"Rais ametoa..."Maono na Dira Pekee Vichwani Viongozi Wa CCM!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,552
11,883
" Kutokana na umri mkubwa wa chama chetu cha CCM, watu wengi wenye kasoro wamejiingiza kwenye chama hiki. Sasa kimekuwa kama dodoki ambalo linabeba vitu visafi na vichafu. Sasa tumekuwa na watu wa ajabu sana ndani ya chama chetu".
Mwl J.K Nyerere.

"Nchi yetu inaongozwa na sheria. Hatuwezi kuchagua kiongozi asiyeheshimu sheria akawa anaongoza nchi kwa kushauriwa na mkewe, maana hamjui kesho akiamka atamshauri nini".
Mwl J.K Nyerere.

" Watanzania wakiyakosa maendeleo ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM".
Mwl JK Nyerere.

" Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kwa paka kufungwa kengere shingoni; tabu ni kumpata panya wa kufanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana kwa kudhani paka watajifunga au kufungana kengere".
Mwl JK Nyerere.

" Tunataka kuona vijana jeuri katika Taifa hili na wenye kujiamini na sio waoga akina " ndiyo bwana mkubwa". Tunataka kuona vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya kidhalimu isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi
Mwl J.K Nyerere.

Miaka 23 baada kifo cha Mwl Nyerere(R.I.P).
Tunaongozwa na viongozi wasiojua dira yao ni nini ili kulikomboa taifa hili kiuchumi,kielimu,kiafya na hata kisiasa pia.
Mwalimu alikuwa kiongozi mwenye dira kichwani.Na pale alipokuwa anapata fursa ya kuielezea,basi hotuba yake ilikuwa ikigeuka kuwa darasa.

Na hata ilipotokea Mwalimu Nyerere kupata fursa ya kuhutubia katika ziara zake ughaibuni ikiwemo huko umoja wa mataifa "UNO".Dunia nzima ilikuwa ikitega sikio kumsikiliza.

Na siku iliyofuatia ungeona vichwa vya habari kwenye Majarida na Magazeti Mengi maarufu Duniani.vikisheheni hotuba au nukuu zake huko.

Baadae Mzee Mkapa(R.I.P) alifuatisha mfumo huo na alifanikiwa kwa kiasi fulani kimataifa pia.

Magufuli(R.I.P),pia alijaribu kwa kiasi chake.kwani walau alithubutu kusema hadharani tena bila kuogopa.Kile ambacho yeye alitaka kiwe ndio Dira ya kulikomboa taifa hili,kutoka kwenye utegemezi na umangimeza wa kimfumo,na badala yake alinuia kuirudisha nchi na uongozi kwenye ngazi ya maamuzi ya walio wengi.

Alimuwia kuukomesha wizi,uzembe,ufisadi na mambo mengineyo mengi tena ya hovyo yaliyokuwa yameshamiri huko awali.

Lakini kwa sababu ni ngumu kupigana vita ya mtu mmoja dhidi ya Magenge ya kifisadi.Magufuli hakuruhusiwa kuishi na kuitimiza ndoto yake.

Sasa tumerudi kule kule,tena sasa tukiwa na viongozi wasomi wengi lakini wasioelimika.nasema wasioelimika kwa sababu

"Elimu ni maarifa mengi yanayopatikana na mtu baada ya kusoma mada fulani au kupata masomo ya maisha ambayo hutoa ufahamu wa kitu. Ni mchakato wa kupata maarifa, ustadi, maadili, imani na tabia."

Kwa muktada huo,tulitegemea kuona viongozi tunaowachagua kwenda Bungeni na baadae baadhi yao kuteuliwa na kuwa mawaziri,wanapaswa kumsaidia Mheshimiwa Rais bega kwa bega.

Wanaishia kutembea nchi nzima wakihubiri mgao wa pesa kutoka serikalini.
Baada ya kuwa Rais amekopa au amepewa msaada kutoka taasisi au nchi mbalimbali wanaojiita marafiki wa Tanzania.

Utawasikia "Mheshimiwa" au " Serikali ya Awamu ya Sita"
Nk.

Tayari Imetoa bilioni.
Au "Mama ametoa"

Na bado kuna bilioni ......zinakuja.!

Je! Hiyo ndio dira pekee mliyobakiza vichwani kwa kuwafanya watanzania kuweza kujitambua na kuelimika kutokana na maarifa ya usomi wenu viongozi,ambao wakati mkigombea na kuomba kura huwa mnajinasibu kwa CV's lukuki majukwaani?

Je tutafika Salama kweli?

Cc Pascal Mayalla

Happy Nyerere Day
JamiiForums-1358734221.gif
 
Back
Top Bottom