Wiki iliyopita kulikuwa na mkutano wa umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote, (Non-Aligned Movement- NAM) uliofanyika kule Venezuela. Wakati wa vita baridi, mikutano ya NAM ilikuwa ya muhimu sana lakini tangu kuanguka kwa himaya ya USSR, mikutano hii imekuwa haina maana tena. Wiki hii vile vile kutakuwa na mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa pale New York ambapo viongozi wa nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa mataifa watapewa nafasi ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa na kuonyesha tambo zao. Maraisi wengi sana wa Afrika, ikiwa ni pamoja na Tanzania, hupenda kuhudhuria mikutano ya namna hiyo, yaani NAM na UN. Mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais, Mzee Mwinyi alihutubia baraza la Umoja wa mataifa akamwita Katibu Mkuu wa umoja huo wakati huo kuwa 'Javia Perezi di Kwela" badala ya "Havia Perez di Kweya". Kikwete, kama mzee Mugabe, hawajawahi kukosa mkutano wowote wa namna hiyo.
Magufuli vipi mwaka huu?