Rais Dkt. Mwinyi Aipongeza UWT kwa Kazi Kubwa Wanayoifanya Ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Chini ya Mwenyekiti wao Mary Chatanda kwa kazi kubwa wanayoifanya katika Nchi hii kwa kutembelea miradi na kufanya Mikutano ya Hadhara mbalimbali pamoja na kazi kubwa ya Kuimarisha Chama ndani ya Tanzania Bara na Visiwani .

Mhe. Dkt. Mwinyi amesema Nimefurahishwa na Umoja wenu ambao mmefanya kazi kubwa ya kutembelea miradi na kuangalia Utekelezaji wa Ilani ulivyofanyika kwa kasi juu hivyo naomba niwapongeze sana Umoja wa wanawake Tanzania .

"Nianze kwa kutoa pongezi nyingi kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Tumeridhika na kazi kubwa na kazi nzuri wanayoifanya nchi nzima, Bara na Visiwani, hongereni sana" - Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

"Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa hamasa, Niwapongeze kwa kutembelea miradi ya Maendeleo kwa kuona ni kwa kiasi gani Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imetimizwa kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" - Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

"Kipindi kilichobaki cha miaka miwili nataka nitoe ahadi kwenu kwamba kasi (Speed) yetu itakuwa ni kubwa zaidi katika kutekeleza Ilani ya CCM 2020-2025" - Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

"Tumeridhishwa na Mwendo mlionyeshe katika kuhakikisha mnaendelea kuangalia Utekelezaji wa Ilani kwetu sisi ni furaha kubwa sana kwa kuwa Wanawake ni Jeshi kubwa katika Taifa Letu ."

UWT IMARA JESHI LA DKT. SAMIA NA DKT. MWINYI KAZI IENDELEE

F-HTrX0XQAABIE_.jpg
F-HTrX5W8AAFCdQ.jpg
F-HHznyXoAAsr4vmnju.jpg
F-NTyMwXgAACrEQ.jpg
F-F-1p8XEAADMGJ.jpg
F-HR5JHXIAAhBbG.jpg
F-HTrX5XwAANW3u.jpg
 
Back
Top Bottom