Rais ajaye akerwe na udini kwa vitendo

Rais ajaye akerwe na udini kwa vitendo

Ushauri kwenu nyie wa hiyo dini
1) kuwekeza kwenye elimu ya mtoto wako sio lazima uwe umeajiriwa na kulipwa posho za semina kama ulivyosema hapo juu. Sasa ivi watu wengi wanajishughulisha na biashara pamoja na kilimo ambazo zinawaingizia pesa nyingi tu. So kuwekeza kwenye elimu ni wewe mwenyewe tu

2) Zanzibar mpo karibu 99% ya watu wote wanaoishi huko na hivyo dini hiyo ndio waliojaa kwenye hizo ofisi huko zanzbar, sasa kwa nn msiwe mfano huko zenj kwa kuwekeza kwenye elimu ikiwa nyie mpo wengi sana kwenye ajira huko?? Hebu tueleze hadi sasa mna vyuo vikuu vingapi na bora?..
Suala la dini ni gumu sana,sijui ni bahati mbaya au ni mpango, dini fulani kubwa watumishi katika ofisi za umma ni wa kutafuta na tochi.

Nipo kwenye idara yenye watumishi 27 lakini afisa muislam nipo peke yangu! Kusema ukweli kwa kadri ninavofahamu sijawahi kuona kubaguliwa kwasababu ya dini yangu.

Suala la semina na vikao (baadhi) kufunguliwa kwa sala na kufungwa kwa sala tena ya dini fulani nimekutana nalo mara kadhaa, nadhani suala hili lipigwe marufuku, Semina na warsha zifunguliwe kwa wimbo wa taifa ambao pia ni dua ndani yake, yaani MUNGU ibariki Afrika....
 
Kanuni za uteuzi na ajira lazima zipitiwe upya ili ziruhusu watu wa dini zote watauliwe na kuajiriwa kwa uwiano hasa baada ya vigezo muhimu vya elimu na uzoefu wa kazi husika kuzingatiwa.

Inahuzunisha kukuta wafanyakazi wote wa ofisi ya umma au taasisi ya umma Ni wa dini fulani tu. Inasikitisha unakwenda kwenye semina au workshop au mkutano na kukuta washiriki wengi Kama sio wote ni wa dini fulani tu. Hivyo kusababisha vikao kufunguliwa na kufungwa kwa maombi ya dini fulani tu...
Kama dini zinawafarakanisha , hazina umuhimu wa kuendelea kuwepo.
 
Isiishie huko tu Hadi kwenye shughuli binafsi unakuta ni wadini fulani tu ndio wameajiriwa, hili lipo sana. Hapa mamlaka za ajira na mifuko ya Jamii ziliangalie hili maana hata wao wanawajua kupitia list za majina wanayokata michango ya wafanyakazi hii itasaidia kuleta balance.
Nyie wa Dini fulani fulani somesheni watpoto wenu waende mpaka vyuo vikuu sio kuwalazimisha masomo ya hizo dini zenu harafu mnakuja kulalamika. Serikali haiongozwi kwa elimu za dini, sasa mkiwajaza elimu dini msubiri kuwapa kazi na vyeo huko huko kwenye dini zenu.
 
Ndugu zetu hawawezi kuwa sawa na sisi. Tatizo lao kubwa, wanawafundisha zaidi vijana wao Elimu Ahera zaidi ya Elimu Dunia. Si Jambo baya, lakin wanakosa ujuzi kutokana na kuwa na Elimu ndogo. Nakubali kuwa, wengi wao waliobahatika kutoboa, wako vizuri kichwani and their good leaders japo itikadi huwa zinawazidi.

Chukulia mfano, Kati ya wanafunzi mia mbili wa Udaktari wanaodahiliwa kila Mwaka na Chuo Kama Muhimbili, Hawa ndugu zetu huwa hawazidi ishirini...

Umesema vizuri. Huo ndiyo ukweli. Madrasa yamewafikisha hapo. Hawana sifa kutaaluma za kuajiriwa.
 
Nyie wa Dini fulani fulani somesheni watpoto wenu waende mpaka vyuo vikuu sio kuwalazimisha masomo ya hizo dini zenu harafu mnakuja kulalamika. Serikali haiongozwi kwa elimu za dini, sasa mkiwajaza elimu dini msubiri kuwapa kazi na vyeo huko huko kwenye dini zenu.

Ukweli mtupu. Debe tupu haliachi kutika.
 
Suala la dini ni gumu sana,sijui ni bahati mbaya au ni mpango, dini fulani kubwa watumishi katika ofisi za umma ni wa kutafuta na tochi. Nipo kwenye idara yenye watumishi 27 lakini afisa muislam nipo peke yangu! Kusema ukweli kwa kadri ninavofahamu sijawahi kuona kubaguliwa kwasababu ya dini yangu. Suala la semina na vikao (baadhi) kufunguliwa kwa sala na kufungwa kwa sala tena ya dini fulani nimekutana nalo mara kadhaa, nadhani suala hili lipigwe marufuku, Semina na warsha zifunguliwe kwa wimbo wa taifa ambao pia ni dua ndani yake, yaani MUNGU ibariki Afrika....
Mara nyingi mtu watu wanashindwa kugundua chanzo cha tatizo. Embu somesheni watoto wenu ili katika maombi ya kazi wawe wengi na wenye uwezo unaotakiwa
 
Mara nyingi mtu watu wanashindwa kugundua chanzo cha tatizo. Embu somesheni watoto wenu ili katika maombi ya kazi wawe wengi na wenye uwezo unaotakiwa
Mkuu nakubali kabisa suala la kusomesha watoto, lkn itachukua karne kwasababu kuna vicious cycle ambayo ishajitengeneza. Binafsi sijui imetengenezwa au imejitengeneza yenyewe, lkn kama nilivyoeleza, katika utumishi wangu sijawahi kuona nimebaguliwa kwa ajili ya dini yangu so I don't know if it's planned or not.

Ila ninachokifahamu ni kuwa watu wa dini fulani ni wachache sana kwenye utumishi wa umma hasa kwa taasisi ninayofanyia kazi, ofcourse hatuwezi kuwa sawasawa lkn angalau kuwa na uwiano unaokaribiana.

Waislamu pia tunapaswa kubadilika, tuishike dini lkn pia tusiache kufanya juhudi katika elimu, wengi tumeshindwa kubalance elimu ya dini na elimu ya kawaida.
 
  • Thanks
Reactions: mij
Mara nyingi mtu watu wanashindwa kugundua chanzo cha tatizo. Embu somesheni watoto wenu ili katika maombi ya kazi wawe wengi na wenye uwezo unaotakiwa

Hiyo propaganda unayoisema leo ndo ilikuwa excuse ya kuwaweka waislamu pembeni kwenye ajira katika miaka ya 1970.

Hiyo propaganda imeshachuja kwa sababu waislamu waliosoma ni wengi mno lakini bado wanabaguliwa kwenye utumishi wa umma na teuzi za serikali!
 
Siku itakaporuhusiwa kuulizwa wewe dini gani kwenye kura ndio siku tatizo litaisha, na katika haya makundi mawili asietaka hili basi anajua jibu fika kama yeye ni minority. Inashangaza kwa nini dini zipo na zinatambulika ila kujua idadi kundi moja halitaki kabisa kusikia hii habari.
Mbona sensa ya mwaka 2012 Kikwete akiwa Rais alikataa hili, je Waislam ndio minority?
 
Tatizo la waislam hawajiamini wanapokuwa madarakani, wenzao wakikamata vitengo, wanakamua ile kinomanoma.
WATCH AND LEARN nyie wazee wa baragashia!
 
Hata ukienda vyuo vingi Kama UD, Mzumbe, SUA n.k ukifanya observation utagundua hawako wengi
Asilimia kubwa ya matumizi ya serikali Ni mishahara, hii ina maana asilimia kubwa ya matumizi ya Kodi za watanzania inakwenda kwenye kundi la jamii lililopewa ajira. Umakini unahitajika Sana kwenye ajira na uteuzi wa watumishi kwenye nafasi mbalimbali.
 
Huoni kwamba hiyo ni dosari mkuu? Observation yako ianzie kwenye Primary schools and Secondary Schools O level hasa za umma ambapo idadi ya wanafunzi inakaribiana. Kadri unavyokwenda kwenye elimu ya juu ndio kundi moja la kijamii linavyozidi kupukutika na kuachwa nyuma! Hivi serikali haioni haja ya kufanya utafiti juu ya jambo hili?
Huko primary kwakuwa Ni bure hakuna malipo utakuta uwiano unakaribiana, ukienda secondary makundi yanaaza kujitokeza ghafla kutokana na purchasing power ya wazazi.

Wenye ajira, na wanaoweza kukopa kwenye vyombo vya fedha wanamudu kugharamia ada za watoto wao kwenye shule bora na hata gharama za kusomesha mtoto kwenye shule za kawaida Kama vile nauli, vitabu, chakula, mavazi na tuition.

Watoto wa wakulima na wachoma vitumbua inawawia vigumu kugharamia watoto wao hata kwenye shule za kata. Maana hata soko la mazao yao halieweki na likieleweka hali ya hewa haieleweki. Humohumo Kuna stakabadhi gharani ambayo hawajui mnunuzi ataleta hela lini.
 
Kama mtu kaupalilia ukabila na ukanda udini ndio atauona???
 
Sasa mchawi upo hapo kwenye elimu kuanzia Msingi hadi Elimu ya Juu. Katika matokeo ya ngazi ya std VII na kidato cha 4 kwa miaka mitano niliyofuatilia(2014-2019; mikoa inayoongoza mara nyingi ni Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Iringa, Njombe, Kagera, Shinyanga, Dar es Salaam na mzunguko huo huendelea.

Mikoa inayofanya vibaya ni Tanga, Mtwara, Lindi, Unguja, Pemba na Mzunguko huendelea. Sasa kwa pattern na trend hiyo inayotokea kwenye drawing board, kwenye msingi kabisa, unadhani elimu ya juu na kwenye ajira, ni nani watakuwa wengi?
Mkulima na muoka mandazi atamfundisha mwanawe kulima na kuoka mandazi, mwajiriwa atamfundisha mwanawe kufanya nini? cycle irajirudia tu. Ndiyo maana mwl Nyerere aliliona hilo na akaamua kuzitaifisha baadhi ya shule za kidini ili watoto wote wasome angalau kupunguzi pengo lililoachwa na wakoloni.

Mwl Nyerere alifanya juhudi za makusudi za kuwajumuisha akina Kawawa na waislamu wengine kwenye uongozi. Ndiyo maana Leo hii unaweza kuwaona watoto na wajukuu wa akina Rashid Kawawa na makamba kwenye ramani
 
Sasa Mzee ili ujue mtu yupo under selected ama la lazima uangalie na proportion yake kwenye population kwanza

Maana Kama Kati ya watu million moja mpo laki moja huwezi kutegemea kwenye selection muwe 50/50
Ndio maana nikatolea huo mfano wa Zanzibar wao wapo wengi na Wakristo wachache so haishangazi Waislam wakawa wengi Serikalini kuliko Wakristo
Kwani wasukuma na wachaga Nani Ni wengi kwenye jamii ya Tanzania? Kwenye ajira pia kuko hivyo? au wanaitana hata kwa kazi za kufagia ofisi na kufyeka majani wizarani?
 
Kwani wasukuma na wachaga Nani Ni wengi kwenye jamii ya Tanzania? Kwenye ajira pia kuko hivyo? au wanaitana hata kwa kazi za kufagia ofisi na kufyeka majani wizarani?
Population sio lazima the whole population. Na hatuwezi kuwa tabia zinazofanana au akili zinazofanana za kuona fursa.
 
Back
Top Bottom