econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,875
- 21,879
Ni muhimu kuwepo sheria ya uchaguzi ambayo itakataza Rais wa nchi ya Tanzania asiwe Mwenyekiti wa chama chochote Cha siasa wakati anagombea na wakati akiwa madarakani. Hii itasaidia Rais kujiweka asilimia Mia moja kwenye Mambo ya serikali na sio chama. Pia itamsaidia Rais kutokupendelea chama chake na baadala yake kuwaunganisha wananchi.
Kwa Tanzania tunapata shida Sana kulikubali suala la Ushindani wa kisiasa. Kwa Tanzania Ushindani wa kisiasa hakuna kabisa maana chama kimoja kimehodhi mchakato wote wa kisiasa, kwa sababu Rais was nchi ndiye Mwenyekiti wa chama kinachotawala CCM.
Kwa mfano
1. Rais wa nchi ambaye Ni Mwenyekiti wa CCM ndiye mwenye mamlaka ya kuamua Kama vyama vya siasa vifanye mikutano ya hadhara ama la. Kwa Sasa Kuna katazo la vyama vya siasa la kufanya mikutano ya hadhara kwa miaka Saba 7 Sasa.
Yani Mwenyekiti wa CCM anaviamulia vyama vingine visifanye siasa kabisa.
2. Rais wa nchi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM ndiye mwenye mamlaka ya kuamua spika wa bunge aongee Nini na asiongee nini.
Na wabunge walliowengi wanaogopa kwenda kinyume na Mwenyekiti wao wa chama maana wanaweza wasirudi au kufutiwa uanachama. Hivyo bunge kwa kumtii Mwenyekiti wa CCM limekuwa kibogoyo na chombo Cha kusifia hata maamuzi yasiyofaa.
Kwa mfano, Bunge Ni chombo Cha wananchi na sio serikali. Spika wa bunge anapoongea anawakilisha maoni ya wananchi, lakini juzi Happ Spika Ndugai Kama spika alipopishana kauli na Mwenyekiti wake wa chama, ilibidi ajiuzulu.
Hii iliondoa Uhuru na mamlaka ya bunge, na sasa bunge sio mhimili unaojitegemea bali kikao cha kupitishwa mawazo ya Mwenyekiti wa chama na sio matakwa na matarajio ya wananchi.
3. Rais wa nchi ambaye Ni Mwenyekiti wa chama anamteua Mwenyekiti na Viongozi wengine wa Tume ya Uchaguzi. Inakuaje Mwenyekiti wa chama anawateulia vyama vingine mtu wa kuwasimamia uchaguzi mkuu?.
Mwenyekiti huyo huyo baada ya uchaguzi ndio anapewa ripoti ya uchaguzi na ndio anayetoa pesa kwenye Tume ya Uchaguzi. Kwa Hali hiyo unategemea Ushindani wa kisiasa utakuwa wa Haki?
Ni hitimisho kwa kusema kwamba Rais wa nchi asiwe Mwenyekiti au kiongozi wa chama Cha siasa ili ajikite kwenye masuala ya serikali na Wanachi pekee.