Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,999
Mnyonge Mnyongeni...........hapa Jk Anahitaji Pongezi.. Wise And Brave Decision. Isije Ikawa Tu Ndio Chanzo Cha Kumfunga Mdomo 'dogo',si Mnakumbumbuka Marmo?mzindakaya? Time Will Tell.
Wana JF, tusihukumu kamati kabla haijatoa taarifa. Tuvute subira, tuone ni lipi jipya watakaloliibua. Inawezekana wakaja na taarifa nzuri. Ni mapema sana kuanza kuishambulia kamati.
OMG,
Yaani Zitto amezungukwa na kina Cheyo, Mark Bomani, na Mwakyembe? Hii kamati imekufa on arrival!
Mweh!!! watanzania tumezidi kulalamika na kupinga kila kitu, sasa kamati haijaanza kazi tushaanza kuhoji mbona fulani hayumo, tuwaache wafanye kazi kwanza. Nina uhakika ata kama wangewekwa malaika tupu bado tungehoji.
Mweh!!! watanzania tumezidi kulalamika na kupinga kila kitu, sasa kamati haijaanza kazi tushaanza kuhoji mbona fulani hayumo, tuwaache wafanye kazi kwanza. Nina uhakika ata kama wangewekwa malaika tupu bado tungehoji.
Tatizo lililokuwepo ni mikataba ya madini na inaonekana kazi ya msingi ya hii kamati ni kupitia upya hii mikataba.
Tukumbuke kuwa Mheshimiwa Jk ni mtu anaefahamu fika yaliyomo kwenye mikataba. Ni busara tukimpa nafasi kuona anataka kufanya nini. Yeye binafsi alionyesha siku nyingi kuwa kuna vitu kwenye hii mikataba vinamkera. Kwa kuunda kamati inaonyesha ameamua kufanyia kazi mtazamo wake wa hii mikataba.
Tuwe na subira tuache kupiga kelele za ramli na kutabiri matokeo.. huo ni uchawi sasa.
Tushukuru kamati imeundwa na waheshimiwa Zitto na Cheyo ambao wamekuwa wajasiri kuelezea hisia za wananchi bungeni wamo. Tuamini pia uwepo wao kwenye kamati utakuwa na matokeo mazuri kwenye kamati.
Hivi lakini hapa nimegundua kuna watu wanaona ufahari kupinga kila kitu. hata kama JK angemteua Shivji na Lissu kwenye kamati bado wangepinga tu. JK alipokaa kimya tulilalamika, akichukua hatua anaitwa msanii. Tusubirini kidogo jamani hata kamati hawajatoa tamko tunalalama.... Mwe!