Hicho Kizinza hata hakijui na mara zote tangu wakati wa Kikwete na kipindi chote cha kampeni alipofika kwenye vijini vya Wazinza wilaya ya Sengerema alikuwa anaongea Kisukuma. Ukweli ni kuwa Magufuli ni Msukuma.
Kabila la Wasukuma ni kubwa na hakuna ambaye ukoo wake haujatokana na kabila jingine. Kuna Wasukuma waliotokea visiwa vya Ukelewe na kwingineko, mfano muna koo za Watimba, hawa wapo Wasukuma, Wajita, Wakerewe nk. Lakini kabila la mtu ni lile alilozaliwa akakuta wazazi wanaliongea.
Wakati wa kampeni alipokuwa Misungwi alisema babu yake aliishi pale mpaka uzee wake. Tusijidanganye, Magufuli ni Msukuma.
Na watu wengi sana wamebadili makabila yao na kuwa Wasukuma kutokana na eidha kuoa Wasukuma au muolewa. Wengi waliooa kwa Wasukuma vizazi vyao vimebadilika na kuwa Wasukuma.