Rais Magufuli awataka TRA kuacha kubambikia wafanyabiashara kodi, asema wanakadiria kodi kubwa ili wapewe rushwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,977
Rais Magufuli ameitaka TRA kuacha kuwabambikia kodi wafanyabiashara na badala yake watoe makadirio ya haki.

Rais Magufuli amesema tabia ya kubambika kodi inawafanya wafanyabiashara washindwe kulipa na kutafuta njia za kukwepa kabisa kulipa.
Rais Magufuli amesema baadhi ya watumishi wa TRA wamekuwa na tabia ya kutoa makadirio makubwa na baadae kuomba wapewe rushwa ili wayapunguze.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Vita kati ya wafanyabiashara na TRA haitaisha kamwe kwa sababu zifuatazo.
1. Wafanya biashara wengi hasa wadogo na wa kati hawajui sheria za kodi.

2. Wafanyabiashara wengi hasa wadogo na wakubwa hawana rekodi sahihi za mapato, matumizi na faida. Yaani hawana vitabu vya hesabu. Jambo hili linasababisha ugumu katika kukokotoa kodi.

3. Mfumo wa TRA wa sasa wa EFD ni dhaifu. Una rekodi mauzo tu, hauruhusu wafanya biashara kuweka matumizi. Hauwezi kukadiria kodi kwa mauzo tu.

4. Mianya ya ukwepaji kodi ni mingi kutokana na mfumo wa biashara kuwa holela. Huwezi ku control wachuuzi kwa mamilioni waliopo sasa hivi.

5. Mfumo wa kodi una shida. Kuna ubaguzi baina ya wafanyabiashara. Mangi hama efd wala si VAT registered, mchuuzi wa barabarani hana efd wala si VAT registerd, lakini mwenye duka kubwa ana efd ni VAT registered. Wote wanauza biadhaa zinazofanana. Huyu mwenye EFD na VAT registered wakifuata sheria watakuwa ghali kuliko hao ambao si VAT registerd na hawatauza.

6. Huduma nyingi za kibiashara hazina risiti. Kwa mfano wewe kama una duka, ukinunua bidhaa kariakoo, unazipeleka mbagala utakodi kirikuu. Ila mwenye kirikuu hatakupa risiti. How do you account for that transanction. Same kwa nyanya na nyama kama una hotel. au ukioanda dala dala kwenda kuchukua mzigo hupati risiti ya TRA.

Nini kifanyike:

1. Badala ya ku categorise wafanya biashara kwa volume ya mauzo hawa ndo wawe VAT register au la. Classification ifanywe kwa aina ya bidhaa. Kwa mfano bidhaa za kila siku ambazo zinauzwa kwa mangi maduka ya aina hiyo yasiwe VAT registered. Lakini bidhaa zingine zote bila kujali ukubwa wa biashara wawe VAT registered.

2. Mfumo wa EFD utoe uwezo wa kurekodi matumizi ya biashara. Ili jioni unapopeleka taarifa uingize na matumizi ya siku hiyo. Kwa mfano uweke manunuzi ya mzigo uliofanya siku hiyo, pamoja na matumizi mengi kama usafiri, vibarua etc.

3. Kodi ikokotolewe kutokana na hesabu za mfumo ulioboreshwa.

4. Kutoa elimu ya kutosha. Kuwe na mtihani kabisa, kabla mtu hajapata leseni ya biashara ihakikishwe kuwa amesoma nankuelewa mfumo wa kodi kulingana na aina ya biashara anayotaka kufanya. Elimu elimu elimu.
 
Magufuli huwa anatengeneza tatizo watu wanaumia then anatafuta namna yakulitatua akisubiri pongezi!

Sera za kodi pamoja na sheria zake nchini sio rafiki kwa wajasiriliamali mambo yamekua magumu sana kwa sasa.TRA inatakiwa ibadili sera zake kwani zinaleta misuguano kati ya biashara moja na nyingine.
 
Vita kati ya wafanyabiashara na TRA haitaisha kamwe kwa sababu zifuatazo...
Upo sahihi kasoro sehemu moja tu. Kila mfanya biashara akisoma sheria za kodi haitasaidia maana huwezi kuwaza mzigo utaupata vipi kwa bei rahisi huku unawaza PAYE, WT,SDL,CT, PIT, Assessment, Provision n.k

Vijana wenye elimu ya fedha wajifunze kuhusu kodi, wafanyabiashara tujifunze kuwatumia hawa vijana kwa malipo.
 
Uko sahihi. Simaanishi wafundishwe wawe wataalamu. Ila wafundishwe ili waone umuhimu wa kuwatumia wataalamu. Just wapate ABC kujua compliance ina hitaji nini na nini kwa juu juu.
 
Nina kibanda eneo fulani changamfu leo nimeenda kukadiriwa TRA. Kibanda changu nalipia kodi 100,000 tra wananambia hiyo kodi haipo mtaa huo kwaiyo nimekadiriwa kuwa kodi yangu ni 300,000 huku sio kweli.

Nalipa laki kwahiyo kwa kipanda hicho napaswa kulipa mapato kwa mwaka 600,000 na kodi ya pango 360,000 jumla 960,000.... Kwanzia manager mpaka wasaidizi wake hawaja nielewa mpaka natoka pale.

Sasa hivi vilio tunapeleka kwa nani?
 
Rais Magufuli ameitaka TRA kuacha kuwabambikia kodi wafanyabiashara na badala yake watoe makadirio ya haki.

Rais Magufuli amesema tabia ya kubambika kodi inawafanya wafanyabiashara washindwe kulipa na kutafuta njia za kukwepa kabisa kulipa.
Rais Magufuli amesema baadhi ya watumishi wa TRA wamekuwa na tabia ya kutoa makadirio makubwa na baadae kuomba wapewe rushwa ili wayapunguze.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

This has been a general cry all over the country. Kuna watu naamini hawastahili kuwa TRA. Hawana nia njema kabisa na kuboresha mazingira ya biashara wala kuhakikisha sector binafsi inakua ili ajira ziongezeke
 
Shida ya TRA ni mindset hasi ya watendaji kwa wafanyabiashara, kufanya kazi kwa mazoea, kukimbizia malengo kwa hofu bila kueleza ukweli kuwa hayafikiki,kukosa ubunifu wa kupanua wigo wa kodi ili idadi kubwa ya wananchi washiriki kulipa kodi ya moja kwa moja direct tax na hususani kupunguza sekta isiyo rasmi. Mwisho kupenda Rushwa hususani vijana wasio na uzalendo. Kuna haja ya kuangalia upya sera,sheria na kanuni za kodi na tozo.
 
Njaa inapotangulia mbele, hapo hakuna namna haki itatendeka. Ninachoogopa ni wao kukosa kabisa uoga kumaliza biashara za watu kwa kodi zisizolipika. That is extremely worrying trend.
Mpaka Rais anasema, anajua nini kinaendelea nyuma ya pazia. Tubadilike. Kuna wakati nahisi wataanza kushika hela za moto in bog numbers.
 
Uko sahihi. Simaanishi wafundishwe wawe wataalamu. Ila wafundishwe ili waone umuhimu wa kuwatumia wataalamu. Just wapate ABC kujua compliance ina hitaji nini na nini kwa juu juu.
Kabisa boss. Upo sawa.
 
Back
Top Bottom