Rais Magufuli apendekeza soko kuu la Dodoma liitwe Soko kuu la Ndugai

Rais Magufuli ametoa pendekezo kuwa soko kuu jipya linalojengwa jijini Dodoma liitwe Soko kuu la Ndugai.

Hii ni kstika kuenzi mchango wa Spika Job Ndugai wa kuuletea maendeleo ya haraka mkoa wa Dodoma

Source TBC

Roho ileile ya KUJIMWAMBAFY inaendelea kujiinua...!!!
Kwanini Rais Magufuli asingependekeza Soko Kuu liitwe SOKO KUU LA MWALIMU NYERERE ambaye ndiye alipendekeza MAKAO MAKUU KUHAMIA DODOMA??? Hivi Ndugai amefanya kitu gani cha maenedeleo ya haraka Dodoma mjini zaidi ya kuwa Spika Bungeni na kuhakikisha Kambi ya Upinzani inasambaratishwa nje na ndani ya Bunge?
Kiukweli ni kwamba Rais Magufuli anafanya hivo kama Fadhila kwa Job Ndugai kwa kuhakikisha Wapinzani wanasambaratishwa nje na ndani ya Bunge kwa speed ya supersonic..!!! Lakini pia Ndugai si Mbunge wa Jimbo Dodoma Mjini yeye ni Mbunge wa Jimbo la KONGWA ambalo halihusiani kabisa na Jimbo la DODOMA MJINI hivo si sahihi kusema Ndugai kaleta maendeleo Mjini Dodoma ilhali yeye anatoka Kongwa swekeni...!!
 
Ameifanyia nini spesho kwenye nchi hii hadi jina lake litumike?..kuwa spika wa bunge hakumfanyi yeye kuwa legendary
 
Jamani/ Faru Ndugai, Soko la Ndugai, Mwisho Nyoka Ndugai nk.

Tuwaenzi na hawa akina mama. Mama Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mama Fatuma Karume nk.

Kina ndugai tuwaache wana yao ambayo wengine wanao ukakasi.

Kinachoonekana hapa ni Ubinafsi na Roho mbaya kuliko hata shetani mwenyewe....!!
Dikteta siku zote ni watu wenye kujiinua na kupenda mijisifa na mbwembwe nyingi!
 
Rais Magufuli ametoa pendekezo kuwa soko kuu jipya linalojengwa jijini Dodoma liitwe Soko kuu la Ndugai.

Hii ni kstika kuenzi mchango wa Spika Job Ndugai wa kuuletea maendeleo ya haraka mkoa wa Dodoma

Source TBC
Huyu mzee tangia aweke mic sikioni huku akisema "Harooo unanisikia" Akili zimezidi ku-zygomycomyphatta. Sasa Ndugai kafanya nini zaidi ya kulidhalilisha bunge na kulishushia heshima?
 
Rais Magufuli ametoa pendekezo kuwa soko kuu jipya linalojengwa jijini Dodoma liitwe Soko kuu la Ndugai.

Hii ni kstika kuenzi mchango wa Spika Job Ndugai wa kuuletea maendeleo ya haraka mkoa wa Dodoma

Source TBC
What a loss!
 
Kwa tija ipi kwa taifa ambayo ndungai katengeneza kuzidi watu kibao waliomtangulia wakina pius Msekwa Na Samwel Sitta basi mimi napendekeza apewe Kibajaji ilo jina la soko maana ni zaidi ya Tyson Ndungai.
,kumvua lisu ubunge si jambo dogo,kupambana na CAG,mpaka kaachia ngazi sio jambo dogo,kwa kweli jiji lote liitwe jiji la ndugai
 
Naona wanapena mapande tu, juzi bunge limetoa azimio maalumu la kumpongeza Rais leo Rais anapendekeza Soko liitwe Ndugai!
 
Rais Magufuli ametoa pendekezo kuwa soko kuu jipya linalojengwa jijini Dodoma liitwe Soko kuu la Ndugai.

Hii ni kstika kuenzi mchango wa Spika Job Ndugai wa kuuletea maendeleo ya haraka mkoa wa Dodoma

Source TBC
Sio kwamba kapendekeza bali katoa amri
 
Ninapendekeza badala ya soko Ikulu ya Chamwino iitwe NDUGAI PALACE hii ndiyo heshima anayosyahili kupewa.
 
Apewe tu hasa kwa kuunga mkono juhudi za kuua upinzani na kufunika/kusafisha ufisadi wa jiwe kwa brashi ya bunge.

Muhimili wa bunge Ndugai kauinamisha kifudifudi kumsujudia jiwe anayejiita kiongozi wa malaika. Jiwe naye anaamua kumshushia ndugai punje za "mana".

Huu ni zaidi ya upumbavu. Tatizo hatuna jina la kuuita huu ushirika wa ibada za kishetani.
 
Back
Top Bottom