Rais ajaye baada ya Magufuli atalipa madeni mengi sana

Rais ajaye baada ya Magufuli atalipa madeni mengi sana

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
18,878
Reaction score
29,403
Kuna maamuzi mengi yanayofanywa kwa ubabe na Serikali ya Awamu ya 5 ambayo yanakiuka sheria sana. Yana athari kubwa sana kwa wananchi wanao tendewa. Rais ajaye baada ya JPM ajiandae kutumia makusanyo ya TRA kulipia madeni yafuatayo;

1. Deni la la Taifa linapanda kila kukicha kwa kuwa miradi mingi kama SGR na STIGLERS. Miradi hii itakuwa itakamilika kati ya 2023 na 2025, hivyo repayment period itakuwa ndiyo inaanza. Kwa hiyo Asilimia kubwa ya makusanyo ya TRA itaelekezwa kulipa deni

2. Fidia kwa waliobomolewa Ubungo-Kibamba huku wakiwa na zuio la Mahakama. Kwa wakati huu Mahakama ziko mfukoni mwa JPM ndiyo maana Serikali haijatoa fidia na imekaidi zuio la Mahakama. Itakapo kuja Serikali inayo jali haki za binadamu, wale wote wenye nyaraka zao sahihi za Kimahakama au hati za umiliki watafidiwa tu. Hata kama watakuwa wamefariki, warithi wao watapata haki zao.

3. Mafisadi wa kutakatisha fedha feki. Watu wengi amewatupa rumande kwa kudai kuwa ni mafisadi na wametakatisha fedha lakini miaka 3 kesi haziendelei kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea. Ukiacha hawa walioingia plea bargain na wakatoka, wale waliobaki watadai fidia tu na watapata.

4. Wafanya biashara ambao wananyang'anywa mali zao kwa sababu ya chuki binafsi tu.

Ushauri wangu kwa Wa Tanzania ni kwamba watunze rekodi tu, hii hali ya dhuluma haiwezi kuwa ya kudumu. Ipo siku utakuja utawala unaojali utawala wa sheria utawafidia
 
baada ya Magufuli ,Rais ajaye hakika atafanya kazi rahisi sana. atafanikiwa kulipa madeni yote katika deni LA taifa kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

hao unaosema watatoka, watatokaje kama ni sheria ya uhujumu uchumi ndio imewatia hapo mahabusu? usijidanganye juu hilo jambo hata kidogo na watatoka kama sheria itasema vinginevyo juu yao.

chuki ipi kwa wafanyabiashara unayoizungumzia? Leo serikali kukusanya inachostahili kwa wafanyabiashara limekuwa kosa? wengi sana wamefurahi kuona serikali iko makini kukusanya kodi hasa kwa hao wafanyabiashara
 
Kuna mtu kule Mpanda alishinda kesi ya ardhi dhidi ya wananchi waliovamia shamba lake lakini amri ilitolewa na JPM kuwa wananchi waachwe. Naamini anatunza nyaraka zake na wale wananchi wajiandaye kisaikolojia. Huyu naye atalipwa fedha kibao hapo mbeleni
 
i
Kuna mtu kule Mpanda alishinda kesi ya ardhi dhidi ya wananchi waliovamia shamba lake lakini amri ilitolewa na JPM kuwa wananchi waachwe. Naamini anatunza nyaraka zake na wale wananchi wajiandaye kisaikolojia. Huyu naye atalipwa fedha kibao hapo mbeleni
takuwa kama meli ya samaki na kile kituo cha mafuta mwanza
 
Hizo pesa za magendo na utakatishaji zilikuwa kinyume cha sheria

Nitajie Nchi yeyote ile ambayo inamaduka holela ya kubadilisha pesa kama ilivyokuwa Tanzania

Tatizo hujui
Wamiliki wa maduka ya kubadili pesa za kigeni wamedhulumiwa pesa zao nyingi wanalia moyoni wametunza kumbukumbu wanasubiria mda tu kuanzisha madai yao.
 
Wazo mujarabu kabisa, babangu alibomolewa nyumba ya ghorofa kimara akiwa na zuio la mahakama mkononi,
awamu ya 5 imejaa dhuluma.
Kuna watu walidhulumiwa Awamu ya 1 wakati wa zoezi la wahujumu uchumi lililo endeshwa na Edward Sokoine mwaka 1982 kama yule Karasinga wa Bukoba kwa jina Kugis.

Walifungua kesi wakaja kushinda na kufidiwa wakati wa AH Mwinyi. Sasa hivi watoto wa Mzee Kugis ndiyo ma transporter wakubwa wa mkoa wa Kagera kwa jina la Kugis Transport.

Tunza document, haki haipotei bali hucheleweshwa tu
 
Kama ambavyo na yeye anatakiwa alipe madeni ya yule mkulima anaeidai serikali tangu 80s. Chuki ni kitu kibaya sana. Mwinyi kalipa madeni,Mkapa kalipa madeni hadi yakafutwa,Jk kalipa madeni,JPM analipa madeni. Sasa kibaya au cha ajabu nini Rais ajaye akilipa madeni?
 
Si mbaya kama kazi yake itakuwa hiyo maana miundombinu itakuwa tayari kila kona, tatizo alipe madeni wakati huo bado anajenga miundo mbinu hiyohiyo iliyokopewaa.
 
Back
Top Bottom