Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Kaunga,

Nilidhani hii habari imeripotiwa na vyombo vya habari kumbe ni taarifa rasmi kutoka Ikulu kwenda kwa vyombo vya habari.

Ina maana wakati anairudisha hiyo dhahabu kulikuwa hakuna hata waandishi wa habari pale was kuiripoti?

Seriously, hatuhitaji press release kutoka Ikulu zenye vichwa vya habari "Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu".

Ina maana alikuwa harudishi zawadi kama hizo na kwamba hii habari ni ushahidi tosha kuwa sasa amebadilika na huwa anazirudisha?

Akiwa kama kiongozi wa umma Rais hatakiwi kupokea milungula kama hiyo. Sheria za utumishi wa umma ziko wazi kwa hilo.

Kiranga atakuwambia kuwa imefikia mahali ambapo kutokana na kuwa na watawala wabovu unakuta mtawala anajisifia au anasifiwa kwa kufanya jambo ambalo alitakiwa afanye kwa mujibu wa sheria au majukumu yake ya kazi.

Sioni sifa yoyote kwenye hii taarifa kutoka Ikulu bali ni taarifa ya kujikosha kama siyo ya kinafiki.

Mkuu EMT,

Swali langu hapa ambalo litakuwa linahusika kwako counsel, ni kwamba, rais Kikwete alilazimika kurudisha zawadi au alirudisha kwa utashi wake tu?

Kwa maana nyingine, tuna sheria zinazoelezea ni kipi kinaweza kukubalika kama zawadi kwa viongozi wa serikali na kipi hakikubaliki? Pia, kinachokubalika akipewa mtu kama Kikwete kinakuwa mali ya Kikwete au mali ya serikali? Kinakuwa declared vipi na recorded wapi ili watu waweze kufuatilia endapo wakitaka?

Nishaona kuna mabenki ya kimataifa yanakataza wafanyakazi wake kuchukua zawadi inayozidi $ 25 kutoka kwa wateja kwa sababu ya kuepuka muonekano tu wa rushwa, je serikali ya Tanzania ina sheria/ miongozo kama hii? Kipi kinakubalika na kipi hakikubaliki?

Hatuwezi kupigia makofi Kikwete kurudisha zawadi moja wakati hatujui ngapi anachikichia (Savile Row suits anybody?).Hatuwezi kuridhika na Kikwete kurudisha zawadi moja kama hakuna sheria wala muongozo wa jinsi gani viongozi wa serikali wanatakiwa kufanya katika ku handle zawadi.

Hususan kwa kuwa mazingira ya leo hayana mpaka madhubuti kati ya "zawadi" na rushwa.

Serikali ina Anti-Bribery Best Practices/ Policies? Tanzania ina kitu kama UK Bribery Act or US Foreign Corrupt Practices Act na kuzungumzia habari ya zawadi?

Hatuwezi kutegemea wema wa viongozi wajirudi wenyewe kutoka kuchukua zawadi zinazorandana na muonekano wa rushwa, inabidi tuwe na sheria na miongozo ainifu inayoweza kufuatwa bila mgogoro.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
DU safi sana mhe. Rais lakini mwenzako uzalendo ulimshinda akabeba bakuli la dhahabu, sijui kama bado analo au la? umeonyeshwa kuwa wewe si mtu wa kupenda vizawadi, viongozi wengine wangeiga mfano wako kusingekuwa na ten parcent
 
Rais jakaya kikwete amekataa mche wa dhahabu aliopewa kama zawadi na kampuni ya nyamigogo holding yenye uzito wa gramu 250 na kutaka mche huo uuzwe ili pesa zake zilasaidie maskini, mnanipa Mimi ni nikafanyie nini? Aliuliza Rais kikwete?

alikuwa wapi? hapa bongo au nje ya nchi?. mia
 
hapo kuna moja kati ya haya[1]aliidharau zawadi kwa kuona nindogo gramu250,ndio maana akauliza hizi nizifanyie nini?[2]ama ni movie iliyoandaliwa ili ajioneshe kwa wananchi kua ni honesty.hiyo tumeiona wananchi
 
Back
Top Bottom