Jamani kama sikosei kisheria Mh. Rais kama mtumishi wa umma, anayo haki na stahiki ya kwenda likizo ya mwezi kila mwaka kama ilivyo kwa watumishi wote wa umma.
Hata kwa wenzake waliomtangulia walienda likizo mara kwa mara na sote tulifahamu hili. Kwa jinsi mambo yalivyo mengi sasa hivi nchini tunahitaji uongozi uliotimamu kifikra na kimwili ili kuweza kupeleka mambo inavyotakiwa kwa kiasi cha kutosha.
Ni vigumu kuwa fiti kifikra na kimwili kwa mtu yeyote kwa kufanya kazi miaka miwili mfululizo bila kupumzika hata kama unahudumiwa kiasi gani. Na kwa kuzingatia ukubwa wa majukumu yake, ni vigumu kuamini kama binadamu wa kawaida anaweza kumudu na akaweza kutoa matokeo chanya katika majukumu yake.
Tumshauri huyu anaeratibu shughuli na ratiba za Mh. Rais akumbuke kumpa Mh. Rais likizo kwani ni haki yake kisheria na kwa mstakabali mzima wa Taifa na watu wake kwa ujumla.
Tunaweza kulaumu baadhi ya mambo yanavyokwenda bila kutambua kuwa, kuna mtu anafanyishwa kazi mpaka brain inashindwa kutoa maamuzi.