Rais Magufuli: Benki ya Dunia wanatoa pesa wakijua Tanzania tuna msimamo gani na tunafanya nini, wapiga kelele wapuuzwe

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
RAIS.jpg

Rais Magufuli akiwa katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na mabalozi Ikulu leo, amesema kwamba kuna mambo mengi yamezungumzwa na tuyapuuzie. Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia alikuja hapa, mwaka jana, kwahiyo wanatoa pesa wakijua sisi Tanzania tuna misimamo gani na tunafanya nini, hao wengine ni wapiga kelele tu, wala msiwajibu kwasababu watu wa namna hiyo hawaishi duniani.

Awali wiki iliyopita, zilikuja taarifa kwamba Benki ya Dunia WB imesema inafikiria uwezekano wa kuikopesha Serikali ya Tanzania mkopo wa dola za kimarekani milioni 500 sawa na Trilioni 1.152 za Kitanzania kwa ajili ya kuboresha sekta ya Elimu, mkopo uliokuwa umesimamishwa na benki hiyo kutokana na Rais Magufuli kutangaza kuzuia wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kutoendelea na masomo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, benki ya Dunia imedai kuwa ilipokea barua kutoka wanaharakati kutoka nchini Tanzania ambao walieleza kuwa, Benki ya Dunia kuendelea kutoa mkopo huo ni kuendelea kuwabagua wanafunzi kwa kigezo cha waliojifungua, wenye ujauzito na wasio Wajawazito.

Hivyo walitaka benki hiyo kusitisha mkopo huo tangu mwaka 2018, mpaka serikali itakapobadili sera yake ya kumzuia mwanafunzi aliyepata mimba kuendelea na masomo.

Pia soma > Tanzania yaweza kukosa Mkopo wa Dola Milioni 500 kutoka Benki ya Dunia
 
Mimi nashangaa sana waandamizi serikalini kwa kurumbana na wanaharakati wakati wanachotakiwa ni kufanya mawasiliano ya karibu na watoa pesa ambao ni Benki ya Dunia!

Kazi ya msingi ya waandamizi serikalini ni kuhakikisha wanafanya linalowezekana ili maombi ya mkopo yakubaliwe. Kukubaliwa kwa maombi yao ya mkopo itakuwa ni jibu lao kwa wanaharakati na sio kupigizana kelele!

Please, focus on the World Bank and the rest will take care of itself!
 
Ni kweli wapiga kelele wapuuzwe tu hakuna namna, wewe unapiga kelele na bado serikali hiyo hiyo inakuhudumia,unaishi kwa amani pamoja na njaa yako na shida zako lakini bado tu unapiga kelele,usaidiweje sasa?

nitarudi baadae
 
Back
Top Bottom