Sasa hata nusu kilo haijafika jamani? Bora angepewa tofali kama Mkapa angeweza kukubaliRais jakaya kikwete amekataa mche wa dhahabu aliopewa kama zawadi na kampuni ya nyamigogo holding yenye uzito wa gramu 250 na kutaka mche huo uuzwe ili pesa zake zilasaidie maskini, mnanipa Mimi ni nikafanyie nini? Aliuliza Rais kikwete?
Arudishe na zile suti alipewa Arabuni..
Mmbwa akimng'ata binadamu sio habari ila binadamu akimng'ata mbwa ni habari!...hii ni habari!
THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
[TABLE="width: 655"]
[TR]
[TD="width: 239"] Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
[/TD]
[TD="width: 104"][/TD]
[TD="width: 270"] PRESIDENTS OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameirudishia Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya Mkoani Geita zawadi ya gramu 227 za dhahabu safi akielekeza kuwa zawadi hiyo itumike kuwasaidia watoto yatima.
Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu, Novemba 11, 2013, baadaya kukabidhiwa zawadi ya dhahabu hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua mgodi wa uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogo wa Kharuma ambako ndiko makao makuu ya wilaya mpya ya Nyanghwale,Mkoa wa Geita.
Gramu hizo 227 ambazo ni sawa na aunzi nane zina thamani ya Sh. milioni 16 kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.
Baadaya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais Kikwete ameuliza: Sasa nifanye nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popote mnakotaka na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima.
Akizungumza na wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete ameupongeza uongozi wamgodi huo akisema kuwa umeongeza thamani ya dhahabu na ya maisha yawananchi katika eneo hilo nje ya mji mdogo wa Kharuma.
Hatahivyo, Rais Kikwete ameushauri uongozi wa mgodi huo kufanya jitihada za kuboresha teknolojia inayotumika. Mmefanya vizuri sana na mgodi huu ni mradi wa maana sana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili. Ubunifuhuu unastahili pongezi.
Ameongeza Rais Kikwete: Lakini lazima tuboreshe teknolojia. Teknolojia inayotumika kwenye mgodi huu bado ni ya zamani kidogo. Hii ni sawa na hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii ya vipofu watupu. Yeye anaonekana kama mfalme.
Mgodi wa Nyamigogo ambao ni mgodi wa marudio kwa maana ya kwamba unazalishadhahabu kutokana na mchanga ambao huko nyuma umepata kufuliwa nakutoa dhahabu, ulianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa zimewekezwa kiasicha Sh.bilioni 1.6 katika uendelezaji wa mgodi huo.
Risala ya uongozi wa mgodi huo inasema kuwa mgodi huo unaozalisha kiasi chagramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi na unaajiri watu 45 wakiwemo wanawake 10.
Tokea kuanzishwa kwake, mgodi huo umekuwa unaunga mkono shughuli za jamii inayouzunguka ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati na madarasa yashule katika vijiji viwili.
Rais Kikwete amezindua mgodi huo ikiwa sehemu ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika ziara yake rasmi ya kikazi katika Mkoa waGeita, moja ya mikoa minne ambayo aliianzisha mwaka jana. Mikoa mingine ni Simiyu, Njombe na Katavi.
Ziara hiyo ya siku tano inamalizika kesho, Jumanne, Novemba 12, 2013, na mbali ya kuzindua mgodi huo, Rais Kikwete leo amepokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Nyanghwale na kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kharuma uliohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi.
Rais kikwete anatarajia kufanya majumuisho ya ziara yake Jioni ya leo!
Imetolewana:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam.
11Novemba, 2013
JK ana busara sana, ingekuwa ni babu angepokea.
Nchi hii ikikombolewa utatafutwa tu popote ulipoJK ana busara sana, ingekuwa ni babu angepokea.