EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,356
Halafu ni taarifa toka ikulu kwa kitu cha sh 16mil
Kaunga,
Nilidhani hii habari imeripotiwa na vyombo vya habari kumbe ni taarifa rasmi kutoka Ikulu kwenda kwa vyombo vya habari.
Ina maana wakati anairudisha hiyo dhahabu kulikuwa hakuna hata waandishi wa habari pale was kuiripoti?
Seriously, hatuhitaji press release kutoka Ikulu zenye vichwa vya habari "Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu".
Ina maana alikuwa harudishi zawadi kama hizo na kwamba hii habari ni ushahidi tosha kuwa sasa amebadilika na huwa anazirudisha?
Akiwa kama kiongozi wa umma Rais hatakiwi kupokea milungula kama hiyo. Sheria za utumishi wa umma ziko wazi kwa hilo.
Kiranga atakuwambia kuwa imefikia mahali ambapo kutokana na kuwa na watawala wabovu unakuta mtawala anajisifia au anasifiwa kwa kufanya jambo ambalo alitakiwa afanye kwa mujibu wa sheria au majukumu yake ya kazi.
Sioni sifa yoyote kwenye hii taarifa kutoka Ikulu bali ni taarifa ya kujikosha kama siyo ya kinafiki.