Rais Magufuli aidha amedanganywa kuhusu Barakoa au kuna tatizo sehemu (kwa alichoongea leo Feb 21, 2021)

Ila magu, kwa kweli kama huwa unamaanisha na unamtumainia Mungu, wewe binafsi kiasi hicho, achana na mambo ya kuwaogopa wapinzani na n.k, basi imani yako ni ya kuigwa. ni kubwa mno.
 
sio bado anasema mpaka leo! Amesemea kanisani ili tuamini kirahisi. si unajua huku bongo kuna wakatoliki kuliko rome;
Anaharibu sana separation of church and state.

Nyerere alikuwa anaenda kanisani kila siku. Si kila Jumapili. Kila siku aliyokuwa Dar alikuwa anaanza na sala St. Peters.

Mkapa yeye alienda kanisani Jumapili alivyokuwa rais.

Sikuwahi kuwasikia hawa wakisimama mbele kanisani kutoa hotuba za kisiasa.

Walijua kitu kinaitwa "separation of church and state".

Huyu wa sasa akiambiwa na Waislamu kwamba nchi inaongozwa na Mfumokristo atakataa?
 
Kua uyaone mdogo wangu!
Mkuu TUJITEGEMEE,

Ninyi ndo wana JF tunaowategemea huko kwenye mfumo kwa sasa.

Naomba tuelewe:

1) Issue ya Barakoa: Mwambieni Rais anachemka big time, sisi wananchi si wajinga kiasi hicho.

2) Kuhubiri kanisani na kwenda na wapiga picha: Viongozi wa Dini wanaweza wasiwe wanamwambia, anakosea. Si sahihi, ingekuwa mara moja moja wala nisingetia neno

3) Kuhusu Chanjo: The last time alipoongea ilionyesha wazi alikuwa off key sana. Yaani, hadi mtu unajiuliza kama kawasiliana na Wizara (kama taasisi) au kaishia kuongea na Waziri tu. Kama kuna mtu kampelekea taarifa zile, basi naye alimpoteza parefu. Nakubali, tunaweza kukataa kutumia chanjo yoyote - ni haki yetu kama Taifa na Rais anaweza kutusemea ila asianse kutengeneza nadharia na kuziongea! Simply aseme watu wangu hawatatumia hadi zithibitishwe. That’s it.

Tunawategemea sana mkuu!
 
Wakuu,

Nimemsikiliza Rais Magufuli akiwa anaongea leo kanisani. Nimeshtuka, Rais anaongea kama layman kabisa. Hii ni hatari kwa Usalama wa Taifa kwa mtu ambaye amepewa dhamana ya juu kabisa hapa nchini.

Rais ni Comforter-in-Chief hivyo kama mfariji mkuu wa Taifa ana mamlaka makubwa aliyobebeshwa na hili inaelekea Magufuli analisahau sana. Huwezi toka huko na kuanza kuwambia watanzania eti “Kufa tutakufa tu”.

Rais ni kama BABA katika familia, na kwa Taifa yeye anasimama kama kichwa cha familia. Huwezi kuwa baba bora ukawa unatishia watu wako (wanao, mkeo, ndugu n.k). Kama baba, unaweza kulaumiwa, unaweza kuliliwa, unaweza kupongezwa, unaweza kuumizwa na hatutarajii kuwa utaitangazia familia kuwa wakome kufanya hivyo! Utakuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yako.

Rais ni KIUNGO katika Taifa. Unapotokea mgawanyiko, ana wajibu wa kuhakikisha watanzania wanakuwa wamoja. Hili limekuwa likionekana kuwa tofauti kwa Rais wetu huyu.

Rais anapotoa kauli, ni kauli ya Taifa si yake. Mambo mengi anayoongea Magufuli watanzania walio wengi (wanaojielewa) watakubaliana nami kuwa si yale ambayo kimataifa tungependa kiongozi wetu ayaongee kwa niaba yetu!

Msikilize:

Sasa:

1) Magufuli leo kaongea UONGO mwingi kuhusu barakoa. Alichokiongea ni matusi kwa serikali yake mwenyewe!

- Kama barakoa zilizoingizwa nchini zina virusi au hazifai; kwanini watendaji wake wameziacha ziingizwe sokoni? Anataka kutuambia kuwa TBS na TFDA hawajui kazi yao? Kwanini watendaji wakuu wa taasisi hizi bado wapo kazini?

- Tukubali kuwa tumeingiziwa barakoa zenye kuwa na virusi ambazo zitawaua watanzania: Kwanini Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, IGP na CDF bado wapo kazini? Taifa letu manake usalama wake upo hatarini. Kwa mantiki hiyo, maduka ya madawa yavamiwe mara moja na barakoa zote ziondolewe sokoni

2) Magufuli amekuwa Rais wa kwanza mimi kumuona akiwa anahubiri katika Ibada za Kanisa Katoliki. Huu ni utaratibu wa kawaida kwa wakatoliki? Halafu anawachamba viongozi wa kanisa kwa kuhimiza waumini kujilinda?

3) Rais ametangaza dawa kadhaa kama Bupiji, COVIDOL etc, anataka kuwaaminisha watanzania kuwa Sayansi haifanyi kazi tena? Kuwa watanzania wasiziamini hospitali tena? Haya matangazo ya dawa za asili imekuwaje hadi wasaidizi wake wamwacha hadi ataje baadhi ya dawa moja kwa moja? Ana maslahi nazo? Nasikia mtu aliwahi kuwa RC wa Dar ana mkono kwenye pharmacy chain flani, na kuna tetesi kuwa yupo kwa niaba ya ‘mzee’; hii haoni inazidi kujenga hisia zisizo sahihi?

Nitarejea

Shida yenu hampendi kuambiwa ukweli, barakoa ziliingizwa nyingi sana kipindi cha mwaka jana, na baada ya serikali kugundua hilo walianza kuzuia baadhi ya barakoa zinaonekana zina walakini, na ndio maana kuna kipindi surgical mask zilikuwa adimu hadi mahospitalini kiasi kwamba madaktari walianza kulalamika. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, MSD walifanya dharura ya kujenga kiwanda cha kuzalisha barakoa za mahospitalini (surgical mask) amabapo kimeanza full production mwezi wa tisa mwaka jana.

Kuhusu dawa za asili nadhani wewe una tatizo kichwani na pengine unachanganya uchawi na dawa za asili. Aliyekuambia dawa za asili nazo si sayansi ni nani? Tofauti ya dawa za asili na hizi za kawaidi ni matumizi ya kemikali. Halafu hata hizo dawa za asili nazo ni sayansi pia, kwani wanachofanya NIMR ni nini kama siyo sayansi?

Halafu kosa ni lipi kwa yeye Rais kutaja dawa ili wananchi wazitumie wapone? Yeye kataja zile ambazo serikali imethibitisha zinafanya kazi, na wananchi wana haki ya kuzijua ili wazitumie wapone, sasa ulitaka afiche ili kiwe nini? Au mleta mada una dawa yako ambayo imeshindwa kuthibitishwa ubora wake hivyo unaona wivu kutajwa dawa zingine?

Pia viongozi wa dini kama binadamu wengine wanachambwa kama kawaida pale wanapokosea. Aliyekuambia kiongozi wa dini hakosolewi basi alikudanganya sana. Unzuri wa Magufuli anakupa za uso hapo hapo hajali wewe ni nani. Ni lazima tuambiane ukweli ili tuweze kubadilika.

Kingine, anachofanya Magufuli si mahubiri, mahubiri ya Kanisa katoliki yanafanywa kabla ya kutoa sadaka baada tu ya somo la Injili ambapo huwa ni katikati ya ibada au misa. Muda anaosimama Magufuli ni muda wa matangazo ambapo misa au ibada inakuwa imeisha. So usichanganye hivyo vitu, kanisa katoliki lina utaratibu wake, na ibada au misa zina miongozo yake ya kufuata.
 
Anaharibu sana separation of church and state.

Nyerere alikuwa anaenda kanisani kila siku. Si kila Jumapili. Kika siku aliyokuwa Dar alikuwa anaanza na sala St. Peters.

Mkapa yeye alienda kanisani Jumapili alivyokuwa rais.

Sikuwahi kuwasikia hawa wakisimama mbele kanisani kutoa hotuba za kisiasa.

Walijua kitu kinaitwa "separation of church and state".

Huyu wa sasa akiambiwa na Waislamu kwamba nchi inaongozwa na Mfumokristo atakataa?
Exactly my point.

Ikulu ni taasisi, ni zaidi ya mtu mmoja. Taasisi ijitafakari katika anachofanya aliyekalia kiti. Anaacha legacy gani? Akija mwingine anaweza kufanya zaidi ya hivyo.

Hii Ikulu inaendeshwa kwa kodi zetu watanzania. Tuna haki ya kukataa baadhi ya mambo. Ndo uzalendo!
 
Wakuu,

Nimemsikiliza Rais Magufuli akiwa anaongea leo kanisani. Nimeshtuka, Rais anaongea kama layman kabisa. Hii ni hatari kwa Usalama wa Taifa kwa mtu ambaye amepewa dhamana ya juu kabisa hapa nchini.

Rais ni Comforter-in-Chief hivyo kama mfariji mkuu wa Taifa ana mamlaka makubwa aliyobebeshwa na hili inaelekea Magufuli analisahau sana. Huwezi toka huko na kuanza kuwambia watanzania eti “Kufa tutakufa tu”.

Rais ni kama BABA katika familia, na kwa Taifa yeye anasimama kama kichwa cha familia. Huwezi kuwa baba bora ukawa unatishia watu wako (wanao, mkeo, ndugu n.k). Kama baba, unaweza kulaumiwa, unaweza kuliliwa, unaweza kupongezwa, unaweza kuumizwa na hatutarajii kuwa utaitangazia familia kuwa wakome kufanya hivyo! Utakuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yako.

Rais ni KIUNGO katika Taifa. Unapotokea mgawanyiko, ana wajibu wa kuhakikisha watanzania wanakuwa wamoja. Hili limekuwa likionekana kuwa tofauti kwa Rais wetu huyu.

Rais anapotoa kauli, ni kauli ya Taifa si yake. Mambo mengi anayoongea Magufuli watanzania walio wengi (wanaojielewa) watakubaliana nami kuwa si yale ambayo kimataifa tungependa kiongozi wetu ayaongee kwa niaba yetu!

Msikilize:

Sasa:

1) Magufuli leo kaongea UONGO mwingi kuhusu barakoa. Alichokiongea ni matusi kwa serikali yake mwenyewe!

- Kama barakoa zilizoingizwa nchini zina virusi au hazifai; kwanini watendaji wake wameziacha ziingizwe sokoni? Anataka kutuambia kuwa TBS na TFDA hawajui kazi yao? Kwanini watendaji wakuu wa taasisi hizi bado wapo kazini?

- Tukubali kuwa tumeingiziwa barakoa zenye kuwa na virusi ambazo zitawaua watanzania: Kwanini Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, IGP na CDF bado wapo kazini? Taifa letu manake usalama wake upo hatarini. Kwa mantiki hiyo, maduka ya madawa yavamiwe mara moja na barakoa zote ziondolewe sokoni

2) Magufuli amekuwa Rais wa kwanza mimi kumuona akiwa anahubiri katika Ibada za Kanisa Katoliki. Huu ni utaratibu wa kawaida kwa wakatoliki? Halafu anawachamba viongozi wa kanisa kwa kuhimiza waumini kujilinda?

3) Rais ametangaza dawa kadhaa kama Bupiji, COVIDOL etc, anataka kuwaaminisha watanzania kuwa Sayansi haifanyi kazi tena? Kuwa watanzania wasiziamini hospitali tena? Haya matangazo ya dawa za asili imekuwaje hadi wasaidizi wake wamwacha hadi ataje baadhi ya dawa moja kwa moja? Ana maslahi nazo? Nasikia mtu aliwahi kuwa RC wa Dar ana mkono kwenye pharmacy chain flani, na kuna tetesi kuwa yupo kwa niaba ya ‘mzee’; hii haoni inazidi kujenga hisia zisizo sahihi?

Nitarejea
Unataka kusema bupiji ma covido siyo science imetumika kuzitengeneza? Mbona wewe ndiyo unaonekana hujitambui mapema kweupe?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Huyu bwana kama kweli anachokizumza ndicho anachokiamini mi naona aachwe aendelee kuhubiri maana hamna namna kama corona yenyewe inamuogopa kama ukoma
 
Anasema watu wanakufa kwa mipango ya Mungu. Anajivua lawama kwamba hata watu wafe wangapi yeye hahusiki, hana uwezo wala jukumu la kuzuia hilo.

Ana uwezo mdogo sana wa kufikiri na anawapa kazi sana wasaidizi wake. Nahisi wameamua wamuache tu!
Kwel kabsa mkuu ulichoongea uko sahh nakubalia na ww %100
 
Barakoa zina corona,chanjo ina madhara makubwa ikiwemo kuwafanya wanawake wagumba na wanaume mazezeta, social distance ni njia ya kutuletea hofu na kufanya tusizaliane hakuna corona ni magonjwa ya kawaida ya changamoto ya kupumua(serikali).

Wataam wa afya na vyombo vya dini 'corona ipo tuchukue tahadhari za kuvaa barakoa,social distance na kufwata ushauri wa wataalam wa afya'.

Hivi hii chanjo aliyo chanjwa biden,Obama,prince Philip,Queen Elizabeth, Putin na viongozi wengine wakubwa ndiyo iyo tunaambiwa si salama?. Tujaribu kuwaza tu hyprocratic politicians kama yule anaye vaa tai ya taifa,yule prof wa jalalani ni kweli hawajapigwa chanjo hadi muda huu?.
Una uhakika chanjo unayoletewa ndiyo hiyo ya akina Biden? Africa imeandaliwa chanjo yake tofauti na ya hao unaowataja ndugu yangu.
 
church and state
Mbona hamuhoji wale wa church wanaposahau mpaka wa state ulipo na kuhimiza wananchi wafanye mambo yasiyo ya ki-church bali ya kisiasa shughuli zinazo fungamana na state!? Tukisema mnafanya double standard gestures tutakosea!?
 
Kwanza kabisa. Umekubali Magufuli kaharibu?

Tumalize hili kwanza.

Huko kanisani kuna uozo ambao kila siku nausema hapa, kwa hiyo kati ya wasiohoji uozo wa kanisa, mimi usiniweke.

Ukiniweka huko, nitaona hunifuatilii.
 
Ukishazoea kuloga watu uhisi KILA mtu anataka kukuloga.
Unaweza ukawa umepita shule na bado ukawa mweupe vile vile
 
Did I dispute matumizi ya dawa za asili? Hapana, nataa narrative ya kuwa barakoa wanazotumia watanzania si salama.

View attachment 1708150
Kuna kipindi barakoa za mahospitali (surgical mask) ziliadaimika sana hadi mahospitalini kiasi kwamba hadi madaktari walianza kulaumu kwa kukosa kitendea kazi hicho muhimu. Kilichotokea ni kuzuiwa uingizwaji wa barakoa nyingi ambazo zilikuwa si salama. Sasa hivi hilo tatizo limepungua baada ya MSD kuanza uzalishaji wa surgical mask. MSD wameanza uzalishaji mwezi wa tisa mwaka jana. Pia serikali baada kugundua kuwa kuna barakoa nyingi zisizo salama zimeingia nchini walifanya msako kwenye maduka ya mauzo.
 
Shida yenu hampendi kuambiwa ukweli, barakoa ziliingizwa nyingi sana kipindi cha mwaka jana, na baada ya serikali kugundua hilo walianza kuzuia baadhi ya barakoa zinaonekana zina walakini, na ndio maana kuna kipindi surgical mask zilikuwa adimu hadi mahospitalini kiasi kwamba madaktari walianza kulalamika. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, MSD walifanya dharura ya kujenga kiwanda cha kuzalisha barakoa za mahospitalini (surgical mask) amabapo kimeanza full production mwezi wa tisa mwaka jana.
Let’s assume unasema ukweli na sisi tunaoohoji ndo hatujielewi:

1) Mwaka jana (2020) ni NANI alikuwa Rais wa Tanzania? Ilikuwaje Taifa likafanyiwa hujuma hii bila kushtukiwa? Usalama wetu kama Taifa ulikuwa compromised? Nani hasa walizileta? Walichukuliwa hatua gani na umma ulijulishwa?

2) Kama Sept 2020 (unavyodai) zilizalishwa masks za kutosha, kwanini leo aongelee masuala ambayo yamepitwa na wakati? Si hazipo hizo? Kwanini aongelee kisichokuwepo? Na, kwanini wakati wa kampeni alikuwa anadai “Tumeimaliza Corona nchini mwetu” hadi baadhi ya maigizo yakafanywa na kanisa flani kutoa certificate ya ushindi dhidi ya Corona?
Kuhusu dawa za asili nadhani wewe una tatizo kichwani na pengine unachanganya uchawi na dawa za asili. Aliyekuambia dawa za asili nazo si sayansi ni nani? Tofauti ya dawa za asili na hizi za kawaidi ni matumizi ya kemikali. Halafu hata hizo dawa za asili nazo ni sayansi pia, kwani wanachofanya NIMR ni nini kama siyo sayansi?
Hapa umeamua kusimama hivi, ni haki yako. Lakini, umeelewa nilikuwa namaanisha nini. So, TZ mna mpango wa kuondoa dawa za kemikali au nazo zitaendelea kuwepo sokoni?

Halafu kosa ni lipi kwa yeye Rais kutaja dawa ili wananchi wazitumie wapone? Yeye kataja zile ambazo serikali imethibitisha zinafanya kazi, na wananchi wana haki ya kuzijua ili wazitumie wapone, sasa ulitaka afiche ili kiwe nini? Au mleta mada una dawa yako ambayo imeshindwa kuthibitishwa ubora wake hivyo unaona wivu kutajwa dawa zingine?
Ukiwa Rais, ukiamua KUTAJA mfano dawa au bidhaa - taja zote. Kataja mbili, watamtumia sauti yake na video for marketing. Wrong!

BTW, jifunzeni kukosolewa kwa nia ya kujenga. Yeyote anayewakosoa mnamwangalia kwa jicho la chuki tu. Tunajenga Tanzania moja mkuu!
Pia viongozi wa dini kama binadamu wengine wanachambwa kama kawaida pale wanapokosea. Aliyekuambia kiongozi wa dini hakosolewi basi alikudanganya sana. Unzuri wa Magufuli anakupa za uso hapo hapo hajali wewe ni nani. Ni lazima tuambiane ukweli ili tuweze kubadilika.
The approach was totally wrong. Nafasi ya Rais msiichukulie poa, come again. Think about it!

Nashauri: Fikiria nafasi ya Rais kama Mfariji Mkuu wa Taifa, utaelewa. Hapo bado amechemka! He needs to know his limits and his obligations. Bahati mbaya huenda unanisoma ukinifikiria kama nisiyemtakia mema Magufuli!
Kingine, anachofanya Magufuli si mahubiri, mahubiri ya Kanisa katoliki yanafanywa kabla ya kutoa sadaka baada tu ya somo la Injili ambapo huwa ni katikati ya ibada au misa. Muda anaosimama Magufuli ni muda wa matangazo ambapo misa au ibada inakuwa imeisha. So usichanganye hivyo vitu, kanisa katoliki lina utaratibu wake, na ibada au misa zina miongozo yake ya kufuata.
Hahaha, mkuu nadhani hujui unayeongea naye ni nani. Nalijua Kanisa vema! Simply - change the approach. Iheshimuni madhabahu
 
Back
Top Bottom