mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Rais Magufuli akiwa katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na mabalozi Ikulu leo, amesema kwamba kuna mambo mengi yamezungumzwa na tuyapuuzie. Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia alikuja hapa, mwaka jana, kwahiyo wanatoa pesa wakijua sisi Tanzania tuna misimamo gani na tunafanya nini, hao wengine ni wapiga kelele tu, wala msiwajibu kwasababu watu wa namna hiyo hawaishi duniani.
Awali wiki iliyopita, zilikuja taarifa kwamba Benki ya Dunia WB imesema inafikiria uwezekano wa kuikopesha Serikali ya Tanzania mkopo wa dola za kimarekani milioni 500 sawa na Trilioni 1.152 za Kitanzania kwa ajili ya kuboresha sekta ya Elimu, mkopo uliokuwa umesimamishwa na benki hiyo kutokana na Rais Magufuli kutangaza kuzuia wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kutoendelea na masomo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, benki ya Dunia imedai kuwa ilipokea barua kutoka wanaharakati kutoka nchini Tanzania ambao walieleza kuwa, Benki ya Dunia kuendelea kutoa mkopo huo ni kuendelea kuwabagua wanafunzi kwa kigezo cha waliojifungua, wenye ujauzito na wasio Wajawazito.
Hivyo walitaka benki hiyo kusitisha mkopo huo tangu mwaka 2018, mpaka serikali itakapobadili sera yake ya kumzuia mwanafunzi aliyepata mimba kuendelea na masomo.
Pia soma > Tanzania yaweza kukosa Mkopo wa Dola Milioni 500 kutoka Benki ya Dunia