Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Nampongeza Rais Kikwete kwa ujasiri huo. Kila kiongozi akikataa zawadi za mitego ya namna hii makampuni yatazingatia masharti ya uwekezaji ikiwamo kuwajali wananchi!
 
Watu hamnaga jema yaani akichukua maneno akiacha maneno.
 
usanii tu huo nani atathibitisha kweli zimekwenda kusaidia watoto yatima
 
Tatizo unapenda sana kuwasikiliza Wazungu! Una uhakika kama kweli? Hivi dhahabu hiyo angepewa ntu kama Babu Slaa na Mbowe wangeikataa?

Shangingi tu la Bungeni ameshindwa kurudishaa? Itakuwa dhahabu , tena zawadi?

Zawadi kwa Rais wa Jamhuri maana yake nini? What is the motive behind ya kamgodi kadogo kanakochenjua mabaki ya mchanga wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo kutoa zawadi kwa Rais? Mgodi ambao unawafanyisha watoto na akina mama kazi kwenye mazingira hatarishi bila kufuata taratibu za usalama kazini? Teknolojia duni? ukosefu wa vifaa vya kujikinga (personal protective equipment), uchafuzi wa mazingira, matumizi ya kemikali hatari kama mercury na cyanide katika elution columns? Halafu zawadi kwa Rais? Na Rais anawapongeza? Sipati picha!
 
Hili nalo lilihitaji public attention? Mambo mengine ni kujidharirisha tu. Kwani angerudisha halafu wakaacha magazeti yaandike bila ya ofisi ya mawasiliano ikulu kutoa taarifa, ingekuwaje?
 
thamani ya hiyo dhahabu ni nusu ya mshahara wake kwa mwezi, ndio maana kasema afanyie nini, hata nauli ya Los Angeles haitoshi.
 
Amekuwa si mstaarabu.
Sheria na taratibu zinaruhusu kiongozi kupokea zawadi na akishaipokea anaokabidhi serikalini. So kama kiongozi mkuu wa nchi angeipokea na kisha palepale angemkabidhi dc au rc na kumuagiza waisimamie iuzwe na kisha fedha itakayopatikana itumike kwenye ujenzi wa shule au kununua madawatilpl
Kwenye shule ya jirani.
Kisha yeye afuatilie utekelezaji. Kwa kitendo chake cha kukataa tena hadharani sio picha nzuri
 
Katemeshwa ngese hivi hivi

On a serious note: Ukute ni muvi imeandaliwa, TZ kuna chip plotiks kama nini

Unadhani rais huwa anasupraiziwa? Intelijensia yake ina kazi gani sasa? Hata sumu si atapewa?

Walifanya vibaya, wangemfungia kiparcel maskini.
 
ingekuwa ni vizuri angeuza yeye mwenyewe na kukabithi fedha kwa walengwa moja kwa moja, la sivyo wasio na maadili wataiweka mikononi mwao.
 
Nadhani ilikuwa ni ungwana kwa rais kuipokea kushukuru kisha kuomba iuzwe na pesa zake kupewa watoto yatima. Alichofanya ni kama kuionesha hiyo kampuni kuwa imekosea. Ameogopa yaliyomkuta Mkapa. Kila mazingira/shughuli huendana na zawadi zake. Ukienda Arusha au Shinyanga utapewa zawadi ya mbuzi au ng'ombe, ukienda Mtwara utapewa zawadi ya korosho au samaki nchanga(panya) Na hao wamempa dhahabu kwakuwa ndicho wanachozalisha. Ingekuwa ajabu wakampa mpunga au ndizi! Na zawadi kusema kweli hata kama huipendi au unaiogopa huwa huoneshi hivyo hadharani. Na sio busara kuigawa tena hadharani mbele ya waliokupa. Sasa hao waliompa walijisikiaje?
 
mil 16 ? hata mimi kama ndo rais nakataa amejibu vizuri "afanyie nini?" hela kidgo ivyoo?
 
Unafiki ni adui wa taifa hili,tutakwisha kwa unafiki...
 
Back
Top Bottom