Rais Samia azindua ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo. Asema Serikali imeongeza bajeti ya utafiti kutoka Tsh 7.35bn hadi 11bn

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
320
412
Rais Samia Suluhu Hassan anazindua Ugawaji wa Vitendea kazi kwa Maafisa Ugani nchini ikiwemo Pikipiki 2,000, Vifaa vya Kupima afya ya Udongo (Soil agro scanner) 143, simu janja 384 na visanduku vya ufundi vya Maafisa Ugani 3,400.

#TunaImaninaSamia
#Hakunakinachosimama
#KaziInaendelea.

------
rais samia.jpg

HOTUBA YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN (KWA UFUPI)
Tuliyoyapata mwaka huu ni mafanikio yaliyopatikana baada ya kuweka nguvu katika maeneo mbalimbali kwenye kilimo.

Tumeongeza bajeti ya utafiti kutoka shilingi bilioni 7.35 hadi bilioni 11, nimeyafanya haya kama muumini wa kilimo na nikiamini kitatusaidia kupiga hatua.

Tumefanikisha kufungua masoko ya mazao mbalimbali ikiwemo zao la Parachichi katika nchi za India na Afrika Kusini na hii ni baada ya kukidhi viwango vya ubora.

Mchele wetu sasa unaliwa Ulaya, leo ukienda katika supermarket za Ubelgiji na Ufaransa utaukuta mchele kutoka Tanzania, wameanza kidogo kidogo na wamewezeshwa na benki zetu.

Tumeweza kufanikisha kupatikana kwa ithibati ya ubora yenye viwango vya kimataifa kwa maabara zetu za mimea na viuatilifu.

Kiwanda cha kuchakata tumbaku mjini Morogoro tunakwenda kukifungua, na hii inatokana na uzalishaji wa tumbaku kuongezeka.

Serikali inaendelea kuimarisha huduma za ugani, tunakwenda kugawa pikipiki 6700 leo, na pikipiki 300 tulishagawa hapo kabla na kufanya jumla ya pikipiki tutakazogawa kuwa 7000.

Nimeridhia ombi la maafisa ugani la kumilikishwa moja kwa moja pikipiki watakazopewa baada ya kuzitumia kwa miaka miwili na hii itaenda sambamba na masharti tutakayoyaweka.

Leo tutagawa pia vipima afya ya udongo katika halmshauri 143, tunafahamu kuwa ukiwa na afya njema utazalisha zaidi, hivyo hivyo na kwenye udongo.

Utafiti.jpg

Janga la Uviko-19 limebadilisha mwelekeo wa uchumi duniani na kufanya hata mazao ya biashara na yasiyo ya biashara yote kuwa ni mazao ya biashara.

Niwaombe sana vijana wa Tanzania kuingia katika sekta ya kilimo, hamtajuta. Mtatengeneza fedha nyingi za halali.

Wizara ya Kilimo ihakikishe huduma ya upimaji wa udongo inakua, kwa muda mrefu udongo wetu umetumika kwa muda mrefu sasa ipatikane tiba.

Tuanzishe mifuko ya mzunguko (Revolving Fund) ya pembejeo na maendeleo ya kilimo, pale tunapopata shida katika kupata pembejeo na pembejeo kupanda bei mfuko huu ukashushe bei ili wakulima wetu wasiumie.

Nitoe wito kwa maafisa ugani, vifaa mlivyokabidhiwa ikiwemo pikipiki mvitunze na mkavitumie kwa kazi zilizokusudiwa.

Nawaombeni sana wabunge, tuibebeni sana sekta ya kilimo, kwa kauli moja muipitishe ili yale tuliyoyapanga yaende kutekelezwa.

Tunakoelekea sasa ni kwenye kilimo cha kisasa, kuongeza uzalishaji wa mazao yetu, kufanya kilimo biashara na ndio maana tunajielekeza kujenga maghala na kufungua masoko mapya.

Sekta ya Kilimo imeendelea kuwa muhimili muhimu katika taifa letu na kuchangia maendeleo. Sekta ya Kilimo imetoa ajira kwa asilimia 61 ya watu wote na pia asilimia 65 ya malighafi lakini pia ni sekta inayofanya tujitosheleze kwa chakula.


HOTUBA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA (KWA UFUPI)
Wakati wote Rais anaposimama mbele ya jukwaa na kuwahutubia Watanzania, msisitizo wake ni kuhakikisha tunajikita katika kuboresha uchumi wetu wa ndani na katika sekta mbalimbali, sekta ya kilimo ikiwemo.

Nataka niwape siri, Rais wetu Samia Suluhu alitoa maelekezo kwa Serikali. Na mimi ndiye ninababe maelekezo yote ya serikali na kuhakikisha kuwa wakulima wanalima kilimo chenye ticha ili kiwasaidie Watanzania.


HOTUBA YA WAZIRI BASHE(KWA UFUPI)
Sekta ya kilimo haiwezi kubadilika bila kuchukua mabadiliko kwenye mambo ya msingi, kilimo ni biashara. Sekta hii inachangia wastani wa 25% hadi 27% ya pato la Taifa.

Kwa muda mrefu Mhe. Rais sekta hii imekuwa haikui kwa muda mrefu, biashara ya kilimo katika soko la Afrika inatarajiwa kuwa na dola trilioni moja ikifika mwaka 2030. Sisi kama Tanzania tunatakiwa kunufaika na biashara hii.

Mhe. Rais, tija ina fomula yake. Tija inahitaji mbegu bora, ticha inahitaji viwatilifu. Na leo utafanya zoezi moja, la kugawa pikipiki kwa maafisa ugani 7000 wa nchi nzima kama vitendea kazi.

"Sasa Mhe. Rais, Afisa ugani kwenye pikipiki yake atakuwa na Soil Scanner, atakuwa na uniform maalum ya kumtambulisha kama ilivyo kwa daktari. Na Wizara tutatenga bajeti ya uniform mbili kwa kila afisa ugani kwa mwaka.
Pikipiki.jpg
Mhe. Rais sasa ninakuomba kama ikikupendeza, ninaomba baada ya maafisa ugani kuzitunza na kutumia pikipiki hizi kwa muda wa miaka miwili, basi ziwe za kwao. Hii itakuwa ni motisha kwao.

Lazima tuwe na kanda za kilimo kwenye nchi yetu, haiwezekani korosho inalimwa kuanzia Tandahimba hadi Uvinza. Hailipi, lazima tutengeneze kanda za uzalishaji.

Lakini Mhe. Rais na mimi nataka niseme bila unafiki, kabisa. Nimekuwa mbunge tangu 2015, nimesikiliza hotuba tatu za Marais, wewe ni Rais pekee uliyeipatia nafasi sekta ya kilimo.

Rais, mahitaji ya mafuta ya kula nchini ni wastani wa tani laki sita na nusu kwa mwaka, uzalishaji wetu wa ndani hauzidi laki mbili na arobaini kwa mwaka, tuna tofauti ya karibu laki nne.

Mama nasisitiza, maugani hawa wakiupiga mwingi baada ya miaka miwili pikipiki hizi tuwaachie ziwe mali yao.
 
Leo maafisa ugani (extension officers) wanakabidhiwa Pikipiki, vipima udongo na simu janja (smart phone) ili viwawezeshe kutekeleza majukumu yao.

Hii fani ya maafisa ugani ilipoteza umuhimu kuanzia miaka ya 1980s. Hongera Samia kwa kumfanya Hussein Bashe kuwa Waziri kamili wa kilimo.
 
Too theoretical
Tatizo la wakulima sio maafisa ugani
Tatizo ni masoko, bei za pembejeo

Sumry ana maafisa ugani wake wengi tu lakini kilimo nacho kimemshinda kapunguza sana uzalishaji na anataka kuacha.
Na huyo ni mkulima mkubwa aliyeinvest billions of money
Lakini leo hii Bei ya pembejeo kununua zaidi ya mara 3 ni ajabu na asingeweza.

Ila pole kwa taifa la Tz, viongozi hawajui vipaumbele
 
Too theoretical
Tatizo la wakulima sio maafisa ugani
Tatizo ni masoko, bei za pembejeo

Sumry ana maafisa ugani wake wengi tu lakini kilimo nacho kimemshinda kapunguza sana uzalishaji na anataka kuacha.
Na huyo ni mkulima mkubwa aliyeinvest billions of money
Lakini leo hii Bei ya pembejeo kununua zaidi ya mara 3 ni ajabu na asingeweza.

Ila pole kwa taifa la Tz, viongozi hawajui vipaumbele
Sumry yupi tena?

Si alishafariki?
 
"Kwa sasa idadi ya maafisa ugani tulionao nchini ni 6,704, idadi hii ni ndogo ukilinganisha na mahitaji yetu ya maafisa ugani 20,538 nchini, pamoja na idadi hii ndogo, pia kuna changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi na mafunzo rejea kwa maafisa ugani nchini"

🎤 Waziri Mkenda

#BajetiYaKilimo2021
 
"Nimeridhia ombi la maafisa ugani la kumilikishwa moja kwa moja pikipiki watakazopewa baada ya kuzitumia kwa miaka miwili na hii itaenda sambamba na masharti tutakayoyaweka" Mhe. @SuluhuSamia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

#AlipoMamaVijanaTupo
#Kaziiendelee
Screenshot_20220404-154017.jpg
 
Too theoretical
Tatizo la wakulima sio maafisa ugani
Tatizo ni masoko, bei za pembejeo

Sumry ana maafisa ugani wake wengi tu lakini kilimo nacho kimemshinda kapunguza sana uzalishaji na anataka kuacha.
Na huyo ni mkulima mkubwa aliyeinvest billions of money
Lakini leo hii Bei ya pembejeo kununua zaidi ya mara 3 ni ajabu na asingeweza.

Ila pole kwa taifa la Tz, viongozi hawajui vipaumbele
Pamoja na yooote Mh. Bashe anaonyesha dhamira ya kweli katika kukiendeleza kilimo. Binafsi siamini katika muundo huu wa ugani na wakulima wadogo ambao efficiency yao ni ndogo. Pia mfumo huu wa kilimo ndiyo unaosababisha masoko kutokupatikana kwakua unaleta ushindani usio wa lazima huku kila kaya ikijilisha yenyewe hivyo kuvuruga utaratibu wa soko....

Hata hivyo bado Waziri mwenye dhamana anaonyesha angalau kuijali sekta tofauti na watangulizi wenzake
 
Too theoretical
Tatizo la wakulima sio maafisa ugani
Tatizo ni masoko, bei za pembejeo

Sumry ana maafisa ugani wake wengi tu lakini kilimo nacho kimemshinda kapunguza sana uzalishaji na anataka kuacha.
Na huyo ni mkulima mkubwa aliyeinvest billions of money
Lakini leo hii Bei ya pembejeo kununua zaidi ya mara 3 ni ajabu na asingeweza.

Ila pole kwa taifa la Tz, viongozi hawajui vipaumbele

Mkuu unafikiri kwanini Sumry anataka kuacha kulima..?
Unafikiri kwa mkulima wa level ya sumry naye niwakutafutiwa masoko na serikali?..

Kilimo ni biashara na uwekezaji, binafsi naamini kilimo kufanywa na mtu masikini ni kuendelea kumfanya masikini tu...Kilimo naamini kinahitaji uwekezaji wa kulima kuanzia ekari 10 na kuendelea na sio chini ya hapo...Kulima ekari tano kushuka chini ni kutafuta chakula tu na hela ya kula..

Kilimo bila ya uwekezaji ni sawa na bure tu, masoko yaliyoko huko duniani yanahitaji constant supply ya mazao, ukiweza hili na dunia ikajua kila miezi fulani inaweza kupata say 1000ton lazima wateja waje, na kuzipata ton hizo kwa constant supply unahitaji uwekezaji sio hiki kilimo chetu cha kimasikini..

Mfano, kila siku asubuhi pale London wanahitaji fresh flower na unapaswa kujaza ndege, sasa mkulima wa hivi lazima awe bepari...
Zimbabwe baada ya kunyang'anya mashamba wazungu walishindwa kulima maana walitegemea kulima kwa jembe la mkono wakati wenzao waliwekeza..

Duniani nchi zilizoendelea kilimo kinafanywa na wafanyabiashara wakubwa matajiri sio watu masikini, maana yake ni nini, Kilimo kinahitaji uwekezaji mkubwa ndio tafsiri....

Ni mara chache sana kilimo kinamtajirisha mtu masikini, kilimo kinawezekana tu kufanywa na matajiri...
 
Ninaomba kufahamu, ni kwanini bei ya pembejeo Msumbiji na Malawi iko chini kuliko hapa kwetu?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom