunafaidika katika hali hii iliyopo sasa. Hapa masuala ya sheria na uchumi yanachukua nafasi yake. Inahusu namna tunavyoingia mikataba ya uwekezaji na wazungu. Mikataba inabidi itengenezwe kwa terms zetu. Botswana wamefanikiwa sana katika hili. Sisi bado tunaingia mikataba nao kinyonge mno, as if hatuna kitu. Wao wana pesa na teknolojia, siye tuna maliasili. Hivyo, hapo ni 50-50, wala siyo 4-96 au 30-70!
Pili, ni kujitoa kwenye hizo pingu na ndoa. Hii ni extreme na radical way. Inahitaji kiongozi revolutionary, ila aliye smart kama Nyerere. Na Magufuli is quite the opposite, siyo revolutionary na wala smart. Kujitoa pia kutategemea na jinsi gani sisi kama taifa tupo tayari kwa aftermath ya kujitoa huko. Itakuwa balaa, maana tutagemea sanctions na isolations za kufa mtu. Itabidi tuwe katika hali ya kuweza kufanya deals kupitia South-South cooperation. Hili linawezekana, angalia uwepo wa BRICS (Brazil, India, China na ZA).
Kazi kwako Rais Magufuli!