Rais Kikwete amteua Zitto kamati ya Madini

Mnyonge Mnyongeni...........hapa Jk Anahitaji Pongezi.. Wise And Brave Decision. Isije Ikawa Tu Ndio Chanzo Cha Kumfunga Mdomo 'dogo',si Mnakumbumbuka Marmo?mzindakaya? Time Will Tell.

kanaKansungu, apongezwe kwa kufanya kazi kwa shinikizo? Kwa kukubali kuunda Kamati na kumuweka Zitto ndani ina maana amekubali siyo tu kuna matatizo bali matatizo makubwa. Kwanini basi Zitto alifungiwa na kwanini Karamagi alisema mjadala kuhusu kudurusu mikataba umekoma? Kuna mambo ya kupongeza hili ni la kushukuru tu kuwa angelifanya mwaka mmoja uliopita!
 
Kwa Mwanzo huu wa kumchagua Mh.Zitto kuwepo kwenye hiyo kamati ya Madini ni wazi kwamba Rais atamuondoa Karamagi ktk Wizara ya MADINI.Sina wasiwasi sana na Uteuzi wa hao Wajumbe wa Kamati,haswa ukizingatia kuwepo kwa Jaji Bomani na Dr Mwakyembe,kwani hao wote kwa wakati tofauti wameonyesha kuwa kuna upungufu ktk suala zima la Mikataba ya Madini.Ili Tume iwe Huru na ifanye kazi bila kuingiliwa ni wazi kuwa Karamagi ataondolewa kwenye Wizara ya MADINI.
 
Wana JF, tusihukumu kamati kabla haijatoa taarifa. Tuvute subira, tuone ni lipi jipya watakaloliibua. Inawezekana wakaja na taarifa nzuri. Ni mapema sana kuanza kuishambulia kamati.
 
Wana JF, tusihukumu kamati kabla haijatoa taarifa. Tuvute subira, tuone ni lipi jipya watakaloliibua. Inawezekana wakaja na taarifa nzuri. Ni mapema sana kuanza kuishambulia kamati.

Hii Kamati kwa jinsi ilivyo, ninaweza kuandika report watakayotoa baada ya kutafuna mabilioni ya pesa.

Huwezi kuwa serious unaunda kamati ya madini eti unamweka Cheyo, Mark Bomani, na Mwakyembe!

Hapa ni uchemfu mkubwa na kama kawaida Kikwete anaendeleza usanii wake hapa! damn this guy siku akiondoka nchi itakuwa imekwisha hiyo
 
OMG,

Yaani Zitto amezungukwa na kina Cheyo, Mark Bomani, na Mwakyembe? Hii kamati imekufa on arrival!

Mwafrika wa Kike, kwa taarifa yako Dr Mwakyembe pamoja na kuwa CCM, lakini ana msimamo kama vile yuko upinzani; hataki ku-entertain ufisadi unaondelea ndani ya serikali ya CCM ... kwa inaonekana JK anataka kufanya kweli this time!
 
Hiyo kamati bila ya kuwa na meno haitakuwa na lolote.Mimi naona kwenye hiyo kamati ni Zito tu,huyo cheyo ni heri aondelewe mara moja awekwe hata Butiku.
Pili Je itapewa nguvu ya kuhoji mtu yeyote yule bila ya kutishwa tishwa? na mamlaka husika au ni wapi itachorwa mipaka ya nguvu ya kamati hii.
Tatu kwa nini wasomi na wanaharakati kama akina Shivji hawajawekwa kwenye hiyo kamati kama kweli tunataka ufumbuzi wa matatizo ya mikataba hii.
Wembe
 
Inabidi kumpongeza JK kwa kuunda kamati hii. Sasa Zitto atumie maoni yetu kuimarisha hiyo mikataba.
 
Mweh!!! watanzania tumezidi kulalamika na kupinga kila kitu, sasa kamati haijaanza kazi tushaanza kuhoji mbona fulani hayumo, tuwaache wafanye kazi kwanza. Nina uhakika ata kama wangewekwa malaika tupu bado tungehoji.
 
Mimi nashukuru kumuweka Zito lakini pia sikuona kwa nini kamati haijawahusisha wataalamu wa sheria haswa kama Shivji ambaye ameonekana kuonyesha ubovu wa sheria tulizonazo.

Hapa nina wasiwasi kama kweli watawala wetu wako makini. Hivi wataalamu kama shivji ni wakufundisha tu vyuo? Hivi tunahitaji sheria kweli za kutukomboa kututoa katika midomo ya Mabepari? Au tunatengeneza sheria za kuwasaidia mabepari. Anyway CHey angelipunguzwa kwenye hiyo tume.
 
Mweh!!! watanzania tumezidi kulalamika na kupinga kila kitu, sasa kamati haijaanza kazi tushaanza kuhoji mbona fulani hayumo, tuwaache wafanye kazi kwanza. Nina uhakika ata kama wangewekwa malaika tupu bado tungehoji.

Mweh,

ulishakuwa rais wa china au russia hapa kuamulia watu cha kusema tena?

Kama memba hapa anaona kuwa kamati imewekwa watu wasiofaa basi ana kila haki ya kuhoji hiyo kamati na legitimacy yake unless kama unataka kusema kuwa hapa ni china, or north korea!
 
..hakuna kitu hapo ni usanii tuu na hakuna hata mkataba mmoja uliokwisha sainiwa utabadilishwa,msicheze na kitu inaitwa contract na huku nchi yako ikitegemea almost nusu ya budget kutoka kwa hao wazungu,tumeliwa basi inatosha kinachotakiwa sasa ni kubadilisha policy zote za madini ili mikataba ijayo iwe kwa faida yetu ili sio kutuzuga na kutupotezea muda na pesa eti kuangalia upya mikataba ya madini huku wakijua hakuna kitu wanaweza kubadilisha
 
Mweh!!! watanzania tumezidi kulalamika na kupinga kila kitu, sasa kamati haijaanza kazi tushaanza kuhoji mbona fulani hayumo, tuwaache wafanye kazi kwanza. Nina uhakika ata kama wangewekwa malaika tupu bado tungehoji.

Mkuu Icadon

Siyo kulalamika ni Mitazamo tofauti.
 
Tatizo lililokuwepo ni mikataba ya madini na inaonekana kazi ya msingi ya hii kamati ni kupitia upya hii mikataba.

Tukumbuke kuwa Mheshimiwa Jk ni mtu anaefahamu fika yaliyomo kwenye mikataba. Ni busara tukimpa nafasi kuona anataka kufanya nini. Yeye binafsi alionyesha siku nyingi kuwa kuna vitu kwenye hii mikataba vinamkera. Kwa kuunda kamati inaonyesha ameamua kufanyia kazi mtazamo wake wa hii mikataba.

Tuwe na subira tuache kupiga kelele za ramli na kutabiri matokeo.. huo ni uchawi sasa.

Tushukuru kamati imeundwa na waheshimiwa Zitto na Cheyo ambao wamekuwa wajasiri kuelezea hisia za wananchi bungeni wamo. Tuamini pia uwepo wao kwenye kamati utakuwa na matokeo mazuri kwenye kamati.
 
Hivi lakini hapa nimegundua kuna watu wanaona ufahari kupinga kila kitu. hata kama JK angemteua Shivji na Lissu kwenye kamati bado wangepinga tu. JK alipokaa kimya tulilalamika, akichukua hatua anaitwa msanii. Tusubirini kidogo jamani hata kamati hawajatoa tamko tunalalama.... Mwe!
 
Wazee naomba kuuliza swali tu Hivi Hadidu za Rejea maana yake nini maana mmeniacha kabisa na sielewi maana yake. Tafadhalini.
 
Tatizo lililokuwepo ni mikataba ya madini na inaonekana kazi ya msingi ya hii kamati ni kupitia upya hii mikataba.

Tukumbuke kuwa Mheshimiwa Jk ni mtu anaefahamu fika yaliyomo kwenye mikataba. Ni busara tukimpa nafasi kuona anataka kufanya nini. Yeye binafsi alionyesha siku nyingi kuwa kuna vitu kwenye hii mikataba vinamkera. Kwa kuunda kamati inaonyesha ameamua kufanyia kazi mtazamo wake wa hii mikataba.

Tuwe na subira tuache kupiga kelele za ramli na kutabiri matokeo.. huo ni uchawi sasa.

Tushukuru kamati imeundwa na waheshimiwa Zitto na Cheyo ambao wamekuwa wajasiri kuelezea hisia za wananchi bungeni wamo. Tuamini pia uwepo wao kwenye kamati utakuwa na matokeo mazuri kwenye kamati.

Hii kamati na ile ya kwanza ilokuwa inapitia madini wakati Karamagi akisaini mkataba London ina tofauti gani? Taifa la watanzania liliambiwa kuwa mapendekezo mapya ya mikataba ni mazuri na kuwa mkataba wa Buzwagi ndio umeboreshwa zaidi?

Kinachosemwa hapa ni nini?
 
Hivi lakini hapa nimegundua kuna watu wanaona ufahari kupinga kila kitu. hata kama JK angemteua Shivji na Lissu kwenye kamati bado wangepinga tu. JK alipokaa kimya tulilalamika, akichukua hatua anaitwa msanii. Tusubirini kidogo jamani hata kamati hawajatoa tamko tunalalama.... Mwe!

Nurujamii,

Ulishaambiwa hapa JF hakuna anayependelewa na ndio maana wale wanaopondea JF kila mara kuwa ni kijiwe cha CHADEMA walichemsha maana hapa kila mtu hata kina Mnyika hupata dosier yao.

Issue hapa ni tahadhari hata kwa huyo Zitto kama akikubali huo uteuzi wa Kikwete kujua kuwa hakuna ize ride hapa. Akikubaliana na ushenzi na spin za kina Mwakyembe na Mark Bomani atapata the same standard toka kwa JF members.

So far, issue ya kumweka Mwakyembe na Mark Bomani kwenye hii kamati ni ushahidi tosha kuwa usanii unatumika hapa. Hii kamati imepewa onyo na wanaJF kuwa watanzania hawataki usanii kwa hiyo kila kinachosemwa hapa ni muhimu!
 
Wana JF nadhani tufike mahali tutumie Busara. Tukitaka kila mtu awepo kwenye kamati basi kutakuwa na watu wengi saaana. Ikumbukwe kwamba hii kamati

itatumia pesa za walipa kodi kuweza kutekeleza majukumu yake watu wakiwa wengi peas zaidi.

ikumbukwe kwamba hii kamati haitakaa ndani ya chupa kujifungia huko wakati inafanya kazi yake. Itahitaji ushauri wa kitaalum kutoka kwa watu wengine pale inapobidi kufanya hivyo

Hivyo basi badala ya kuanza kuponda kama huu ni wakati wa kuwapa inputs ili wanapifanya mchakato huo wajue ni vitu gani vimekosekana viongezwe, vipunguzwe, n.k

Nawakilisha hoja
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom