Rais Kikwete akifanya mazoezi arusha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete akifanya mazoezi arusha.

Discussion in 'Jamii Photos' started by tz1, Jun 3, 2012.

 1. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ti1.jpg

  ti3.jpg Anavyo penda pamba hadi kasahau kama Ccm wana track suti zao.  936_21306403.jpg Akijitahidi kidogo akaacha safari atakuwa kama huyu jamaa.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ameenda kufanya mazoezi nyumbani kwa Lwaiganan.... ha ha ha ha...JK kiboko!
   
 3. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Sema hivi jk akifanya mazoezi hotelini maana hapo ni ngurudoto
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  mwambieni ajiunge na kitambi fc
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Big up Jk, hivi Dr Slaa anafanyaga mazoezi?
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaa sio bishoo ndio maana huwezikujua kama anafanya mazoezi!! Lakini si unamuona alivyokuwa physically fit; hana kitambi!!
   
 7. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,279
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Within hotel premises
   
 8. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  CCM na CHADEMA tukichukulia ni kama SIMBA na YANGA tutapotoka.
   
 9. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  kula vizuri, fanya mazoezi utaishi mda mrefu.
   
 10. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 35
  Mzee unamaanisha au unatania?yaani kitambi kilivyomtepeta bado unasema hana kitambi!au siyo slaa huyu?
   
 11. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  What u mean here
   
 12. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Anatamba sasa baada ya Lema kuporwa ubunge, wakati Lema ni kidume wa jiji asingethubutu kutamba na track suit zake.
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata kama hauitendei nchi yako haki? Hata kama hautekeleze kile kiapo cha kuitetea na kuilinda katiba ya Tanzania?
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Porojo tu hizo hana lolote!
   
 15. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Tukichukulia hivyo, bora CDM iwe Simba! LOL
   
 16. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  kaunga umeonaeee, 2015 ccm tutawaimbia dada huyo ameolewa, nasikia mahari ya ccm tayari, kwikwikwi! Mboni yangu mie! Muumba juu atupe pumzi tu, tushuhudie! Amen!
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Jk anapasha safi sana
   
 18. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #18
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani taifa linapotoka hapa jamvini sioni hata mmoja wetu mwenye constructive criticism, hivi kwanini tusijenge utamaduni wa kusifia panapo stahiki na kukosoa/kushauri panapo upungufu. Rais wetu kufanya mazoezi ni jambo zuri sana kiafy, je na wewe unafanya mazoezi?
  Basi jifunze nini maana ya mazoezi!
   
 19. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.

  "Ndugu Wananchi;


  Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

  "Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge".

  Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .

  Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

  Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni "Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu " umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako , hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa , Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar , mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

  Mh Rais , Mama Theresa , Nelson Mandela , Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao , sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu , nahitaji dhamira safi , nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini , nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya , ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta , magorofa , magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki ,Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo, pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi , Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe , hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho , nitakufa siku moja ambayo siijui , napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana , lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki , kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana , unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako , niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

  Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

  Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

  Mh Rais "Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri" Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

  "ONLY TIME WILL TELL".


  GODBLESS .J. LEMA.
   
 20. M

  Mubii Senior Member

  #20
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huu ni mfano mzuri kwa Watanzania. Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kuwa na afya njema.
   
Loading...