Rais Magufuli atahudhuria UN General Assembly Jumatatu?

Rais Magufuli atahudhuria UN General Assembly Jumatatu?

Kwani mmeshabadili mawazo kuhusu kumtaka aende Bukoba?
 
natamani aende ili akabanwe na waandishi wa habari wa kimataifa ambao hawezi kuwakimbia au kuchagua wa TBC kama hapa bongo , ataulizwa mambo ya Zanzibar, udikteta, demokrasi, uchumi wetu, rushwa, n.k
Swadaktaaaa nenda kote mashariki,magharibi,kusini,na kaskazini issue kuu ni hapo hao waandishi watakukimbilia hadi hotelini kwako lundo na makamera yao wakuhoji mambo uliyoyataja.
 
Humu mna ****** wengi sana,wanaodhani kujua kingereza ndio kua msomi,anaweza kwenda na akahutubia kwa kiswahili maana ni lugha ya kimataifa,Rais wa China akienda anahutubia kichina na wakalimani wapo sasa nyie mnaodhania kiingereza ndio elimu mjue mmetawaliwa bado fooool
Mkuu wewe tu unashindwa kuunganisha mambo mbona kama kutawaliwa,bado unatawaliwa!!!? bora uamue moja wekeni mitaala ya Kiswahili mwanzo mwisho vinginevyo kwa sasa mitaala yote sekondari na vyuo ni kwa kiingereza,sheria zote kwa kiingereza,vyeo vyote majeshini kwa kiingereza upooo???na yule anayebeba gongo lake pale mjengoni vipi sio ukoloni wa kiingereza??jumuiya ya madola mkuu wake ni malkia na mnaenda vepeeee??kubali mfumo wa elimu mbovu??huko darasani kemia angefundisha Kiswahili??kazi kwako.
 
UN UNARUHUSIWA KUTUMIA LUGHA YOYOTE..HATA KAMA MAGU ATATUMIA KISWAHILI TRANSLATOR MACHINE ZIPO...
SO HAKUNA WASI...
MBONA WARUSI WACHINA ETC WANAONGEA LUGHA ZAO..

OVA
anaogopa anaweza ulizwa lini ataanza peleka mitumba ulaya kutoka TZ
 
UN General Assembly inaanza Jumatatu Sept 19 2016. Hivi ni lazima Rais aalikwe kuhudhuria mkutano huo au huwa wanaenda tu?..Rais wa Nigeria atahutubia na ameshawa taarifu wananchi wake nini atahutubia. Nakumbuka hata Rais Mstaafu Mwinyi niliwahi kumshuhudia akihutubia..Sijui Mheshimiwa Magufuli atahudhuria na kuhutubia? Nafikiri Msigwa atatuhabarisha.
Duuuh, sijui kama atakwenda
 
Mbona watanzania hamna jema kipindi cha JK mlisema anasafiri sana kipindi hiki cha JPM ametulia hasafiri ovyo bado mnalalamika kua hasafiri sijui watanzania mnataka nini acheni kulalama ovyo..
Tatizo la nchi yetu ni hatuna viongozi wa wastani, JK alikuwa anasafiri mno na Magufuli hasafiri mno, Tunataka rais wa wastani.
 
Kule ataenda kuongea nn kisukuma? Kama sio kisukuma basi hawezi kwenda huku kiongozi wa wasukuma
 
Pia kujua kiingereza hakuzuii kufanya yote ulioyasema hapo juu....acha uvivu kijana hata marekan walipelekewa kiingereza na wanaongea mpk kesho...nchi za east africa zote wanaongea kuswahili plus lugha nyingne sa c watz tunataka kiswahili tuu!!!
Na hicho ndicho kilichotufanya kuwa WAJINGA, WASWAHILI NA WANAFKI hata ktk hiyo EA
 
Ndio maana kuna msemo unaosema; binadamu hawana jema.
Kikwete alikuwa anasafiri sana wakasema amezidi kusafiri akatungiwa majina mengi kiguu na njia mda wote anaruka angani Siku alizotumia kwa safari za nje ni nyingi kuliko alizotumia kukaa ofisini.

Kaja JPM asiyetaka kusafiri Mara kwa mara wanasema hajui kingereza,
Kweli nineamini upinzani wa tz una safari ndefu.
Kikwete kweli alizidi ameenda mpaka nchi zisizo na faida kwetu, lakini haimaanishi anayefuatie asishiriki mikutano yote e.g. AU, UNO, SADC etc

Hatuwezi kuwa kisiwa kila jambo ni kwa kiasi
 
Wiki iliyopita kulikuwa na mkutano wa umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote, (Non-Aligned Movement- NAM) uliofanyika kule Venezuela. Wakati wa vita baridi, mikutano ya NAM ilikuwa ya muhimu sana lakini tangu kuanguka kwa himaya ya USSR, mikutano hii imekuwa haina maana tena. Wiki hii vile vile kutakuwa na mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa pale New York ambapo viongozi wa nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa mataifa watapewa nafasi ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa na kuonyesha tambo zao. Maraisi wengi sana wa Afrika, ikiwa ni pamoja na Tanzania, hupenda kuhudhuria mikutano ya namna hiyo, yaani NAM na UN. Mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais, Mzee Mwinyi alihutubia baraza la Umoja wa mataifa akamwita Katibu Mkuu wa umoja huo wakati huo kuwa 'Javia Perezi di Kwela" badala ya "Havia Perez di Kweya". Kikwete, kama mzee Mugabe, hawajawahi kukosa mkutano wowote wa namna hiyo.

Magufuli vipi mwaka huu?
 
Akafanye nini kwani akienda huko itasaidia kuongeza ajira au kupunguza tatizo la madawati wilayani kwako,acha rais wetu atumikie watanzania ndiyo waliomchagua.
 
Back
Top Bottom