Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 612
JK amteua Zitto kamati ya madini
MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
RAIS Jakaya Kikwete, amemteua Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Jaji Mark Bomani na kuongoza Kamati ya Kuangalia upya Mikataba ya Madini, ikijumuisha wabunge wawili wa upinzani na wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, imewataja wabunge wa upinzani waliomo katika kamati hiyo kuwa ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kupitia Chadema, Zitto Kabwe na Mbunge wa Bariadi Mashariki, Chadema, John Cheyo.
Kwa upande wa CCM wabunge walioteuliwa yumo Dk. Harrison Mwakyembe wa Kyela na Ezekiel Maige wa Msalala. Wajumbe wengine wametajwa kuwa ni pamoja na Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba.
Wengine ni Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.