Rais aliwaasa viongozi waandamizi kufanya KAZI Kwa kujiamini, DC Sumbawanga kafanya Kwa kujiamini akatumbuliwa. Bado kuna tatizo sehemu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
875
4,101
DC Sumbawanga ametumbuliwa Jana Bila Sababu yakumbuliwa kwake kuwekwa wazi. Mitandao ya kijamii imeandika kwamba zoezi la utayari lililoandaliwa na Askari WA kike ndicho chanzo cha kutumbuliwa kwake.

Wakati vyanzo vikinyetisha kwamba zoezi la utayari Ndilo lililomtumbua naomba tutumie Sababu hii inayoelezwa kwenye mitandao ya kijamii kujiuliza maswali yafuatayo
1. Nani alitoa gari zakufanyia mazoezi ya utayari Kwa Askari wale wa kike?

2. Nani alitoa silaha zakufanyia mazoezi na kisha kwenda kwenye maonyesho?

3. Je, maandalizi haya yalijadiliwa kwenye kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya? Kama yalijadiliwa na yakapitishwa taarifa haikutumwa Kwa mkuu WA mkoa? Kama ilitumwa Kwa mkuu WA mkoa aliwaarifu wajumbe wake wa kamati ya usalama? Kama aliwataarifu, walijulisha mamlaka za juu?

4. Kama hii ndiyo Sababu, vipi vigezo vya utumbuaji? Ametumbuliwa Kwa kuikiuka sheria au kanuni gani?

5. Kwanini barua zakutumbua watendaji zisiandikwe kitaalamu kukata kiu ya wananchi? Zionyeshe kosa, sheria au kanuni iliyokiukwa kumsaidia mtumbuliwa kuelewa kosa lake?

Maswali haya yanalenga kuhoji endapo kauli ya Mhe. Rais kwamba watumishi wajiiamini katika KAZI inatekelezeka? Kama haitekelezeki tatizo lipo Kwa wateulowa au washauri WA mteuaji?

Mamlaka ya uteuzi ikiwa unaweka wazi Sababu za utenguzi itasaidia Sana watumishi WA umma kuelewa kipi Mhe. Rais anapenda na kipi hapendi......nchini Kenya hii tengua tengua hakuna; same to mataifa mengi ya Afrika.. nadhani hii culture aliyoleta JPM inapaswa kutathimiwa upya.
 
Back
Top Bottom