Watanzania mngependa Paul Makonda Ateuliwe na Rais Samia Katika nafasi ipi ya uongozi katika serikali ijayo 2025-2030

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
19,134
13,448
Ndugu zangu Watanzania,

Kutokana na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda,uzalendo wake, ujasiri wake katika kufanya maamuzi na kuchukua hatua ,bidii katika kazi ,ubunifu katika kazi,kasi yake kiutendaji,maono ya mbali kiuongozi,uzoefu wake katika uongozi,uchungu wake katika maisha ya watu,upendo wake kwa Taifa na watanzania wanyonge.je Watanzania wenzangu mngependa kuona Rais Samia akimteua Mheshimiwa Makonda katika nafasi ipi ya uongozi?

Mngependa kumuona Mheshimiwa akipewa nafasi ipi ambayo itampatia meno,mamlaka na nguvu zaidi ya kuwachukulia hatua moja kwa moja watumishi ,watendaji na viongozi wazembe,wala rushwa,mafisadi,wanaofanya kazi kwa mazoea,wanao wadhulumu na kupindisha haki za wanyonge? Mngependa kuona Mheshimiwa akiapishwa na kushika nafasi ipi katika serikali ya Rais Samia.

Mnafikiri kwa aliyoyabaini na kuyakuta huko mikoani na namna anavyoongea kwa uchungu na maumivu makali mpaka kusema kuwa anatamani angemchapa mtu makofi .mnafikiri hali ingekuwaje kama angekuwa na mamlaka mkononi mwake ya walau hata kumsimamisha mtu uongozi papo kwa papo kwa ajili ya hatua za kiuchunguzi? Mnafikiri katika ziara zake hizi wakuu wangapi wa wilaya au wakurugenzi au ma ocd au rpc au mameneja wangesombwa na upepo? Mnafikiri ni viongozi wangapi wangeng'olewa huko papo kwa papo?

Maana kwa sasa anaendelea na ziara na kinachofuata utakuwa ni kupeleka ripoti kwa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Dr Mama Samia Suluhu Hasssan juu ya kile alichokibaini huko katika ziara zake ,ikiwa ni pamoja na watu gani anaona ni kikwazo katika kuchochea maendeleo maeneo yao,kuchelewesha miradi ya maendeleo,kuwaonea wananchi,kudhulumu na kuchelewesha haki za watu.

Kwa sasa angalieni namna mikutano yake inavyofurika na kumiminika maelfu ya watu,angalieni namna anavyogusa maisha ya watu,angalieni namna anavyokubalika kwa watu,angalieni namna watu wenye kero na shida wanavyomlilia na kumng'ang'ania ili awasaidie kero zao. Kwa Sasa nimeshuhudia hadi watu wa upinzani wakihudhuria kwa wingi katika mikutano yake kumsikiliza ,lakini pia hata wale wapinzani walio mbali ambao hawafanikiwi kufika kwenye mikutano yake unaona namna walivyo Bize kumfuatilia kupitia mitandao ya kijamii.


Ndio maana hata ukipita kwenye kurasa za mitandao za viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao unaona wakiwa wamepost na kujadili habari za Mheshimiwa Makonda katika kuonyesha kuwa macho na masikio yao yote yameelekezwa katika kufuatilia ziara zake pamoja na hotuba zake na kile kinachojili huko mikutanoni. Kwa sasa Mheshimiwa Makonda kateka habari zote za kisiasa hapa nchini,yeye ndiye habari kuu iliyoteka habari zote katika vyombo vyote vya habari na mitandao yote ya habari.yeye ndiye habari kuu hapa Nchini. ukifungua redio au Tv au magazeti au kuingia mitandaoni lazima ukutane na habari zake tu.angalia hata hapa jukwaani tu ni habari ngapi kwa siku kuhusu mh Makonda zinaletwa?

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
IMG-20240206-WA0027.jpg
IMG-20240202-WA0004.jpg
IMG-20240114-WA0016.jpg
IMG-20240115-WA0007.jpg
IMG-20240208-WA0009.jpg
IMG-20240206-WA0025.jpg
img_tmp_tag1705908502140.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kutokana na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda,uzalendo wake, ujasiri wake katika kufanya maamuzi na kuchukua hatua ,bidii katika kazi ,ubunifu katika kazi,kasi yake kiutendaji,maono ya mbali kiuongozi,uzoefu wake katika uongozi,uchungu wake katika maisha ya watu,upendo wake kwa Taifa na watanzania wanyonge.je Watanzania wenzangu H]View attachment 2899295View attachment 2899296
Yaanii unaanza kuwaza teuzi saivii ndio kero za Watz saivii,
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kutokana na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda,uzalendo wake, ujasiri wake katika kufanya maamuzi na kuchukua hatua ,bidii katika kazi ,ubunifu katika kazi,kasi yake kiutendaji,maono ya mbali kiuongozi,uzoefu wake katika uongozi,uchungu wake katika maisha ya watu,upendo wake kwa Taifa na watanzania wanyonge.je Watanzania wenzangu
Prime Minister itapendeza zaidi halafu pale kwa naibu wa Rais hebu Emmanuel akae apo 🐒


Binafsi nawashukuru sana viongozi wangu wote waliofanya kazi katika nafasi hizo na kwakweli bado wanafanya vizuri. Taifa litawakumbuka kwa kazi zao njema, nzuri na za mfano 🐒

Hata hivyo ni kwa Neema na Baraka za Mungu yote yanawezekana.

When God says Yes, No body can Say No...
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kutokana na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda,uzalendo wake, ujasiri wake katika kufanya maamuzi na kuchukua hatua ,bidii katika kazi ,ubunifu katika kazi,kasi yake kiutendaji,maono ya mbali kiuongozi,uzoefu wake katika
Rais amateue kuwa Mbunge alafu ampe Uwaziri wa TAMISEMI.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kutokana na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda,uzalendo wake, ujasiri wake katika kufanya maamuzi na kuchukua e na kile kinachojili huko mikutanoni. Kwa sasa Mheshimiwa Makonda kateka habari zote za kisiasa hapa nchini,yeye ndiye habari kuu iliyoteka habari zote katika vyombo vyote vya habari na mitandao yote ya habari.yeye ndiye habari kuu hapa
Ateuliwe kuwa mfungwa kwenye gereza lolote nchini ili aitendee haki dhambi aliyoifanya kwa Lissu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kutokana na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda,uzalendo wake, ujasiri wake katika kufanya maamuzi na kuchukua hatua ,bidii katika kazi ,ubunifu katika kazi,kasi yake kiutendaji,maono ya mbali kiuongozi,uzoefu wake katika
Mikono yake imejaa damu za aliowaua ....hatumtaki ....anasubiriwa gerezani damu za watu wasio hatia hazitamuacha salama....muda utaongea
 
Yaanii unaanza kuwaza teuzi saivii ndio kero za Watz saivii,
Siyo teuzi bali majukumu.tunahitaji Mheshimiwa Makonda apewe majukumu kwa ajili ya kumsaidia Mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan katika kuwahudumia wananchi.hii ni kutokana na uchapa kazi wake uliotukuka na ulioikosha mioyo ya watanzania.
 
Mikono yake imejaa damu za aliowaua ....hatumtaki ....anasubiriwa gerezani damu za watu wasio hatia hazitamuacha salama....muda utaongea
Acha uzushi, uongo,fitina na chuki binafsi.acha kuongea vitu pasipo ushahidi.acha kumchafua kiongozi wetu mchapa kazi na muadilifu mwenye mikono safi na moyo safi.
 
Back
Top Bottom