Rais ajaye baada ya Magufuli atalipa madeni mengi sana

Wangembembelezabembeleza hadi leo huo mradi wa barabara ungekuwa unasubiri zuio la mahakama.
Duh!
Tutamlipaga tu barabara zitakapoanza kujenerate mifweza ya kutosha.
Uwekezaji wowote unaopuuza mali na haki ya mtu mmoja mmoja siyo maendeleo. Maendeleo yoyote lazima yamlenge binadamu na siyo kumrudisha nyuma.

Usifurahie kuona mwenzio alivunjiwa nyumba wakati kuna zuio la mahakama, jiulize ingekuwaje kama ingekuwa ni nyumba yako!!
 
Siyo kila mtu ana uwezo wa kuchambua masuala ya kitaalamu yahusuyo uchumi, biashara na uwekezaji. Subiri zitakapo buma ndiyo utaikumbuka thread hii
Haibumi kamanda labda tukosee kuchagua tuwarudishe wapiga madili tena.
 
Hatakuwa na kazi kwa sababu atauzi mandege yote na kwenda kulipa madeni. Kwa sababu raisi ajaye madege sio kipaumbele chake
 
Kuna mtu kule Mpanda alishinda kesi ya ardhi dhidi ya wananchi waliovamia shamba lake lakini amri ilitolewa na JPM kuwa wananchi waachwe. Naamini anatunza nyaraka zake na wale wananchi wajiandaye kisaikolojia. Huyu naye atalipwa fedha kibao hapo mbeleni
Kwani sheria ya ardhi inasemaje? mkuu nahitaji ufafanuzi iliusaidie na wengine hapa waliochukulwa ardhi kwa mtindo huo
 
Haibumi kamanda labda tukosee kuchagua tuwarudishe wapiga madili tena.
Kupiga dili ? Mbona hamna mtu anamzidi Jiwe kupiga dili!! Miaka 4 katengeneza Tsh 2.4 Trilion kupitia Uwanja wa Chato, Boeing na Stigler!!
Msijifanye hamumjui mtu aliyekubuhu kupiga dili wakati inajulikana Jiwe akiwa Waziri katengeneza fedha kupitia Kivuko cha Bagamoyo na Nyumba za Serikali.
 
Kupiga dili ? Mbona hamna mtu anamzidi Jiwe kupiga dili!! Miaka 4 katengeneza Tsh 2.4 Trilion kupitia Uwanja wa Chato, Boeing na Stigler!!
Msijifanye hamumjui mtu aliyekubuhu kupiga dili wakati inajulikana Jiwe akiwa Waziri katengeneza fedha kupitia Kivuko cha Bagamoyo na Nyumba za Serikali.

Mwache apige kwani yeye sio Mtanzania? Na wewe kama unaweza nenda kapige!
 
DENI LA TAIFA HALILIPIKI
Hakuna rais wa nchi yoyote anayeumiza kichwa kuhusu kumaliza au kupunguza deni la taifa. Cha kufanya ni kuhakikisha unaendelea kukopesheka
 
Ufanuzi gani? Kwani lazima utosheleze?Sheria siyo hoja kwani inategemea dhamira ya huyo anayetunga kama ni ovu au njema. Sheria nyingi zilizotungwa katika miaka 3-4 iliyopita zina dhamira mbovu. Baadhi ya sheria hizo zenye nia ovu zimesharekebishwa kwa shinikizo ya Benki ya Dunia! Wabunge wetu wamepiga kelele lakini hazikusaidia. Makaburu wa Afrika Kusini walikuwa na sheria ya kuhalalisha ubaguzi wa rangi na kuwanyima Waafrika walio wengi haki za kidemokrasia. Sheria unayozungumzia imetungwa 2019 wakati utaratibu huu wa watu kununua uhuru wao ulianza mara tu baada ya uchaguzi. Suala hili lilitinga bungeni mwaka huu ambapo serikali ilihojiwa kuhusu sheria inayotumika kufanya hivyo. Kama kawaida utratibu ukatetewa kwa hoja za nguvu lakini baada ya hapo haraka haraka sheria ikatungwa.

Kwa hiyo wewe kasuku huku JF ndio una akili nyingi kuliko wabunge wote pale Idodomia. JF kuna kazi kweli kweli, chacha njomba vipi wewe mwerevu unashinda na njaa huku JF? Maana huandiki bure humu JF kuna kitu ambacho unahitaji kibadilike au umekerekwa nacho ambacho kinafanywa na Serikali, kulikoni?
 
Back
Top Bottom