Rais Magufuli atahudhuria UN General Assembly Jumatatu?

Rais Magufuli atahudhuria UN General Assembly Jumatatu?

UN General Assembly inaanza Jumatatu Sept 19 2016. Hivi ni lazima Rais aalikwe kuhudhuria mkutano huo au huwa wanaenda tu?..Rais wa Nigeria atahutubia na ameshawa taarifu wananchi wake nini atahutubia. Nakumbuka hata Rais Mstaafu Mwinyi niliwahi kumshuhudia akihutubia..Sijui Mheshimiwa Magufuli atahudhuria na kuhutubia? Nafikiri Msigwa atatuhabarisha.
Haendi hata siku moja, ng'o!!!!! sababu? ngeli!!!!!!
 
Humu mna vilaza wengi sana,wanaodhani kujua kingereza ndio kua msomi,anaweza kwenda na akahutubia kwa kiswahili maana ni lugha ya kimataifa,Rais wa China akienda anahutubia kichina na wakalimani wapo sasa nyie mnaodhania kiingereza ndio elimu mjue mmetawaliwa bado fooool
 
English shida kweli inasikitisha viongozi hata written speech wanaisoma kwa kusua sua. Samia ndio kidogo afadhali.Nimecheka sana Majaliwa aliposema welcome members of diplomatic corpse badala Corp.
 
Kiingereza hakileti chakula. Kiingereza hakiondoi rushwa na ufisadi. Kiingereza hakiboreshi hali za maisha ya watanzania. Kwahyo hata kama Rais Magufuli angekuwa anaweza kuongea kiingereza bora kuliko binadam yeyote hapa duniani haimaanishi kuwa angefanya vizuri katika kutatua matatzo ya watanzania
 
Kuyaelewa matatzo ya watanzania na kujua jinsi ya kuyatatua hakuendani na umahiri wa lugha ya kiingereza. Rais bora wa watanzania ni yule mwenye Kuyaelewa matatzo ya watanzania na kuwa na suluhisho la hayo matatzo. Kama kiingereza kingekuwa ni sifa ya mtu kuyaelewa matatzo ya watanzania na kuwa na uwezo wa kuyatatua basi tunge mkodisha mwingereza aje awe Rais wa Tanzania
 
Tukija kupata Rais wa Tanzania ambaye ni bingwa wa kiingereza kuna baadhi ya watanzania wenzetu watategemea kuwa ndio atakuwa sio fisadi na ataifanya Tanzania iwe miongoni mwa nchi bora zaidi hapa duniani. Poleni sana
 
Kuna watanzania wenzetu wamevurugwA akili na wadhungu mpaka wamefikia kujichukia na kujishusha hadhi wenyewe. Ukianza kubeza lugha yako ni dalili ya kwamba hujitambui, hujithamini na hujiamin kama na wewe ni binadam kama binadam wengineo hapa duniani
 
Hapo lazima Mama Suluhu, au PM ahusike maana hata kutembeza bakuli kwa mabalozi kuhusu issue ya Kagera ilibidi asimamie PM, Ki..Elizabeth jamani hatariiiiiii..
 
Hujui lugha ina mchango wake katika kuondoa umasikini?
Kama ni mtu mzima basi watoto wako wana hasara sana na pia kama ni kijana taifa lina hasara sana

Hujui hata nini maana ya lugha ?

Na kama lugha ni mafanikio katika maisha dunia nzima leo tungekuwa tunaoongea kichina au kiarabu kwa Ku refer Oman na Saudi arabia
 
Tutapiga sana kelele humu jukwaani lakini ukweli utabaki palepale ngeli ni muhimu sana sababu inakufanya ujiamini popote unapoenda. Kumbuka mzungu akitaka kitu chako hata broken english ongea tu ili mradi anajua mwisho wa siku ataondoka na alichokifuata; lakini ukitaka kitu kutoka kwake lazima ujue kujieleza mpaka akuelewe, sasa kwa mkulu tuliyenaye hii tuhesabu tumeshaumia na ikumbukwe Tanzania ni changa kutegemea misaada ni lazima. Mungu wangu sijui tutafanyeje kwa hali hii
 
Hebu tupende kudumisha lugha yetu bhana.....kwan kuitukuza lugha ya kigen huo ni ukoloni mambo leo tuamke kifikra wana Afrika mashariki, tena ningefurahi sana kama Raisi JPM awepo na azungumze kiswahili kwenye mkutano huo
Au wengine mnakubaliana na usemi wa Trump kwamba tutawaliwe upya maana mnaitukuza sana hii lugha ya kigeni kwa kutokujua huo ni ukoloni
Lugha inadumishwa na katiba sio kiholela kama unavyota sio kila ajaye anaibuka na lugha yake.
 
Back
Top Bottom