Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Adrian Stepp

R I P
Joined
Jul 1, 2011
Posts
2,764
Reaction score
2,600
THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

[TABLE="width: 655"]
[TR]
[TD="width: 239"] Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
[/TD]
[TD="width: 104"][/TD]
[TD="width: 270"] PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameirudishia Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya Mkoani Geita zawadi ya gramu 227 za dhahabu safi akielekeza kuwa zawadi hiyo itumike kuwasaidia watoto yatima.

Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu, Novemba 11, 2013, baadaya kukabidhiwa zawadi ya dhahabu hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua mgodi wa uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogo wa Kharuma ambako ndiko makao makuu ya wilaya mpya ya Nyang'hwale,Mkoa wa Geita.

Gramu hizo 227 ambazo ni sawa na aunzi nane zina thamani ya Sh. milioni 16 kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.

Baadaya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais Kikwete ameuliza: "Sasa nifanye nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popote mnakotaka na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima."

Akizungumza na wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete ameupongeza uongozi wamgodi huo akisema kuwa umeongeza thamani ya dhahabu na ya maisha yawananchi katika eneo hilo nje ya mji mdogo wa Kharuma.

Hatahivyo, Rais Kikwete ameushauri uongozi wa mgodi huo kufanya jitihada za kuboresha teknolojia inayotumika. "Mmefanya vizuri sana na mgodi huu ni mradi wa maana sana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili. Ubunifuhuu unastahili pongezi."

Ameongeza Rais Kikwete: "Lakini lazima tuboreshe teknolojia. Teknolojia inayotumika kwenye mgodi huu bado ni ya zamani kidogo. Hii ni sawa na hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii ya vipofu watupu. Yeye anaonekana kama mfalme."

Mgodi wa Nyamigogo ambao ni mgodi wa marudio kwa maana ya kwamba unazalishadhahabu kutokana na mchanga ambao huko nyuma umepata kufuliwa nakutoa dhahabu, ulianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa zimewekezwa kiasicha Sh.bilioni 1.6 katika uendelezaji wa mgodi huo.

Risala ya uongozi wa mgodi huo inasema kuwa mgodi huo unaozalisha kiasi chagramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi na unaajiri watu 45 wakiwemo wanawake 10.

Tokea kuanzishwa kwake, mgodi huo umekuwa unaunga mkono shughuli za jamii inayouzunguka ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati na madarasa yashule katika vijiji viwili.

Rais Kikwete amezindua mgodi huo ikiwa sehemu ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika ziara yake rasmi ya kikazi katika Mkoa waGeita, moja ya mikoa minne ambayo aliianzisha mwaka jana. Mikoa mingine ni Simiyu, Njombe na Katavi.

Ziara hiyo ya siku tano inamalizika kesho, Jumanne, Novemba 12, 2013, na mbali ya kuzindua mgodi huo, Rais Kikwete leo amepokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Nyang'hwale na kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kharuma uliohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi.

Rais kikwete anatarajia kufanya majumuisho ya ziara yake Jioni ya leo!

Imetolewana:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam.
11Novemba, 2013
 
Rais Kikwete leo kapewa zawadi ya bonge la dhahabu yenye uzito wa granu 227 kutoka mgodi wa Nyamigogo mkoani Geita. Lakini akawauliza "niipeleke wapi sasa hii dhahabu?"
Akatangaza palepale hadharani kuirudisha dhahabu ile kwa waliomtunza na akawaambia waiuze ili wawasaidie watu na watoto wasiojiweza wanaozunguka mgodi huo.
Dhahabu hiyo ikiuzwa kwa soko huria la leo ina thamani ya shilingi milioni 16
 
Unasifia ujinga, badala ya kujiuliza taifa ni wapi lilipopotea ? ukiona tumewaweka migodini watu kuchimba madini na kuendekeza zawadi za dhahabu kwa viongozi jua taifa limekwisha
 
Unasifia ujinga, badala ya kujiuliza taifa ni wapi lilipopotea ? ukiona tumewaweka migodini watu kuchimba madini na kuendekeza zawadi za dhahabu kwa viongozi jua taifa limekwisha

Mkuu
Unaweza kunionyesha sehemu niliposifia chochote katika maandiko yangu?
 
Rais Kikwete leo kapewa zawadi ya bonge la dhahabu yenye uzito wa granu 227 kutoka mgodi wa Nyamigogo mkoani Geita. Lakini akawauliza "niipeleke wapi sasa hii dhahabu?"
Akatangaza palepale hadharani kuirudisha dhahabu ile kwa waliomtunza na akawaambia waiuze ili wawasaidie watu na watoto wasiojiweza wanaozunguka mgodi huo.
Dhahabu hiyo ikiuzwa kwa soko huria la leo ina thamani ya shilingi milioni 16

Aktaka tumuamini akatae zile ridhiwan anazochota za familia GEITA GOLD MINING KILA SKU NA BARRICK KWA SIKU BILIONI 1 HUO NI UNAFKI ..AKATAE NA TENDA ALIZOFORCE FAMILIA YAKE IKACHUKUA KUPTIA PUMA NA WAKAMFUKUZA MKURUGENZI MKUU WA TANESCO KWA KUKATAA KAMPUN YA FAMILIA YA JK,,PIA AKATAE NA TENDA YA KSHERIA WALIYOMSMAMISHA KAZ LAWRENCE MAFURU WA NBC BAADA YA KUKATAA KUIPA GRK ADVCATE TERNDA YA KUSMAMIA KES ZA NBC WAKAT MAFURU ALISEMA NI KAMPUN YA KHUN HAINA CV ...PIA AKATAE MKAKAT WANAOUFANYA ILI KUMNYANG'ANYA MKONO TENDA ZA TANESCO ..PIA AKATAE PESA ANAZOLIPWA KUPTIA IPTL ..AKATAE TENDA WANAZOCHUKUA KILA SEKTA KUPTIA LUGUMI INTERPRISES HAYO NI MACAHACHE BADO ZLEE BIASAHARA ZETU ZILEEEEEEEEE
 
JK ana busara sana, ingekuwa ni babu angepokea.

wewe mbona juzi nilimuona akipokea kamba za ngombe na vitenge vya mke wake huko geita ...star tv wakati akizindua mkoa geita kwenye vumbi
 
sehemu nilizowekea red niambieni kama hawa watu waliajiriwa kwa sifa au ni kujuana!!!!!!!!!!!

theunited republic of tanzania

directorateof presidential communications

[table="width: 655"]
[tr]
[td="width: 239"] telephone: 255-22-2114512, 2116898
e-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
fax: 255-22-2113425

[/td]
[td="width: 104"]

[/td]
[td="width: 270"] president’s office,
the state house,
p.o. Box 9120,
dar es salaam.
tanzania.
[/td]
[/tr]
[/table]

taarifakwa vyombo vya habari

raiskikwete arudisha zawadi ya dhahabu

raiswa jamhuri ya muungano wa tanzania, mheshimiwa jakaya mrisho kikweteameirudishia kampuni ya nyamigogo grand vezir holdings ya mkoanigeita zawadi ya gramu 227 za dhahabu safi akielekeza kuwa zawadi hiyoitumike kuwasaidia watoto yatima.

raiskikwete ametoa maelekezo hayo leo, jumatatu, novemba 11, 2013, baadaya kukabidhiwa zawadi ya dhahabu hiyo wakati wa sherehe ya kuzinduamgodi wa uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogowa kharuma ambako ndiko makao makuu ya wilaya mpya ya nyang’hwale,mkoa wa geita.

gramuhizo 227 ambazo ni sawa na aunzi nane zina thamani ya sh. Milioni 16kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.

baadaya kukabidhiwa zawadi hiyo, rais kikwete ameuliza: “sasanifanye nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popotemnakotaka na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima.”

akizungumzana wananchi katika mgodi huo, rais kikwete ameupongeza uongozi wamgodi huo akisema kuwa umeongeza thamani ya dhahabu na ya maisha yawananchi katika eneo hilo nje ya mji mdogo wa kharuma.

hatahivyo, rais kikwete ameushauri uongozi wa mgodi huo kufanya jitihadaza kuboresha teknolojia inayotumika. “mmefanyavizuri sana na mgodi huu ni mradi wa maana sana kwa kuongeza thamaniya dhahabu na kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili. Ubunifuhuu unastahili pongezi.”
ameongezarais kikwete: “lakinilazima tuboreshe teknolojia. Teknolojia inayotumika kwenye mgodi huubado ni ya zamani kidogo. Hii ni sawa na hadithi ya mtu mwenye chongokatika jamii ya vipofu watupu. Yeye anaonekana kama mfalme.”

mgodiwa nyamigogo ambao ni mgodi wa marudio kwa maana ya kwamba unazalishadhahabu kutokana na mchanga ambao huko nyuma umepata kufuliwa nakutoa dhahabu, ulianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa zimewekezwa kiasicha sh.bilioni 1.6 katika uendelezaji wa mgodi huo.

risalaya uongozi wa mgodi huo inasema kuwa mgodi huo unaozalisha kiasi chagramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi na unaajiri watu 45 wakiwemowanawake 10.

tokeakuanzishwa kwake, mgodi huo umekuwa unaunga mkono shughuli za jamiiinayouzunguka ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati na madarasa yashule katika vijiji viwili.

raiskikwete amezindua mgodi huo ikiwa sehemu ya kukagua na kuzinduamiradi ya maendeleo katika ziara yake rasmi ya kikazi katika mkoa wageita, moja ya mikoa minne ambayo aliianzisha mwaka jana. Mikoamingine ni simiyu, njombe na katavi.

ziarahiyo ya siku tano inamalizika kesho, jumanne, novemba 12, 2013, nambali ya kuzindua mgodi huo, rais kikwete leo amepokea ripoti yamaendeleo ya wilaya ya nyang’hwale na kuhutubia mkutano wa hadharakatika mji mdogo wa kharuma uliohudhuriwa na mamia kwa mamia yawananchi.

imetolewana:
kurugenziya mawasiliano ya rais,
ikulu.
dares salaam.
11novemba, 2013
 
Aktaka tumuamini akatae zile ridhiwan anazochota za familia GEITA GOLD MINING KILA SKU NA BARRICK KWA SIKU BILIONI 1 HUO NI UNAFKI ..AKATAE NA TENDA ALIZOFORCE FAMILIA YAKE IKACHUKUA KUPTIA PUMA NA WAKAMFUKUZA MKURUGENZI MKUU WA TANESCO KWA KUKATAA KAMPUN YA FAMILIA YA JK,,PIA AKATAE NA TENDA YA KSHERIA WALIYOMSMAMISHA KAZ LAWRENCE MAFURU WA NBC BAADA YA KUKATAA KUIPA GRK ADVCATE TERNDA YA KUSMAMIA KES ZA NBC WAKAT MAFURU ALISEMA NI KAMPUN YA KHUN HAINA CV ...PIA AKATAE MKAKAT WANAOUFANYA ILI KUMNYANG'ANYA MKONO TENDA ZA TANESCO ..PIA AKATAE PESA ANAZOLIPWA KUPTIA IPTL ..AKATAE TENDA WANAZOCHUKUA KILA SEKTA KUPTIA LUGUMI INTERPRISES HAYO NI MACAHACHE BADO ZLEE BIASAHARA ZETU ZILEEEEEEEEE

Pamoja na kuwa wewe una maslahi kutokana na kuwa kambi tofauti za urais huko,nakubaliana na wewe kwa yale ya kweli uliyoandika hapa
 
Hiyo haikuwa zawadi bali ulikuwa ni mtego.

Kimoyomoyo anasikitika kweli!
 
Gram 227 ndo unaita bonge? tena ina thamani ya milioni 16 tuuu ndo unampa JK? ndo maana kaikataa kaona kwanza wamemdhalilisha wangeandaa kitofali kama vile vya choma muone kama angekataa
 
Hapa sielewi! Mlitaka Raisi afanye nini na zawadi hii, aichukue na aitumie mwenyewe kwa faida yake au nini!? Hivi kweli hamuoni kwamba hili alilofanya Raisi ni jema kwa umma na kwa hao anaotaka wafaidi baada ya zawadi iyo - "bonge la dhahabu" kuuzwa!? Historia inatuelezea kuwa wengine walishapewa zawadi kama hizo na wakaweka ndani! Tufike mahali tupongeze maamuzi mema jamani. Hongera Raisi kwa uamuzi huu wa busara.
 
kama mlisema vile kwa suti ambazo hamkuona akipokea je dhahabu ambayo mmeona si ingekuwa balaa
 
Rais Kikwete leo kapewa zawadi ya bonge la dhahabu yenye uzito wa granu 227 kutoka mgodi wa Nyamigogo mkoani Geita. Lakini akawauliza "niipeleke wapi sasa hii dhahabu?"
Akatangaza palepale hadharani kuirudisha dhahabu ile kwa waliomtunza na akawaambia waiuze ili wawasaidie watu na watoto wasiojiweza wanaozunguka mgodi huo.
Dhahabu hiyo ikiuzwa kwa soko huria la leo ina thamani ya shilingi milioni 16
team promo..........
 
Back
Top Bottom