Waziri Membe, leo ametetea safari za rais Kikwete, nje ya nchi akisema zina umuhimu na manufaa makubwa sana kwa taifa letu. Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Neptune, Zanzibar leo, alisema kuwa wale wanaomlaumu rais laiti wangejua faida ya hizo safari wasingesema sana na kumlaumu sana rais bila sababu za msingi.
Wamefikia hadi hatua ya kumuita Vasco da Gama, hii ni heshima kubwa sana, kwani huko Ureno kuna majumba mpaka mitaa yenye hilo jina, na mimi Membe ningeitwa hivyo ningefurahi sana, alisema waziri Membe.
Mwaka jana Rais Kikwete, alisafiri mara 17 nje ya nchi kulinganisha na Mbeki wa Afrika Kusini, aliyesafiri mara 21. Bila ya kupata rais wa kuhangaika, nchi haiwezi kuendelea. Alikwenda US kutafuta na kupewa dola 698 millioni na karibuni mtaona matunda yake. Wengine mnasema eti akienda huko Us haonani hata na rais wa huko, sio lazima amuone rais Bush, akienda huko. Anapoenda huko nje, huwa anaenda kuhemea, kutatua migogoro, kimsingi huwa anposafiri huwa ni kwa sababu ya jambo zito sana na sio kutaliii kama wapinzani wengi wanavyosema.