Rais bora atatoka CCM - Mwalimu Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais bora atatoka CCM - Mwalimu Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Oct 14, 2010.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Watu wngi hapa nchini wamekuwa wakitumia nukuu mbalimbali za Mwl Nyerere pale wanapotaka kukosoa ama ku-support jambo fulani. Nilifuatilia kwa makini moja ya hotuba zake akiwa anahutubia mkutano mkuu wa CCM na alisema,

  Nanukuu" KATIKA MFUMO HUU WA VYAMA VINGI, RAIS ANAWEZA KUTOKA KATIKA CHOCHOTE. LAKINI, RAIS BORA NI LAZIMA ATOKE CCM!

  Tatizo letu sisi Watanzania tumekuwa kama bendera, tunafuata upepo unapovuma. Kama kweli tunampenda na kumthamini na kuthamini mawazo na hekima za Mwl Nyerere, hatuna budi kumchagua JK na hapo ndipo tutakuwa tunamuenzi Baba wa Taifa ktk hii miaka 11 ya kifo chake.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huo ubora wa JK ambaye hata hajui kwa nini nchi ni maskini ni upi? Kama kweli JK ana uchungu na nchi yetu awachukulie mafisadi hatua badala ya kuwapamba kwenye mikutano ya kampeni na kwingineko kwamba ni "panga la zamani," "kesi yake ndogo atashinda," "ni ajali tu ya kisiasa," nk! Atumie muda mwingi kutatua matatizo yetu badala ya kuzurura kwenye nchi za watu na kuponda starehe huku akiacha raslimali za nchi zikikwapuliwa na wageni! Kama ubora wa JK ni huo basi hakuna haja ya kuwa na Rais kabisa!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Are you an old-cat?
  Are you living in the past?
  Na tuiache historia iwe historia!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 5. M

  Masauni JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani mtu mzima hovyo. Hivi kwa nini ninyi watanzania swala la hawa jamaa kula rushwa haliwaumi? hamuoni tatizo? hamjiulizi kwa nini CCM mioyo yao inawasuta ndo maana hata wahataki kuongelea jinsi ya kupambana na rushwa. Kwa mtindo huu tusitegemee hipo siku tutatoka kwenye umaskini. Never
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  So na wewe ndo umeamua kutoka hivi? Unahitaji muda!
   
 7. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Huyo Nyerere wako Huyo angekuwa hai leo angemchapa viboko huyo JK. Jaribu kutathimini nini amekifanya nchi miaka 5 ya utawala wake. Jambo la kutia matumaini ni kwamba huko maofsini sijasikia mtu anamfagiliaJK, kwenye daladala hakuna anayemfagilia, jana niliuliza wanafunzi kama wangekuwa wapiga kura mwaka huu wangemchagua nani, kwa kauli 1 bila chenga wanasema CCM hawafai hata kupewa ujumbe wa nyumba kumi kumi!
  Sasa najuuliza mtu atakaye wapigia kura ni nani?
   
 8. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  Aisee!
  Kulitoa taifa hili kutoka huku tuliko kwenda kule kumbe ni kazi kubwa hivi eee?!
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Shimbo & Co
   
 10. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Marais wametoka CCM na mamake TANU kwa miak 50 lakini taifa linazidi kudidimia. Sasa tunabadilisha chama tawala. Huwezi ukachagua watu wale wale kila wakati na ukategemea kuweko na tofauti. Kuanzia sasa, Urais ni miaka 5; kama kuna kitu unaendelea la sivyo unapisha mwingine.

  Lazima kubadilisha CHAMA TAWALA mwaka huu. Tumekichoka hiki kilichopo, kimekuwa kinajizatiti kwenye anasa za viongozi tu na kusahau wananchi. Kwaheri CCM, karibu CHADEMA.

  Tanzania is about to be born again!
   
 11. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Aliyoyafanya JK hamyaoni? UDOM, barabara, umeme na maji(nenda kaone mkoa wa Kigoma) pia kapitisha sheria za gharama za uchaguzi, sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na. 11/2007 hata wapinzani ruzuku zimeongezwa na sasa hata ukiwa na diwan unapata ruzuku. Si hayo tu, amejenga shule za kaka ktk kila kata na hata ule uthubutu wa kuwafikisha mahakamani mawaziri, wkurugenzi na makatibu wakuu si jambo la kubeza.Nadhani mnayajua mengi mazuri kuliko mimi. Jamani, MNYONGE MNYONGENI LAKN HAKI YAKE MPENI
   
 12. u

  urasa JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe unatoka ****** huku mikono yako hujanawa then unakwenda moja kwa moja kwenye keyboard kuandika huu utumbo wako,nawa mikono yako kwanza i gues utaandika kitu constructive
   
 13. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Nimeamini wana CCM na wapambe wao wote akili zao ndogo,

  JK anawafagilia kina Mramba na Lowasa, hulioni hilo. Shule za kata juhudi za wananchi na serikali imeshindwa kupeleka walimu na kujenga maabara. Sheria ya gharama za uchaguzi anavunja mwenyewe kampeni anamaliza baada ya saa 12 jioni, anapandisha mishahara katika kampeni.

  Kwanini una uwezo mdogo kiasi hicho?
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Pointless.
   
 15. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nimeamini wewe jamaa ni wa ajabu sana! Labda umepewa rushwa ya kupewa uwaziri mara baada ya uchaguzi! Tafadhali sana ujue hii nchi ni ya Watanzania wote! Hao mafisadi wako unaowatea ndo wametuleta hapa tulipo! Hivi hujui mpaka leo shule unazosema zimejengwa kwa nguvu ya wananchi halafu mafisadi wameiba fedha za umma na kwa maana hiyo kushindwa kuajiri na kusomesha walimu wa kutosha? Nenda kajifunze Rwanda leo uone wanafanya nini na hapo utajua tumelela.
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  kaumza ni kweli mwalimu aliwahi pia kutamka maneo hayo. Lakini pia aliwahi kutamka kuwa ccm ni kama "nyavu za korokoro, imesomba ndani yake wabaya na wazuri".

  Kutokana na kukerwa na vitendao vya ccm kufumbia macho vitendo vya wizi, ubadhirifu na ufujaji wa mali ya umaa mwaka 1995 mwalimu nyerere alikwenda mbele zaidi kwa kutamka" kuwa ccm sio mama yangu mzazi, hivyo katika ubunge wa musoma vijijini nitamchagua mgombea wa nccr mageuzi balozi paul ndobo na sio mgombea wa ccm dr emmenuel magottti, mwenye tuhuma za ufisadi wa kufilisi ushirika lakini akapitishwa na vikao vya ccm kugombea ubunge".

  Hivyo kwa kuzingatia hali halisi ya ilivyo ndani ya ccm sasa kutoka kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na kuwa
  chama cha wafanyabiashara, mafisadi na wabaka ucuhumi wa tanzania kutokana na viongozi wake kugubikwa na tamaa ya kujilimbikizia mali inayowapofusha kutoona tena uozo ndania yake na ndania ya taifa kwa ujumla;

  na kwa kuzingatia kiwango cha uporomokaji wa maadili ndani ya ccm na hivyo kama chama tawala kuambukiza taifa zima; baada ya miaka 10 ya watanzania kuendelea kuwa na imani na ccm baada ya nyerere umewadia wakati watanzania wakafanya tafakari ya matamko mbali mbali ya mwalimu dhidi ya ccm naviongozi wake kwa nia ya kuiokoa tanzania.

  Kauli ya mwalimu kuwa ccm imeoza inapaswa kupatiwa kipaumbele sasa na watanzania wote wanaccm na wasio wanaccm na wachukue hatua za kuwapigia kura wagombea kutoka vyama vingine ambao hawana tuhuma zozote za ufisadi kama alivyofanya mwalimu nyerere mwaka 1995, kwani ni ukweli usiopingika kuwa wagombe wa ccm kuanzia mgombea urias, wabunge na madiwani wana tuhuma mbali mbali za ufisadi, kushirikiana na mafisadi, kuwasafisha mafisadi au kuunga mkono vitendo vya kifisadi vinavyochochea ongezeko la umaskini, ujinga na maradhi hapa nchini.


  sababu ingine ya watanzania kutoendelea kuwa na imani na ccm ya sasa ni viongozi wake kukuza na kushamirisha matabaka hapa nchini katika kipindi cha miaka 10 kutokea mwalimu nyerere atutoke; katika uhai wake mwalimu nyerere alipiga vita matabaka hadi anaingia kaburini.

  hivyo watanzania watakuwa wanamuenzi nyerere kwa vitendo kwa kuinyima ccm kura na hatamu za kuendelea kuongoza tanzania baada ya miaka 10 ya kuhatarisha mustakabari wa tanzania (kutokea kifo chake), ili viongozi wa ccm wapate nafasi ya kukaa kando na kutubu makosa ya yao
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  Nyerere huyo huyo kwenye kikao hicho hicho cha mwaka 1997 cha Mkutano Mkuu wa CCM KILICHOMPITISHA BW. MKAPA KUWA MGOMBEA URAISI alitahadharisha na kusema yafuatayo:-

  "Watanzania wakimkosa mgombea Uraisi mwenye kukidhi mahitaji ya watanzania ndani ya CCM watamfuta nje ya CCM."

  CHAGUA DR. SLAA................CHAGUA CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
   
 18. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Siku moja tulikuwa kikao kimoja na jamaa zangu wa nchi ya karibu yaani Kenya, walisema vibaya sana kuhusu Tanzania hasa watu wake tulivyokuwa tubafikiria. Nilichukia sana ingawa nilijifanya kuwa mkakamavu kutowapa faida. Sasa wewe uliposema maneno hayo haya nimekumbuka kuwa wale jamaa walisema kweli!! We think different from normal humans; we are cronned!
  Eti kwa risk kubwa tuliyonayo hii at bado tufuate mawazo ya mtu aliyosema kwa wakati wake!! Mungu uwape akili watu wako ingawa ya kufikiri kidogo! Kukosa akili ni kitu kibaya kabisa!!
   
 19. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  URASA, kila mbaya ana mazuri yake. Kikwete ni bora na CCM ni bora zaidi. Hata wewe nikikuambia utaje mazuri na mabaya ya JK, mazuri yatakuwa mengi kuliko mabaya. Sir R, hata Dar haikujengwa ndani ya siku moja. Shule zimejengwa na zitaimarika tu. Je, unajua ktk matokeo ya form 4 mwaka huu, shule za kata zilifanya vema zaidi!!! Ni kweli zimejengwa na wananchi, ila uhamasishaji ni CCM ya JK. Mbona enzi za MKAPA na MWINYI hazikujengwa? Au wananchi hawakuwepo
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Kwani ni deni kumuenzi huyo Baba wa Taifa? Je angekuwapo haya yanayofanywa na JK and kamapani yangetokea?
   
Loading...