MWANAHARAKATI MWEMA
Senior Member
- Dec 16, 2022
- 192
- 270
Kwanza kabisa namshukuru' muumba Kwa kuniweka hai mpaka Leo ninapofanikiwa kuwaona wanaochukia ukabila wa magufuli lakini wao kupitia chuki zao wakiungana Kabila moja na kutunga kitabu kinachozungumzia upande mmoja wa shilingi wa aliyoyatenda wanayemjadili.
Nikienda kwenye mada moja Kwa moja Ni kwamba tumeshuhudia wazilankende walioungana wakizindua kitabu kilichopewa Jina la 'IAM THE STATE'
ambacho Kwa wazi kabisa walioshiriki kukitunga wanajitambulisha kama wanahabari.
Ndani ya kitabu hicho kinachoonesha wazi kukosa weledi wa uandishi wa habari Kwa kuamua Kwa makusudi kutaka kuharibu kabisa legancy ya JPM na kukosa balance ya kuwauliza wenye nchi ambao ni wananchi Ni kiashiria cha ubabaishaji hasa Kwa Sababu wananchi walipaswa wapewe nafasi.
Kwanini nasema waandishi wanatakiwa wapelekwe mahakani Ni Kwa Sababu kitabu hicho kimetungwa si Kwa faida ya watanzania wote bali ni Kwa wale tu walioguswa Kwa Namna moja au nyingine kutokana na utekelezaji wa Sheria na kulinda maslai ya nchi.
Kitabu hiki kimejaa chuki za wazi wazi kabisa, hivi unawezaje kumzungumzia mtu Kwa mabaya tu alafu useme unalikomboa taifa, ukitaka kumjadili mtu mfanyanye kama unapika ugali ili kila upande ujifunze kupitia mazuri na mabaya yake.
Ombi Kwa familia ya magufuli Kwa niaba ya wananchi wengi tunaoamini kupitia utawala wa maliza Kero papo hapo ambao rais wetu kipenzi walio wengi tunaoamini Kwa vitendo Ni KWAMBA WALIOTUMIA PICHA YA MAGUFULI KUTANGAZA KITABU CHAO WAPELEKWE MAHAKAMANI.
Mwisho japo nilitamani niendelee kuna mambo mengi yamefanywa na Marais waliopita, yapo mabaya na mazuri lakini hakujawahi kutungwa kitabu cha kumlenga mtu moja Kwa moja lakini hawa wazilankende kisa tetemeko wanadhani itakuwa rahisi kufuta legancy ya jiwe JPM ilihali vitu alivyovifanya bado vipo na vitaishi milele, MAGUFULI BADO YUPO MIOYONI MWETU.
--
Pia soma
- From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)