Rais Magufuli: Mimi ni mzilankende muyango

Yaani watu ving'ang'anizi kwelikweli.
Kwenye hotuba yake alisema yeye ni muyango mzilankende, halafu watu wanalazimisha awe msukuma, msubi au mzinza.
MNA matatizo sana.
 
Ukoo wa abahinda pamoja na abazilankende umesambaa sana mkoa wa kigoma na wilaya zake za Kibondo na kakonko.Kama walivyo abagisho ambao ni abazilafundi wako Kibondo na wamesambaa sana maeneo ya Chato, Sengerema Geita, Katoro na Ushirombo.Nadhani huko Bukoba siyo sana, asili ya wazazi wa Rais Magufuri ni Kigoma kwa maana ya Muha na sio mrundi wala mnyarwanda.
 
Mimi binafsi siamini kama huyu jamaa ni mtanzania hasa tabia zake na ni mtu ambaye hana utu, huruma wala kauli nzuri, watanzania kiasili hatuko hivyo hata kidogo huwa tunajaliana sana pale panapokuwa na matatizo hata kama uwezo ni mdogo.... Bil. 17 za rambi rambi tena zilizochangwa na wasamaria wema zitumike kutengeneza miundombinu wakati wananchi hawana pa kulala ni ajabu sana! Mkwere wetu tunamkumbuka sana apart from everything alikuwa na huruma na utu!
Niliwaambia mapema kabla jk hajaachia kuwa mtumkumbuka, kwani kabla hajaja mtu mzuri huwezi kujua ubaya wa uliyenaye na kabla hajaja mbaya huwezi kujua uzuri wa uliyenaye.
Namkumbuka sana yule jamaa mbali na kaudhaifu chake hakawezi kufikia uzuri wa faru....means udhaifu wa jk ni afadhali kuliko unaoitwa uzuri wa faru j
 
Wayango, Wazilankende, wako kigoma - hapa mpaka yeye mwenyewe athibitishe wapi chimbuko lake
 
tapatalk_1477339656622.jpeg
 
Basi sawa,tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili tupunguze idadi ya ombaomba mitaani
 
Bila kwenda ndani sana ambako mengine si muhimu. Magufuli ni MCHANGANYIKO wa damu kadhaa MIXED BLOOD.
Ana damu ya KISUKUMA na ana damu ya makabila mengine baadhi ya hayo hapo juu.
Wasukuma huwa HAWANA HASIRA kali Magufuli ni MKALI SANA na mwepesi wa KUKASIRIKA!
Hiyo SI hulka ya WASUKUMA! Wasukuma ni WAPOLE!

ACCENT/ LAFUDHI ya Magufuli si PURE KISUKUMA ukimsikiliza kwa makini ana Lafudhi tofauti. kwa sababu ya DAMU mchanganyiko!

Japokuwa Magufuli anakizungumuza Kisukuma vizuri sana lakini si Msukuma kamili.
Japokuwa familia yake the MAGUFULIS huongea KISUKUMA wakiwa nyumbani bado yeye si PURE Msukuma.

Kama ILIVYO KAWAIDA ya Watanzania wengi, Tuko MIXED blood hakuna aliye PURE kabisa labda wa kule ndani sana.
Hata hivyo ukifuatilia BLOODLINE/UKOO utakuta watu wengi si PURE/ KAMILI katika kabila lake

hata Magufuli ni kama WEWE na MIMI. HUO ndo UZURI wa nchi ya Tanzania INTERMARRIAGE /KUOANA makabila tofauti zimevunja UKABILA.

Labda tu umebaki kwa makabila wachache sana WANAOJIBAGUA na KUOANA wao kwa wao!
INTERMARRIAGE kuona nje ya kabila lako kumeisadia Tanzania. Kwa hilo NAJIVUNIA nchi yangu Tanzania!
hizi "identity politics" hivi zina uhusiano gani na utaifa wetu kama siyo kuudhoofisha?
 
Nafikiri naweza kuwa nimekupata.Na ninakubaliana nawe kuwa
Identity Politics/Ethino-Politics hudhoofisha UTAIFA!
Ni Kweli, Ndio maana Julius Nyerere aliliona hilo akaamua kutozipa nafasi siasa hizi za chimbuko na ukoo,badala yake akavalia njuga Utaifa ambao tunajivunia leo. Bila uamuzi wake huo tungekuwa na zile polities za zamani ambapo baadhi ya mikoa au majimbo yalikuwa chini ya utawala wa machifu,wami,mukama,mangi mwene na kadhalika.Matatizo yaliyoko S.Sudan,Burundi,Rwanda,DRC na Nigeria ni haya haya ya ukoo mmoja kuwa watawala. Ni vizuri kujitambua kuwa unatoka kabila gani na ukoo wako ni upi na alama yenu ni ipi ila isizidi sana hadi kuingilia utaifa,ingawa utaifa umekuja na kuzikuta zile tawala za kimila.Tutekeleze tulichokubaliana kuwa.
 
C&P
::Wazilankende::
Somo la leo la historia ni Wazilankende!
Juzi juzi Mheshimiwa mkulu alipopitia Bukoba pamoja na masimango na kejeli zote vile vile alijinasibu kwamba yeye ni Muyango yaani "abayango" hujiita Wazilankende.
Abayango aka Wazilankende ni moja ya koo kubwa kanda ya ziwa, kiutamaduni Wazilankende ni ukoo wenye kuheshimu sana enkende (kwa kiswahili enkende ni Ngedere) - hawa Wazilankende wanawachukulia ngedere kama ni ndugu zao au sehemu ya ukoo wao kwa hiyo Muyango (Mzilankende) hata akiwaona ngedere njiani inatakiwa awazawadie ndizi, akikuta ngedere amekufa inabidi alie au anaumwa inabidi amsaidie, hao ndo Wazilankende .

Je Wazilankende wanapatikana katika sehemu gani?
Ukweli ni kwamba kama ukisoma historia utakuta koo hizi zinapatikana katika maeneo ya nchi za Uganda (Banyankole, Bachiga, Batoro, Baganda, and Banyoro), RWANDA, Burundi na Tanzania (Wahaya, Wanyambo, Waha, WASUBI, Wazinza, Wakerewe na Waangaza).
Lakini ukweli ni kwamba hakuna MSUKUMA yoyote anaweza kuitwa Muyango Mzilankende, hicho kitu Usukumani hakipo.

Huko nyuma niliwahi kuandika makala ifatayo (copy and paste)

::Uwakiki wa asili? - Kumbe Mungai ni Mkenya? ...

"Tunae Joseph Mungai ambaye asili yake ni huku (Kenya) lakini kule kwetu alipewa nafasi nyeti, akawa mbunge hadi Waziri. Tena amewahi kuwa hadi Waziri wa Elimu" - John Pombe Magufuli, Kenya

Haya maneno ya Mh. Rais yamenistua....

Hivi kama Mungai asili yake ni Kenya, lakini amezaliwa Mufindi na yeye ana kuwa Mkenya? ...Je na yule mwenye asili ya Rwanda aliyezaliwa Biharamulo, anakuwa Mnyarwanda? Au yule Mwenye asili ya Kihindi lakini alizaliwa Kisutu nae ni Muhindi?

Where do we draw the line?

Je tunaulizana asili na makabila tunataka kutambika? Kama alivyojisemeaga baba wa Taifa.
Yeye alikuwa Mzanaki na hakuwahi kujita Mkurya, Mkwere alikuwa 'very proud' na hakujifanya Mzaramo, na yule wa Masasi haku-'pretend' kuwa Mmakonde.
Sasa ni vipi leo Mzinza au Msubi analazimishia sana Usukuma? Kulikoni?

Msema kweli ni mpenzi wa 'mungu' ...

Anyway doesn't real matter sio wakati wa kutambika huu na wote ni Watanza....Giza oops Nia.

[HASHTAG]#Mzilankende[/HASHTAG]
[HASHTAG]#PombeSioChai[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Twafa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#UsirudieKosa2020[/HASHTAG]
 
Ukifika Rwanda kunakile wenyewe huita Gakondo hii ni kama vile koo. Huko Rwanda kunaukoo wa Abhazilakende.

Sasa kama mkulu ni Mzilankende basi ni hatari.
Hii inapasa aseme ni Mzilakende kivipiii maana kusema yeye ni Mzilakende ni kukataa kuwa yeye so Msukuma.
Any Kunawazilankete hata Ukerewe na Mara/ujitani.
 
Ukifika Rwanda kunakile wenyewe huita Gakondo hii ni kama vile koo. Huko Rwanda kunaukoo wa Abhazilakende.

Sasa kama mkulu ni Mzilankende basi ni hatari.
Hii inapasa aseme ni Mzilakende kivipiii maana kusema yeye ni Mzilakende ni kukataa kuwa yeye so Msukuma.
Any Kunawazilankete hata Ukerewe na Mara/ujitani.


Soma haka kakipande nimekaokota kwenye hadithi moja ya MTU anaitea Alex Kimenyi

"Abega and Abakono who share the same totem the frog, Abacyaba and Ababanda whose totem is the hyena and Abazigaba and Abenengwe whose totem is the leopard are probably moieties, groups with a common ancestry who split into two. Abanyiginya, Abasindi and Abatsobe would be a phyratry : a social group which was divided into three separate clans.
There is a possibility also that Abahinda whose totem is inkende ‘squirrel’ and who were the reigning dynastly in Karagwe, Tanzania before immigrating to Rwanda for unknown causes, might be related to Abazirankende, a subclan of Abagesera whose totem is the wagtail. Abazirankende means ‘those for whom the squirrel is a taboo’.
The only clans whose totems are not known are Abanyakarama"
 
Kikabila cha kwako kitafutika! Actually people now are coming to their roots!
Sio kikabila changu tu. Huo ndo ukweli.

Huu mchanganyiko wa leo huu makabila yanabaki kwenye nyimbo za harusi tu na kijijini. Wengi waliozaliwa mjini wanatag za makabila, lugha wanajua robo, mila robo. Mjini now ni karibu 20 percent sasa.

Vijijini wanajiona ni failure hawana influence kwa ndugu zao wa mjini.

Hizi dini za waarabu na wazungu ndo kabisa walishatugeuza na majina kabisa sasa huo utambulisho wa makabila baada ya vizazi vinne utabaki kwenye passport.
 
Soma haka kakipande nimekaokota kwenye hadithi moja ya MTU anaitea Alex Kimenyi

"Abega and Abakono who share the same totem the frog, Abacyaba and Ababanda whose totem is the hyena and Abazigaba and Abenengwe whose totem is the leopard are probably moieties, groups with a common ancestry who split into two. Abanyiginya, Abasindi and Abatsobe would be a phyratry : a social group which was divided into three separate clans.
There is a possibility also that Abahinda whose totem is inkende ‘squirrel’ and who were the reigning dynastly in Karagwe, Tanzania before immigrating to Rwanda for unknown causes, might be related to Abazirankende, a subclan of Abagesera whose totem is the wagtail. Abazirankende means ‘those for whom the squirrel is a taboo’.
The only clans whose totems are not known
 
Back
Top Bottom