Rais Kikwete kweli watu wamekuchoka

me nashangaa sana hv kwa nin anapenda kuzungumza na wazee wa dar? yani ilikuwa bado beat 2,,, taarabu ikamilike
 
Wana JF,
Ndugu zangu nimeshuhudia watu wakizima TV na radio zao baada ya kuona JK anaanza kuhutubia. Wengine wanasema kumsikiliza huyu jamaa ni kujiumiza kichwa bure.Maana TV stations na redio mbalimbali zimeweka hicho kipindi, watu wanaona ni bora kuzima vyote na baada ya yeye kuhutubia ndo wawashe TV na radio zao.Hii inadhihirisha jinsi gani watu walivyomchoka rais Kikwete.

Kama vile umeniona! Nilidhani ni mimi tu. Ni ukweli usiopingika Kikwete Kachokwa na zaidi CCM imechokwa. Sasa hivi CCM inaonekana kama shetani katikati ya malaika wa Nuru. Kikwete ni taswira ya CCM. Hakika kwa dhambi ya CCM inayoifanya kwa sasa hukumu lazima iwaangukie 2015.
 
Inasikitisha kwa kuwaambia Watanganyika wafute historia yao kwakua asilimia 91 wamezaliwa ndani ya Tz.
Huu ni udhaifu mkubwa sana lakini kauli hi kwetu Waznz iishie chumbe.
 
Yaani leo sikutegemea JK kuongea pumba kiasi kile. Wao ccm wanaona wanamamlaka na kila kitu cha watanzania. Kwa hali hii hakuna hata sababu ya kuendelea na mchakato wa katiba. Its an absurd and useless
 
Ukitaka watu wote wakusikilize ongea mawazo yaliyo sawazika, ukionyesha upande ukiwa kiongozi wale wasio wa upande wako hawatakuheshimu. Ukiwa Baba hupaswi kuwapima watoto Wako kwa kuwalinganisha na watakao kurudi hutawaua au kutowajali.
 
Nyerere alipokuwa anahutubia kila mtu alikuwa na hamu ya kusikiliza anasema nini, JK hasemi la maana hivyo naturally watu hawawezi kumsikiliza. Hata UN ukiwa na pumba kama JK wakati unahutubia ndio watu wanatoka kuvuta sigara

Enzi za nyerere hakukuwa na uhuru wa kupata habari. Yeye ndiye aliyekuwa chanzo kikuu cha habari.
 
Tatizo vijana wa sasa hatujui Mambo muhimu na pili watanzania hatuna uzalendo kabisaa. Mie si mfuasi wa vyama vya siasa ila ninajua kumsikiliza kiongozi wa taifa langu ni muhimu sana. Tuwapende na kuheshimu viongozi wetu tusijechekwa na mataifa mengine
Dah mkuu 0
 
Masikini Tz, tunaongozwa na watu wasio na utashi na weledi wa kutosha.
 
Leo ndio nimeona hasira za mama watoto wangu.kweli KJ kapoteza haiba ya urais....mpaka mke wangu tumefurumushana kwa kunyang'anyana remote...nikiweka TBC anatoa,nikiweka anatoa....ikawa balaaaa,mara nikasikia "Hivi wewe huyu unamsikiliza wa nini,??"
Nikaona mhhhh isiwe tabu,ngoja nijiepushe na shari
 
Back
Top Bottom