Rais Magufuli, Punguza confrontation na Wazungu

Rais Magufuli, Punguza confrontation na Wazungu

Ukitaka usitake utafata ya kwao tu, ni heri kutumia diplomasia kupunguza makali.
Lakini yapo mataifa yanaeza kuendelea na yakiwa tofauti na matakwa yao mfano North Korea, Cuba wao wanawezaje na wengine kushindwa?
 
Mie nafikiri na naamini ya kwamba kufahamu vulnerability (matobo) yako uliyonayo, ama kujifahamu sehemu gani uko vizuri na sehemu gani uko vibaya, hii si kwamba ni weakness ama ni woga ama hujitambui, bali hii ni ishara ya strength na mtu unayejitambua barbara. Na hii haina maana ya kumtia woga Rais ama kuabudu mzungu, bali ni kumhamasisha aifahamu tofauti ya ukweli(truth) na hali halisi (the reality on the ground) ili apate ku deal nao intelligently.

Ukiachana tu na bajeti wanayotuchangia, lakini hata mapato tunayokusanya sisi kwa asilimia kubwa ni wao ndo wanawezesha kupatikana, hii ni kwa sababu Meli zinazkuja bandarini ni zao, ndege zinazotua viwanjani kuleta watalii ni zao, na watalii ni wao, machine na vitendea kazi zinazotusaidia kukusanya hayo mapato ni vifaa vyao. Hata dhahabu, shaba ina bei kwa sababu ni wao ndo wanainunua.

Wao ndo wana control hadi makusanyo yetu ya ndani, wakitaka wanaweza amuaa tu meli kutotua habo bandarini, wakiamua ndege hazitui hapo kwetu, wakiamua hata machine ya kunyolea ndevu haitowezekana kununulika.
Tusijidanganye ya kwamba tuna "options", China siyo options. Wakiamua kwenye jumuia zao za kimataifa na kusema hakuna kuuza wala kununua kitu toka bongo, tutasota sana. China hana power yoyote, china anamtegemea Russia kufanya maamuzi yake na Russia ni wazungu wale, naomba unielewe hapa.

Issue ya Syria kwa mfano, ni kwa sababu ya migongano ya kimasilahi baina ya wazungu kwa wazungu, otherwise, Assad hana chochote pale. Na kwasasa nayeamua masilahi ya Assad na Syria ni mzungu Russia, naomba unielewe vizuri. Hata hivyo kwa mfano, russia alimuuzia syria na Iran mwaka 2008 zile silaha zile battery wazungu wengine wakamkataza Russia wakatia sanctions. Na Russia alitulia kwa sababu wakati huo hakuwa na tu nguvu, na kisha Russia akaenda kujipanga upya na alipoona amejiweza sasa kupambana ndo akarudi tena mwaka juzi.
Kifupi hatuna options, tunachotakiwa tu kwa sasa ni kutembea nao intelligently. Yes ni ukweli tunaibiwa, lakini reality on the ground ni tofauti.

Kinachotakiwa sasa, Rais atakachokuta humo kwenye makontena akubali matokeo ya kwamba tunaibiwa na akae nao kwenye meza ya mazungumzo wayamalize kwenye meza ya mduara.
 
Lazima wakuadhibu!Mnakubali vipi kuingia mikataba halafu baadae mnawageuka?Unadhani nani anaweza kukubali kudhulumiwa namna hii?
Unakubaliana nani,nawekeza mabilioni kwenye miundo mbinu ya mgodi,halafu ghafla unasema mmeshtuka?Kwa nini hamkushituka kabla ya kusaini?
Ni sawa na mtu kuposa mke,akaandaa arusi kubwa,akatoa mahari kubwa,halafu wakaishi na mume muda mfupi,kisha baba mkwe anaanza kudai malipo ya ziada kwa vile mwanae ni mzuri sana.Kama mume hataki,basi amuache!!Nyie ni wehu?Kwa nini mlikubali hapo awali?Mtachezea kichapo sana na wameshaanza kutokea Malawi
 
Hii nchi shida sana,raia vilaza,wabunge vilaza,mawaziri mabubu vilaza,executive ndio hvyi tena
 
Hii nchi shida sana,raia vilaza,wabunge vilaza,mawaziri mabubu vilaza,executive ndio hvyi tena

Issue siyo ukilaza, issue nikutambua hali halisi na kufahamu namna ya ku deal na hii hali halisi.
 
Bado nina amini kwenye madini Wazungu wanatuibia through mikataba na sio madini yenyewe; hili nilisemalo nina uhakika nalo; kama hatuamini hili basi tusubiri majibu ya tume ya profesa Mruma au sample alizochukua mhe waziri mkuu.
 
Lakini yapo mataifa yanaeza kuendelea na yakiwa tofauti na matakwa yao mfano North Korea, Cuba wao wanawezaje na wengine kushindwa?

Cuba na North Korea hazina maendeleo yoyote, usisikie.

Cuba walibana uhai wa Castro, sasa hivi wanaanza kidogo kidogo kufunguka wenyewe. North Koreaa huko usisikie, Raia wakipata upenyo tu wanakimbia nchi.

Raia wako taabani, halafu siasa zile za ujamaa hapa kwetu tulishazikataa.
 
Cuba na North Korea hazina maendeleo yoyote, usisikie.

Cuba walibana uhai wa Castro, sasa hivi wanaanza kidogo kidogo kufunguka wenyewe. North Koreaa huko usisikie, Raia wakipata upenyo tu wanakimbia nchi.

Raia wako taabani, halafu siasa zile za ujamaa hapa kwetu tulishazikataa.
Maendeleo yapo huezi linganisha na nchi nyingi za kiafrika, kule wameendelea hasa kwenye sayansi na teknolojia ingawa vikwazo vile viliwayumbisha kiasi.
Ndiyo maana nchi kama Cuba walieza kusaidia hata Tanzania madaktari wa Cuba wapo wengi tu janga la ebola ni Cuba walosaidia sana Afrika, North Korea vikwazo bado wamewekewa lakini wanapambana kuna mengi mazuri ya huko lakini ukiskiliza sana media za wamagharibi utaskia mabaya tu ya huko.

Halafu siku hizi kuna ujamaa ulioboreshwa tofauti na ule wa Nyerere.
 
Mh Rais Magufuli, ktk mambo mengi upo sahihi na kama ni makosa basi ni ya kibinadamu. Ila nafikiri kuna kitu ambacho wenda hujakipatia sawa sawa ama bado hujapata habari kwa usahihi wake.

Mosi, lazima tukubaliane na ukweli kabisa kwamba kutokana na mazingira halisi ya ulaya hawawezi kuishi kwa amani wasiponyonya kwa nguvu nchi za afrika na Karebean na uarabuni. Na hivyo, hakuna fair trade ktk vitu ambavyo wanavyovihitaji kuendesha maisha yao na kizazi chao, na ya kwamba ni lazima wachukue vitu kwa bure ama bei inayokaribia na hapo.

Cha mhimu kujiuliza je tuna nguvu za kuwasimamisha kivita ama ktk ku control financial system? Sasa tukipata majibu inabidi kuchukua tahadhari sahihi hasa tunapo deal na yalipo masilahi yao. Siyo kwamba naandika haya kwa sababu tunawaogopa ila hali halisi yenyewe inanisukuma kuandika haya. Wazungu wao wanasema "wako radhi kufanya kazi na shetani palipo na masilahi yao".

IMF, UN, World bank, mahakama za dunia na vyombo vya habari ni mali za wazungu. Na wazungu ni wamoja sana kupita kipimo. Hivyo ukizuia mali za wazungu, tuseme dhahabu, umezuia mali ya IMF ama World bank.Na hivyo hawa (IMF, World bank, UN, court zote)hawatakuja kufurahia hata kidogo, watakufanyia hujuma na kukwamisha karibu ktk kila kitu.

Maoni yangu, we have to know our place. Ya kwamba tu deal na mafisadi wetu, hawa mafisadi wa dunia jaribu ku negotiate nao objectively na wakati huohuo tukiangalia maeneo mengine yatoyotunyanyua ktk maendeleo. Kukwaruzana nao hasa ktk madini, wanaweza turudisha ktk nyakati za ujima. Hawa jamaa kwa hujuma wame qualify kwa kiwango cha juu sana.

Ushauri, kaa nao mezani mkubaliane nao amicably the way forward. Hiyo kamati uliounda hata wakikuta dhahabu wazungu wanaiba, na imejaa kwenye macontena, naamini kwenye vyombo vyao hawataandika wala kuonesha kwamba wazungu wanaiba africa. Wao watachokifanya ni ku potray wewe, wao wanavyotaka uonekane ktk jamii ya dunia. Again, chochote kamati uliyoiunda itakachokuta kwenye makontena kaa nao ukubaliane kwa mazungumzo mezani.

Vita hii lazima ianzie somewhere! hatuwezi kuacha tu hali hii iendelee milele kama wewe mtoa post unavotaka watu kama wewe ndo walikuwa masnich kwenye harakati za kupinga ukoloni na wale wazee wangewafuata mpaka leo ungekuwa unalima mahindi na kulisha mifugo huko America na kwingineko!! tunakosa nini kwa mfano? muda mwingine ujasiri wako ndio mtaji wako usiwe na nidhamu ya woga kijana
 
Vita hii lazima ianzie somewhere! hatuwezi kuacha tu hali hii iendelee milele kama wewe mtoa post unavotaka watu kama wewe ndo walikuwa masnich kwenye harakati za kupinga ukoloni na wale wazee wangewafuata mpaka leo ungekuwa unalima mahindi na kulisha mifugo huko America na kwingineko!! tunakosa nini kwa mfano? muda mwingine ujasiri wako ndio mtaji wako usiwe na nidhamu ya woga kijana

Tatizo siyo nidhamu ya woga , tatizo ni hali halisi ya kwamba kupigana lazima tupigane intelligently, otherwise tutaendelea kuimba nyimbo zile zile.
Ukoloni ule wa physically ni wao ndo waliamua kutuachia tu kwa sababu ulikuwa ukoloni ambao siyo economical kwao kama modern ukoloni wa sasa unavyowapa faida nzuri. Na pia ni wao ndo waliamua ku abolish utumwa kwa sababu physical utumwa haukuwa economical kama modern slavery ya sasa. Usidhani uko huru ndugu yangu, upo ktk ukoloni mzito kupita ule wa babu zetu. hivyo kinachotakiwa ni kutumia akili kuondokana nao na si kutumia mabavu.
 
Na hii haina maana ya kumtia woga Rais ama kuabudu mzungu, bali ni kumhamasisha aifahamu tofauti ya ukweli(truth) na hali halisi (the reality on the ground) ili apate ku deal nao intelligently.
Ningependa haya maneno yajirudie mara 1000 kwenye masikio ya mkulu pengine atalielewa hili somo.
 
Stop this cheap talk. Mlisema hamuhitaji fedha zao. What happened? Bajeti ya Maendeleo mpaka sasa ni asilimia 37 tu!! You know what that mean?? Muachage kutukana wakunga kabla hamjavuka mito.
 
Stop this cheap talk. Mlisema hamuhitaji fedha zao. What happened? Bajeti ya Maendeleo mpaka sasa ni asilimia 37 tu!! You know what that mean?? Muachage kutukana wakunga kabla hamjavuka mito.

Hatuhitaji fedha zao, lakini pia hatuhitaji confrontation nao. Tofautisha hivi vitu viwili ni sawa na usiku na mchana.
Nikama Iran ama Syria, hawahitaji pesa zao ila wanakaa nao mezani kupunguza confrontation, Iran wanajua walivyokuwa imewa hit hard.

Ku avoid confrontations si kwamba unataka umsaada, kwamba umetukana mkunga. Nafikiri kama unajibu hapa utakuwa una refer maada ambayo siyo sahihi, labda kwa fundo lilokukaa siku nyingi. Labda kwa kukusaidia tu confrontation iliyopo sahivi ni Russia Vs NATO over Syria or over Ukraine. siye bifu hilo hatuwezi hata moja ya 2000.
 
Sioni kama ushauri wako wa kulamba miguu ya Wazungu ni sahihi sana kwa vile tu wana nguvu ya kiuchumi na kijeshi. Kujiamini na kujitetea kwanguvu zote ndilo jambo muhimu zaidi kuliko vyote. JPM aendelee kukaza uzi na sisi tumuunge mkono.
Siwezi kuunga mkono, so long as we are not doing it intelligently.
 
Mkuu treborx
You are grand, and goodbye.
 
Sioni kama ushauri wako wa kulamba miguu ya Wazungu ni sahihi sana kwa vile tu wana nguvu ya kiuchumi na kijeshi. Kujiamini na kujitetea kwanguvu zote ndilo jambo muhimu zaidi kuliko vyote. JPM aendelee kukaza uzi na sisi tumuunge mkono.

Mkuu siyo kulamba, you simply know your place. Kama ni nguvu kujitetea watu wengi wasingeajiriwa, maana zile ajira kwa asilimia 98% tulizonazo ni low wages na ni slavery type. Kwanini hujitetei kwa nguvu zote kuacha ajira yako mara moja, ni kwa sababu you know your place. Kujitetea ni process iliyo na mipango kabambe na siyo, kukurupuka tu unaacha ajira yako.

Mie naamini kwa asilimia kubwa, akija mzungu hapo na kampuni yake na mtanzania na kampuni yako wakatoa ajira asilimia kubwa watakimbilia kwa mzungu, ulishawahi kujiuliza ni kwanini?
 
MkamaP mzungu ni binadamu tu kama wewe, hupaswi kumuogopa binadamu mwenye akili na nguvu za kibinadamu.
Uliyoandika kwenye hii mada yako yanathibitisha kuwa shida ni inferiority complex iliopo kwa Waafrika wengi na ndiyo huu umaskini mkubwa ulowaganda na umejaa barani Afrika.

Huu ni umaskini wa kifikra na vile ni utumwa wa kifikra hakika ukiwa na mawazo kama ya mtoa mada huezi kuendelea milele na milele na Afrika haiendelei sababu ya hivi.

Hata kama huyo mzungu anaingia kuhatarisha uhai wako kwa haya uloandika utaendelea kupiga magoti na kusema acha aniue tu sababu ni mzungu!
Binadamu Mungu alikupa akili na nguvu hivi siyo mapambo anataka uvitumie upambane kwenye kipindi chote cha uhai wa maisha yako.

BADILIKENI KIFIKRA JAMANI MSIISHI NA FIKRA ZILIZOKUFA.

Mzungu ni mwanadamu ni kweli, na si muogopi na hiyo ni kweli pia. Ila inatakiwa process na mikakati na akili ya kukabiliana nao kiakili na si vinginevyo. Lakini ni ukweli usiopingika kwamba, kila kitu tunachotumia ni cha mzungu iwe kwa mawasiliano, kwenye ukusanyi mapato na kote hadi kalamu tunayotumia kuandika.

Hivyo mzungu huko aliko anaona mpaka chumbani wenda kwako, na anaweza zimisha machine yoyote iwe mhimbili, aghakan ama bugando at his will, hilo pia litambue. Na hivyo kama unataka kumpinga mzungu, mpinge intelligently. Kwanza nafikiri anza kuondoa matumizi ya vifaa vyake kidogo kidogo na utakapomaliza kabisa ama kuvibakiza kiduchu, hapo ndo utapata guts zenye tija sahihi.

Na si ajabu, huyo huyo mzungu akija na kampuni lake na likawepo kampuni jingine la mtanzania wakatangaza ajira, watu kwa asilimia kubwa watakimbilia kwa mzungu. It's not about inferiority complexity or umasikini wa fikra but it has got something to do with the reality on the ground. Achana na theory na masimuliza, just check the bits and pieces on the ground.
 
Wakileta longolongo tunaelekea mashariki ambao teknolojia yao imepanda sana.
 
Back
Top Bottom