Rais Magufuli, Punguza confrontation na Wazungu

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,143
3,222
Mh Rais Magufuli, ktk mambo mengi upo sahihi na kama ni makosa basi ni ya kibinadamu. Ila nafikiri kuna kitu ambacho wenda hujakipatia sawa sawa ama bado hujapata habari kwa usahihi wake.

Mosi, lazima tukubaliane na ukweli kabisa kwamba kutokana na mazingira halisi ya ulaya hawawezi kuishi kwa amani wasiponyonya kwa nguvu nchi za afrika na Karebean na uarabuni. Na hivyo, hakuna fair trade ktk vitu ambavyo wanavyovihitaji kuendesha maisha yao na kizazi chao, na ya kwamba ni lazima wachukue vitu kwa bure ama bei inayokaribia na hapo.

Cha mhimu kujiuliza je tuna nguvu za kuwasimamisha kivita ama ktk ku control financial system? Sasa tukipata majibu inabidi kuchukua tahadhari sahihi hasa tunapo deal na yalipo masilahi yao. Siyo kwamba naandika haya kwa sababu tunawaogopa ila hali halisi yenyewe inanisukuma kuandika haya. Wazungu wao wanasema "wako radhi kufanya kazi na shetani palipo na masilahi yao".

IMF, UN, World bank, mahakama za dunia na vyombo vya habari ni mali za wazungu. Na wazungu ni wamoja sana kupita kipimo. Hivyo ukizuia mali za wazungu, tuseme dhahabu, umezuia mali ya IMF ama World bank.Na hivyo hawa (IMF, World bank, UN, court zote)hawatakuja kufurahia hata kidogo, watakufanyia hujuma na kukwamisha karibu ktk kila kitu.

Maoni yangu, we have to know our place. Ya kwamba tu deal na mafisadi wetu, hawa mafisadi wa dunia jaribu ku negotiate nao objectively na wakati huohuo tukiangalia maeneo mengine yatoyotunyanyua ktk maendeleo. Kukwaruzana nao hasa ktk madini, wanaweza turudisha ktk nyakati za ujima. Hawa jamaa kwa hujuma wame qualify kwa kiwango cha juu sana.

Ushauri, kaa nao mezani mkubaliane nao amicably the way forward. Hiyo kamati uliounda hata wakikuta dhahabu wazungu wanaiba, na imejaa kwenye macontena, naamini kwenye vyombo vyao hawataandika wala kuonesha kwamba wazungu wanaiba africa. Wao watachokifanya ni ku potray wewe, wao wanavyotaka uonekane ktk jamii ya dunia. Again, chochote kamati uliyoiunda itakachokuta kwenye makontena kaa nao ukubaliane kwa mazungumzo mezani.
 
Vita ni vita mura...:mad::mad::mad:

Mkuu
Sidhani kama unaweza pigana vita ambayo wafahamu kabisa vita hiyo hutoshinda. Mie impression, niliyoiona kutoka kwa Rais japo ninaweza kuwa wrong , yani ya kwamba akiwakamata wazungu ktk wizi anafikiri " " wenda jumuia yakimataifa itamuunga mkono kwamba ana fight corruption vizuri, jibu ni BIG NO. Wazungu hawawezi kubali hiyo image at any cost, majibu yake itakuwa yeye ndo dikteta "he is killing his own people" something like that.
 
Wewe mleta mada ni hambwe ambaye huna hata robo ya UZALENDO.
Mkuu mtoa mada pamoja na mapungufu yake, andiko lake kuna mazingatio. Mifano ipo mingi tu. Wazungu ni watu wabaya, hao hao wanaohubiri demokrasia na uhuru wa kujieleza, ukienda kinyume nao watatafuta zengwe tu ili kukushughulikia.
Nakumbuka Hugo Chavez alikua mwiba kwa sera za kinyonyaji za WB, IMF et al.
Kilichofuatia wote tunakumbuka, alifuatwafuatwa hadi basi.
 
Tanzania ni zaidi ya Venezuela na Hugo Chavez mkuu. Soma alama za nyakati.
 
Hatukaribii hata robo ya venezuela na huu moto ukiwaka hatouweza

Ni suala la stratejia na mbinu stahiki. Ni kweli wazungu wanaishi kwa kunyonya mataifa masikini. Lakini tutaendelea kuitikia "hewala bwana" mpaka lini. Inabidi kuanzia mahali. Sidhani lengo la Magufuli ni kugombana na wazungu bali anajitahidi kuona kama TZ itaweza kupata a fair deal kwenye madini yetu badala ya kubakia kulalamikia mashimo baada ya migodi kufungwa.
 
Hii ni nchi yetu mwacheni jpm apige kazi na amalize mda wake wazungu hawana shukrani na hawana masilahi na nchi maskini isiyo na rasilimali hvyo hao watu ni majii kuliko hata wale tunaosema wanaiba hapa tz kwetu

Wanapaswa kubanwa hvyo hvyo ili wasichukue rasilimali zetu kijinga
 
Mh Rais Magufuli, ktk mambo mengi upo sahihi na kama ni makosa basi ni ya kibinadamu. Ila nafikiri kuna kitu ambacho wenda hujakipatia sawa sawa ama bado hujapata habari kwa usahihi wake.

Mosi, lazima tukubaliane na ukweli kabisa kwamba kutokana na mazingira halisi ya ulaya hawawezi kuishi kwa amani wasiponyonya kwa nguvu nchi za afrika na Karebean na uarabuni. Na hivyo, hakuna fair trade ktk vitu ambavyo wanavyovihitaji kuendesha maisha yao na kizazi chao, na ya kwamba ni lazima wachukue vitu kwa bure ama bei inayokaribia na hapo.

Cha mhimu kujiuliza je tuna nguvu za kuwasimamisha kivita ama ktk ku control financial system? Sasa tukipata majibu inabidi kuchukua tahadhari sahihi hasa tunapo deal na yalipo masilahi yao. Siyo kwamba naandika haya kwa sababu tunawaogopa ila hali halisi yenyewe inanisukuma kuandika haya. Wazungu wao wanasema "wako radhi kufanya kazi na shetani palipo na masilahi yao".

IMF, UN, World bank, mahakama za dunia na vyombo vya habari ni mali za wazungu. Na wazungu ni wamoja sana kupita kipimo. Hivyo ukizuia mali za wazungu, tuseme dhahabu, umezuia mali ya IMF ama World bank.Na hivyo hawa (IMF, World bank, UN, court zote)hawatakuja kufurahia hata kidogo, watakufanyia hujuma na kukwamisha karibu ktk kila kitu.

Maoni yangu, we have to know our place. Ya kwamba tu deal na mafisadi wetu, hawa mafisadi wa dunia jaribu ku negotiate nao objectively na wakati huohuo tukiangalia maeneo mengine yatoyotunyanyua ktk maendeleo. Kukwaruzana nao hasa ktk madini, wanaweza turudisha ktk nyakati za ujima. Hawa jamaa kwa hujuma wame qualify kwa kiwango cha juu sana.

Ushauri, kaa nao mezani mkubaliane nao amicably the way forward. Hiyo kamati uliounda hata wakikuta dhahabu wazungu wanaiba, na imejaa kwenye macontena, naamini kwenye vyombo vyao hawataandika wala kuonesha kwamba wazungu wanaiba africa. Wao watachokifanya ni ku potray wewe, wao wanavyotaka uonekane ktk jamii ya dunia. Again, chochote kamati uliyoiunda itakachokuta kwenye makontena kaa nao ukubaliane kwa mazungumzo mezani.
Mfano mzuri ni nchi ya Zimbabwe, baada ya Rais Mugabe kuwanyanganya mashamba leo hali ya uchumi wa nchi hiyo imekuwa mbaya sana, mfano mwingine ni Venezuela baada ya hayati Hugos Chaves aliyekuwa Rais wa nchi hiyo kutaifisha makampuni ya mafuta leo hii nchi hiyo pamoja na utajiri wa mafuta maandamano kila siku kutokana na hali mbaya ya uchumi, hawa wazungu walishusha bei ya mafuta kutoka dola 110 mpaka dola 50 ikawa ni vigumu kwa serikali ya Venezuela kuendelea kutoa huduma ilizokuwa inazitoa kwa wananchi wake
Mfano mkubwa ni wa hapa hapa Tanzania baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967 Rais wa awamu ya kwanza alitaifisha makampuni, mashamba, viwanda za hawa wazungu kilichofata walituhujumu kiuchumi mpaka Mwalimu aliamua kuondoka madarakani mwaka 1985. Chukua mfano mzuri hawa majirani zetu wa Kenya walivyopiga hatua kwa kuwa na ushirikiano na hawa wazungu. Tatizo ambalo serikali ya awamu ya tano iliyorithi ni mikataba mibovu iliyosainiwa na serikali ilizotangulia ambazo inatambuliwa kimataifa.
 
Yule Hugo Chavez alikuwa na jeuri ya mafuta lakini bado alichutama kwa wazungu,ingia nao mikataba ukiwa na akili zako timamu,ulisaini halafu baada ya miaka kadhaa unaanza kuwaletea figisu!!watakumaliza wako very smart katika hilo utaburuzwa kwenye mahakama ya biashara ya kimataifa hadi uchanganyikiwe.
 
Back
Top Bottom