Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Haijalishi awe mkristo au muislam, chamsingi ajali maslahi ya wananchi wake tu.....alaf sipend pipoz zinazo associate vitu nyeti kama iv na iman zao....we nid presnt who iz comited to hs/hr pipo regardless dini yake
 
Mkuu umeandika maneno ya maana sana, lakini unfortunately, hali halisi haiko hivyo!

Labda kama unadhani tumepata marais wa dini za tofauti kila awamu kwa bahati mbaya?

Hilo hatuwezi kulikwepa

It is an unwritten rule! Akija rais muislam awamu ijayo lazima kutakuwa na maneno!

Wafikiri kuna atakaye kuja kubadilisha hilo kama wewe bado una mawazo hayo. Tunapopinga udini hizi ni sehemu muhimu za kuanzisha mabadiliko.

Tunapokubali kuendeleza makosa tunayoyajua hata katika mazungumzo ya kijamii kwa kisingizio cha uhalisia hatuko mbali na wapumbafu. Na kama haya ni mawazo yetu ni bora kuacha malalamiko maana tunataka wenyewe, kama kamari vile ukiliwa unaondoka mdogo mdogo na kujaribu bahati wakati mwingine.
 
Wakati Bakhresa anabuni bidhaa MPYA zitakazocompete world markets sisi tunashindania urais, udini, ukabila. Ni hatari sana.

Kwa nini Rais ajaye asiwe malaika ili kuondoa upendeleo?
 
Ni zamu ya mlutherani sasa maana wao hawajawahi kuwa na rais
Mlutheri ni mkristo, hilo si tatizo kabisa kwenye mfumo wa jamii yetu.

Mbona huwa hulalamiki kuhusu matamko yenye ujumbe mmoja kutoka both lutheran, pentekoste and catholic?
 
Hata Kijana, kuanzia jina ni Christian name, mama ni Christian, Mke ni Christian, watoto ni Christian, na kanisani ataingia!. Uislamu wake ni kwa Baba tuu kama alivyo Baraka Hussein!. He is fit in every aspects!.
Pasco

Pasco,

Siamini kama umefikia mwisho wa kufikiri kwa staili hii. Tunachagua rais mkristo sasa Tanzania? Huu si ndio udini wenye badala ya kuangalia umakini wa rais tunaangalia dini yake. Kwa mitazamo hii siamini kuwa tutaelekea kwema huko mbeleni.

So akitokea Rais Mwislamu ila muadilifu, makini na ana akili timamu na anao uwezo wa kuongoza nchi hatutamchagua kwa sababu tu sio mkristo. Kweli tunasafari ndefu na udini huu hatufiki popote.....:angry:
 
Wakati Bakhresa anabuni bidhaa MPYA zitakazocompete world markets sisi tunashindania urais, udini, ukabila. Ni hatari sana.

Kwa nini Rais ajaye asiwe malaika ili kuondoa upendeleo?
Bakhressa anabuni bidhaa mpya kwa uhuru kwa sababu ya amani tuliyonayo ambayo imedumu kutokana na tamaduni kama hi ninayoizungumzia kwenye mjadala huu!
 
Mkuu rejea bandiko lilopita, nadhani pengine hukunipata pale niliposema kuhusu kutokuyatendea haki "mabadiliko yetu", whether mabaya au mazuri! Mengine yameletwa wakati wa uchaguzi uliopita! Na ndiyo maana nikasema mazuri kwa mabaya!

Mkuu kunawatu ambao wanachukuwa muda kubadilika na wakati na wengine ni fasta!

Nimekuja kugunduwa kuwa mojawapo ya mambo yaliyotuweka pamoja kwa muda mrefu kama taifa lenye mshikamano, basi ni utamaduni huu tuliojiwekea ambao hauko kisheria wala kwenye katiba, bali kwa utashi wetu sisi wenyewe!

Tumekuwa tukijigamba kuhusu amani yetu pasipokujuwa chachu za amani hiyo ni zipi?

Mkuu utakuja kuniambia, sishangazwi na wewe kushindwa namna ya kunisaidia! Isipokuwa nitashangazwa kama utamaduni huu utapuuzwa!


Mushi,

Mbona hukufikiria ni wakati sasa Wazanzibari nao wakatoa Rais wa Tanzania ili kudumisha muungano wetu badala yake unapigia debe rais Mkristo? Hii ni kwasababu Tangu Mkapa na Kikwete ni miaka zaidi ya 20 sasa hatujaongozwa na Rais Mzanzibari (Hata huyo Mwinyi anahisiwa sio Mzanzibari Mzawa bali mzawa wa Mkuranga).
Au unaongozwa na msukumo wa udini nyuma yako?
 
Rais anayekuja lazima awe mzanzibar no discussion. ss bara tumepewa akuna tulichofanya.hasa hasa Husein mwinyi yuko fit .
 
ati ni muhimu tukapata wa imani nyingine... Huu ujinga ndio hua unaniacha hoi kwa watanzania, yani akili ya mtu inaktuma kusema hili kabisa, afu anaanza kujitetea dini si kigezo, si kigezo huku umeshaifanya kua kigezo... Ujinga huu hauishi bongo afu uko kwenye population kubwa zaidi ya 90% n am not kidding kuhusu hilo... Bongo haitobadilika na hizi mentality na wengine wanafata mkumbo...

Take five mkuu.
 
Mushi,

Mbona huufikiria ni wakati sasa Wazanzibari nao waiatowa Rais wa Tanzania ili kudumisha muungano wetu badala yake unapigia debe rais Mkristo? Hii ni kwasababu Tangu Mkapa na Kikwete ni miaka zaidi ya 20 sasa hatujaongozwa na Rais Mzanzibari (Hata huyo Mwinyi anahisiwa sio Mzanzibari Mzawa bali mzawa wa Mkuranga).
Au unaongozwa na msukumo wa udini nyuma yako?
Heshma mbele mkuu! Long time not see you mkubwa!

Mkuu tuko pamoja kabisa! Nashangaa sana wanaoipinga rasimu ya katiba mpya iliyopatikana kutoka kwa wananchi na kuwakilishwa kwenye bunge maalum la katiba na mh jaji Warioba.

Ninaweza kuzungumzia hilo, lakini ni ukweli wa wazi kuwa serikali mbili ni kizungumkuti.

Kabla ya hapo, bado tulikuwa tukielekea upande huo huo ninaouzungumzia hapa(wa kupokezana)

Kumbuka Mwinyi alipokuwa akizungumziwa kuwa ni jiwe moja kuuwa ndege wawili? Kwamba alikuwa muislam na kwa asili katokea Zanzibar?

Hadi usawa huu, hatuna utaratibu tena wa kupokezana madaraka kati ya nchi ya Zanzibar na Ile ya Tanganyika! Ndo maana baada ya Mwinyi, hakujawa na rais mwananchi wa Zanzibar aliyetokea kuwa rais wa muungano! Maana kwanza Zanzibar hawana shida kubwa kuhusiana na maamuzi wanayotaka kufanya kama nchi...Wana hadi wimbo wa wa Taifa nk.

Ni vyema tukaweza kutofautisha mambo ya muungano na hili ninalolizungumzia hapa,, ambapo wengi wetu wanaongozwa na hisia pamoja na nidhamu ya woga wa mazoea, wakidhani kuwa amani tuliyonayo ipo kwa bahati mbaya tu!?

Hilo la kipimo ama kikomo cha uongozi, ni Issue ya kikatiba kama ilivyo ile ya muungano.

Sasa umekubali kuhusiana na hayo ya kina Mwinyi, hayo yalikuwa ya kikatiba lakini bado unalalamika kuwa hakuwa mzanzibari, kesho utaacha kulalamika kwanini hakuwa muislam? Sasa hapo nani atakuwa mdini?

Twende taratibu mkuu...Ushaanza kulalamika Mwinyi hakuwa mzanzibari.Unadhani ungeacha kulalamika endapo asingekuwa muislam!?

Unafiki unatusumbuwa watanzania! Tusijadili kwa hisia, tutulizane tutumie fahamu zetu ipasavyo bila bias!
 
nimeamini kuna watanzania wapumbavu, yaani baadhi ya comment ni za kidini halafu watu bila haya wanalike. kuna haja ya kuwa na mkono wa chuma ili watu namna hii wasiishi juu ya uso wa Tanzania.
 
Jmushi, naunga mkono hoja kwa asilimia fulani, huu ndio ukweli ambao watu wanaujua lakini wanogopa kuusema. Na kuwajuza zaidi si mkristo tu lakini ni lazima awe mkatoliki, nasisitiza "MKATOLIKI" hapa ndio utakumbuka vita ya Mrema(mlutheri) na Mkapa(mkatoliki).

2015 mamvi(mlutheri) hana nafasi na CCM wakimsimamisha mkrito mkatoliki ndio utakuwa mwisho wa Chadema na Dk Slaa(mkatoliki) atapotea kiana kumsafishia njia mgombea mkatoliki wa CCM.
Wekeni maneno haya katika kumbukumbu zetu.

Mkuu zamu ya wazazbar ili kudumusha muungano mkuu
 
Mm nasema hiv rais zamu sasa ya Zanzibar
sawa tu, kwani zenji hakuna wakristo? Au mmeshauwa wote?

Kama wapo, tunapata katiba mpya ya wananchi, tunampata rais aliyetokea Zanzibar ambaye ni mkristo.Taifa linasonga mbele!
 
Back
Top Bottom