Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

I wish kama ujasiri huu angekua nao wa kukataa zile suti tulizoambiwa alihongwa na mwekezaji wa nje

Au kwa vile amehongwa hadharani?

Pengine nguvu ya umma imemtisha.

Kwakweli zile suti zilimchafua na hadi sasa hajaweza kujisafisha katika kashfa hiyo
 
Hapa sielewi! Mlitaka Raisi afanye nini na zawadi hii, aichukue na aitumie mwenyewe kwa faida yake au nini!? Hivi kweli hamuoni kwamba hili alilofanya Raisi ni jema kwa umma na kwa hao anaotaka wafaidi baada ya zawadi iyo - "bonge la dhahabu" kuuzwa!? Historia inatuelezea kuwa wengine walishapewa zawadi kama hizo na wakaweka ndani! Tufike mahali tupongeze maamuzi mema jamani. Hongera Raisi kwa uamuzi huu wa busara.

it's funny ameikataa halafu anawaelekeza wakaiuze wawasaidie watoto yatime!!!do you know what does that mean?ni kama ameichukua mwenyewe na kuiuza ila pesa anasaidia yatima.Being the man he is it's no surprise the whole show was pre-calculated.
 
Nimesha fanyia mabadiliko..ni makosa ya kibinadamu tu!
Yeah apologies accepted. Ila nadhani, tunapoweka kitu humu na kama tena ni kutoka kwenye ofisi ya juu kama hiyo, ni LAZIMA tuwe waangalifu, hakuna haraka ni vizuri vitu kama hivi viwe safi na bila makosa ya ajabu ajabu kama hayo yaliyo onyeshwa hapo juu. Mbarikiwe.
 
Hiki ni kipimo kuwa zilikuwa feki.

Na hao walotaka kum-rushwa mkulu wamefikishwa kwenye vyombo vya dola?
 
Nimesha fanyia mabadiliko..ni makosa ya kibinadamu tu!

kumbe ni makosa yako,kama ume-copy na ku-paste hivi basi hili si jambo dogo,taarifa kutoka ikulu haiwezi kuunganishwaunganishwa maneno hivi kama mtoto wa darasa la kwanza halafu useme ni swala la kibinadamu!!no,big no.
 
Hahahah, haifuti zawadi za suti. Halafu ni taarifa toka ikulu kwa kitu cha sh 16mil
 
Gram 227 ndo unaita bonge? tena ina thamani ya milioni 16 tuuu ndo unampa JK? ndo maana kaikataa kaona kwanza wamemdhalilisha wangeandaa kitofali kama vile vya choma muone kama angekataa

Hahahahaha mkuu kitofali kinaweza kuwa na kilo tano na ushee. Hii gramu 200 ni pande la kutosha.
Tukubaliane tu kuwa labda kakataa kwakuwa imetolewa hadharani na akakumbuka mzimu wa zawadi kama hii ya dhahabu ilivyomuandama mtangulizi wake Mkapa baada ya Mrema wa enzi hizo kumuumbua na kumshikia bango.
 
kumbe ni makosa yako,kama ume-copy na ku-paste hivi basi hili si jambo dogo,taarifa kutoka ikulu haiwezi kuunganishwaunganishwa maneno hivi kama mtoto wa darasa la kwanza halafu useme ni swala la kibinadamu!!no,big no.

Noted!
 
HIVI KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU KAZI YAKE NI NINI?
huwa najiuliza sijawahi pata jibu!
serious SIJAWAHI PATA JIBU!
 
Kila nikikumbuka zile suti napata mfadhaiko

Tatizo unapenda sana kuwasikiliza Wazungu! Una uhakika kama kweli? Hivi dhahabu hiyo angepewa ntu kama Babu Slaa na Mbowe wangeikataa?

Shangingi tu la Bungeni ameshindwa kurudishaa? Itakuwa dhahabu , tena zawadi?
 
rais kikwete leo kapewa zawadi ya bonge la dhahabu yenye uzito wa granu 227 kutoka mgodi wa nyamigogo mkoani geita. Lakini akawauliza "niipeleke wapi sasa hii dhahabu?"
akatangaza palepale hadharani kuirudisha dhahabu ile kwa waliomtunza na akawaambia waiuze ili wawasaidie watu na watoto wasiojiweza wanaozunguka mgodi huo.
Dhahabu hiyo ikiuzwa kwa soko huria la leo ina thamani ya shilingi milioni 16

inawezekana alikua anataka yenye thamani kubwa zaidi lakini wao wakampa kidogo
 
it's funny ameikataa halafu anawaelekeza wakaiuze wawasaidie watoto yatime!!!do you know what does that mean?ni kama ameichukua mwenyewe na kuiuza ila pesa anasaidia yatima.Being the man he is it's no surprise the whole show was pre-calculated.
Do you believe you can surprise a President at such functions? ?
 
Angeuza halafu hizo fedha angetoa yeye mwenyewe kwa watoto hao yatima, kwani sina uhakika kama zitawafikia walengwa!
Zawadi hiyo ni sawa na theluthi ya production ya mwezi mmoja. Inaelekea walikua wanatoa rushwa ila rais akawatolea nje. Kuwapa yatima sio lengo lao kwa hivyo itabidi ufuatiliaji thabiti wa ikulu kuona fedha hiyo inatolewa kwa yatima.
 
kumbe ni makosa yako,kama ume-copy na ku-paste hivi basi hili si jambo dogo,taarifa kutoka ikulu haiwezi kuunganishwaunganishwa maneno hivi kama mtoto wa darasa la kwanza halafu useme ni swala la kibinadamu!!no,big no.

Acha gubu..umeshaletewa taarifa..kama una malalamiko wasiliana na Salva Rweyemamu na si kumshambulia mleta mada as if ametenda kosa la jinai..ujifunze kua na shukrani..Bichwa la avatar yako kubwa kweli!
 
Back
Top Bottom