Rais Magufuli afanya mazungumzo na msomi Prof Patrick Loch Otieno Lumumba, msomi huyu ammwagia sifa lukuki Dr Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,946
141,920
Rais Magufuli leo amekutana na msomi mbobezi duniani Prof Patrick Lumumba Ikulu jijini Dsm.

Rais Magufuli amempongeza Prof Lumumba kwa namna anavyojitahidi kuwashauri viongozi wa Afrika namna ya kuzifanya nchi zao zijitegemee.

Nay Lumumba amempongeza Dr Magufuli kwa jinsi alivyoibadilisha Tanzania kutoka kuwa Taifa tegemezi hadi kuwa taifa linalojitegemea.

Prof Lumumba amesisitiza kuwa anaipenda sana kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu iliyoasisiwa na mzalendo wa kweli barani Afrika Rais Magufuli

======

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Msomi na Mwanajumui wa Afrika (Pan-Africanist) Profesa Patrick Lumumba, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli na Profesa Lumumba ambaye ni raia wa Kenya wamezungumzia masuala mbalimbali yahusuyo juhudi za Afrika katika kuimarisha uchumi kwa kutumia rasilimali zake .

Pia wajibu wa Waafrika na viongozi wao katika kuimarisha huduma za kijamii na kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Rais Magufuli amempongeza Profesa Lumumba kwa juhudi zake za kueleza waziwazi makosa yanayosababisha nchi za Afrika kubaki nyuma kiuchumi, kijamii na kisiasa, wajibu wa viongozi na wananchi wa Afrika katika kukabiliana na changamoto zinazozikabili nchi zao na mapenzi yake makubwa kwa Afrika.

Rais Magufuli amemueleza juhudi ambazo Serikali inazifanya katika kujenga uchumi imara wa kujitegemea ikiwamo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa Bwawa la Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 za umeme na kuongeza usambazaji wa umeme kutoka vijiji 2,018 hadi kufikia vijiji 8,587.

Pia, ujenzi wa barabara na madaraja makubwa na madogo, kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, kuongeza mikopo ya elimu ya juu, kuongeza ukusanyaji wa mapato, kudhibiti rasilimali muhimu ya madini na kupambana na rushwa.

“Mimi sijawahi kukutana nawe kabla, lakini nakusikia na kukuona kupitia vyombo vya habari jinsi unavyopaza sauti kuhusu Bara la Afrika, nakupongeza kwa juhudi hizo, na ninafarijika kwamba unaisemea vizuri Afrika,” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake, Profesa Lumumba amemshukuru Rais Magufuli kwa kutenga muda wake kuzungumza naye na amempongeza kwa juhudi kubwa alizozionesha katika kipindi kifupi cha uongozi wake wa miaka minne ambapo ameonyesha mfano wa namna ya kupigania rasilimali za nchi ikiwemo madini, kujenga nidhamu ya utumishi Serikalini, kuimarisha uchumi, kupambana na wizi wa mali za umma, rushwa na ufisadi.

Profesa Lumumba amesema inafaa kwa nchi za Afrika kujifunza mambo yanayofanyika Tanzania kwa sasa na amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Waafrika kujiamini na kuchukua hatua madhubuti za kuwaondoa katika hali ya sasa ambapo rasilimali zake zinachukuliwa na Mataifa ya nje ilihali wananchi wake wakikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na Mwakilishi wa Kansela wa Ujerumani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Guenter Nooke, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Nooke amewasilisha ujumbe wa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na pia ameelezea kufurahishwa kwake na hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa hapa nchini ikilinganishwa na alipokuja miaka iliyopita.

Pia amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali katika kupambana na rushwa na kuimarisha uchumi ambapo ameahidi kuwa Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji na biashara na masuala mengine ya kijamii.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amemhakikishia Kansela wa Ujerumani kuwa Serikali ipo tayari kuuendeleza na kuukuza zaidi uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati yake na Ujerumani, na inawakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini.

Katika mazungumzo hayo, Nooke ameongozana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Regine Hess.

Chanzo: Mwananchi
 
Nilisha kwambia kuwa kwa kazi zangu sioni sababu ya kujikomba kuomba kama wewe ambaye unaitegemea njia hiyo ili uweze kuishi
Nilikuona pale unavyoangaika kumsalimia kabendera ili mradi tu ukianza mizinga dadeeki wewe kiboko kwa kuangalia fursa, nyalandu tu kwa unati humsogelei

In God we Trust
 
Katika ulimwengu uliostarabika Professor atafundisha viongoz juu ya maendeleo ya watu kwny democracy,uhuru wa kujieleza,upelekaji wa elimu Bila upendeleo wa wananchi wake Bila kujali vipato vyao,atapeleka maji na huduma za afya kwa kiwango stahiki..ataelezea kwny ulimwengu huu kwamba democracy na watu lazma vifungamane ndipo maendeleo yenye usawa lazma yapatikane .
Uprofesa sio vyeti wala majoho mengi!! Sasa siku hizi maprofessor wengi wamekua wanaangalia matumbo yao!!
Badala ya kuendelea kufanya tafit na kuendelea kuzifundisha nini cha kufanya SERKALI nyingi duniani wamekubali kutekwa elimu zao na kuminywaa uvunguni mwa wanasiasa !!
Hakika kw hili uprofesa wao hauna maana tena !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom