Rais ajaye akerwe na udini kwa vitendo

Rais ajaye akerwe na udini kwa vitendo

Kanuni za uteuzi na ajira lazima zipitiwe upya ili ziruhusu watu wa dini zote watauliwe na kuajiriwa kwa uwiano hasa baada ya vigezo muhimu vya elimu na uzoefu wa kazi husika kuzingatiwa.

Inahuzunisha kukuta wafanyakazi wote wa ofisi ya umma au taasisi ya umma Ni wa dini fulani tu. Inasikitisha unakwenda kwenye semina au workshop au mkutano na kukuta washiriki wengi Kama sio wote ni wa dini fulani tu. Hivyo kusababisha vikao kufunguliwa na kufungwa kwa maombi ya dini fulani tu...
Naona wewe unakosea, Iwe hivi:
- Maduka yawe kwa uwiano
- Shule kwa uwiano
- Bar kwa uwiano
- Butcha kwa uwiano
- Magenge kwa uwiano
- Wateja kwa uwiano
- Kuoa kwa uwiano
 
Naona wewe unakosea,
Iwe hivi
Maduka yawe kwa uwiano
Shule kwa uwiano
Bar kwa uwiano..
Mmmh!! Umefika mbali, maada Ni kuhusu ajira ambako walioajiriwa Wana chanzo Cha Mapato kisichotetereka kinachotokana na Kodi za walipa Kodi wote nchini. Mtu mwenye ajira ana uhakika wa kipato na uhakika wa kupata mikopo.

Mtu mwenye kipato kisichotegemea hali ya hewa ana uhakika wa kusomesha wanawe, kuwekeza, na kulipia michango mbalimbali. Mada hii inamtaka rais ajae aone Kama watu wenye sifa ya kuajiriwa waajiriwe waajiriwe kwenye nafasi kwa kuzingatia nchi inayo madhehebu mbalimbali Na wanaoitwa kwenye workshops na uteuzi wazingatie hilo pia. Maana ajira Ni ufunguo muhimu sana wa Mambo mengine muhimu kwenye familia ya mwajiriwa. Sasa unachosema hapo uko nje ya mada.
 
Kanuni za uteuzi na ajira lazima zipitiwe upya ili ziruhusu watu wa dini zote watauliwe na kuajiriwa kwa uwiano hasa baada ya vigezo muhimu vya elimu na uzoefu wa kazi husika kuzingatiwa.

Inahuzunisha kukuta wafanyakazi wote wa ofisi ya umma au taasisi ya umma Ni wa dini fulani tu. Inasikitisha unakwenda kwenye semina au workshop au mkutano na kukuta washiriki wengi Kama sio wote ni wa dini fulani tu. Hivyo kusababisha vikao kufunguliwa na kufungwa kwa maombi ya dini fulani tu...
Umeongea kwa staha na tahadhari kubwa sana mkuu. Bahati mbaya hautasikika. Watakaokusikia watakuita wewe ndio mdini na hilo unalotaka lifanyike halitaweza kutekelezwa

Aliwahi kusema Mwl. Nyerere kua Watanzania wengi wanangozi nyembamba sana kuhusiana na suala la dini. Ukiwachuna kidoogo tu watajitokeza kwa misimamo ya dini zao.

Uwiano unaouzungumzia wa kutokua sawa kama ungekua unaathiri dini fulani(jina lapuni) miongoni mwa hizo unazozizungumzia basi kelele zake zingesikika dunia nzima. Kwa mfano katika siku za mwanzo za utawala wa awamu hii kuna baadhi ya watu walikua wanadai teuzi nyingi zina harufu ya ukabila na udini. Ajabu ni kwamba ukabila wakawa wanafafanua kwamba ni kabila lipi linanufaika na awamu hii ya uongozi, lakini udini wakaucha hivyohivyo bila kufafanua, na sasa hawesemi tena bali wakati huu wanalaumu kua kuna upendeleo wa ukabila tu!!!

Wakati wa awamu ya nne kulikua na kelele kuhusu shirika moja la hifadhi ya jamii kwamba ajira zake zina harufu ya udini. Zle kelele zilikua kuubwa sana japo hata ingefanyika sensa bado wale wenye imani isiyokua na uvumilivu na yenyewangekua wengi kuliko wanolalamikiwa!!

Nakumbuka wakati wa awamu ya Tatu iliteuliwa bodi ya misamaha ya wafungwa "Parole Board" ambayo sio tu iliundwa na watu wa dini moja bali katika wale wajumbe 11 wa ile bodi iliyoteuliwa na aliyekua Waziri Mkuu, watatu kati yao walichaguliwa kwa sifa yao (qulification) kua ni viongozi wa hiyo dini fulani!!! Waziri Mkuu wa wakati huo akadai kua serikali inafanya teuzi kwa merits za watu!! Rais wa awamu ya Tatu aliingilia kati na kuivunja ile bodi na kusema lazima teuzi za uma zionyeshe sura za utengamano wa kitaifa wenye kuzingatia uwakilishi wa makundi na imani tofauti kwenye jamii

Hilo ni suala nyeti sana na nadhani kama sio uvumilivu wa watu wa imani moja katika zinazovutana(maana huwa wanakejeliwa kua hawapendi maendeleo) basi umoja wa kitaifa ungekua shakani
 
Sikuwa na maana ya dini moja tu ndiyo inayoonewa, lakini mtu yeyote atakayeibagua dini nyingine kwenye ajira, semina na uteuzi hafai bila kujali anaikandamiza dini gani. Tunachosema ss pale ofisini au kwenye semina kuwe na mchanganyiko wa kiwiano, kuitana kwa kuzingatia dini, kabila au Kanda fulani.

Maana unapoijaza mapesa jamii moja na kuichacha jamii nyingine kwa bahati mbaya au kwa makusudi inasababisha kuipatia ufunguo wa maendeleo jamii moja na kuinyanganya ile nyingine.

Mfano, Kuna wakati taifa bila kujuwa lilikuwa linatumia pesa nyingi sana kulisimesha kabila moja kitu kilichosababisha kuwa na waajiriwa wengi sana kutoka kabila hilo na kabila hilo likatumia pesa hizo za ajira kuwekeza kwenye elimu za watoto wao, kila sehemu utawakuta wapo
 
Kanuni za uteuzi na ajira lazima zipitiwe upya ili ziruhusu watu wa dini zote watauliwe na kuajiriwa kwa uwiano hasa baada ya vigezo muhimu vya elimu na uzoefu wa kazi husika kuzingatiwa.

Inahuzunisha kukuta wafanyakazi wote wa ofisi ya umma au taasisi ya umma Ni wa dini fulani tu. Inasikitisha unakwenda kwenye semina au workshop au mkutano na kukuta washiriki wengi Kama sio wote ni wa dini fulani tu. Hivyo kusababisha vikao kufunguliwa na kufungwa kwa maombi ya dini fulani tu...
Tusipombadilisha aliyepo waislamu wataendelea kuachwa.
 
Ushauri kwenu nyie wa hiyo dini
1) kuwekeza kwenye elimu ya mtoto wako sio lazima uwe umeajiriwa na kulipwa posho za semina kama ulivyosema hapo juu. Sasa ivi watu wengi wanajishughulisha na biashara pamoja na kilimo ambazo zinawaingizia pesa nyingi tu. So kuwekeza kwenye elimu ni wewe mwenyewe tu

2) Zanzibar mpo karibu 99% ya watu wote wanaoishi huko na hivyo dini hiyo ndio waliojaa kwenye hizo ofisi huko zanzbar, sasa kwa nn msiwe mfano huko zenj kwa kuwekeza kwenye elimu ikiwa nyie mpo wengi sana kwenye ajira huko?? Hebu tueleze hadi sasa mna vyuo vikuu vingapi na bora?...
Nikitoka tu job napitia Mandela road naingia mitaa ya river side napiga safari mbili baridiiii na kitimoto safi na kachumbali. Jana nimelipia wanangu ada
 
Kanuni za uteuzi na ajira lazima zipitiwe upya ili ziruhusu watu wa dini zote watauliwe na kuajiriwa kwa uwiano hasa baada ya vigezo muhimu vya elimu na uzoefu wa kazi husika kuzingatiwa.

Inahuzunisha kukuta wafanyakazi wote wa ofisi ya umma au taasisi ya umma Ni wa dini fulani tu. Inasikitisha unakwenda kwenye semina au workshop au mkutano na kukuta washiriki wengi Kama sio wote ni wa dini fulani tu. Hivyo kusababisha vikao kufunguliwa na kufungwa kwa maombi ya dini fulani tu...
wewe wanena kwa mafumbo, sema tu Rais ajae aweke mfumo wa uwiano sawa kwenye ajira na elimu kati ya wakristo , waislam na wapagani unazunguuuuka! unaogopa kutaja dini na utamaduni wa kijinga wa wabongo kuficha ficha mambo wakati baba yetu kashafungua njia akimtumbua mlevi anasema huyu mlevi akimtumbua anaejidai boss sana anasema, wewe umekwama wapi mkuu?
 
Kwenye kutumbuliwa umekosea sana, magu anatumbua kama huendi nae sawa yaani anavyotaka yeye hata kama kakosea yeye. Nakutolea mfano wa wa dini nyingine aliowatumbua,
- Prof. Godius Kahyarara - alikuwa mkurugenzi mkuu NSSF
- Modestus Kipilimba - alikuwa mkurugenzi mkuu TISS
- Felchism Mramba - alikuwa mkurugenzi mkuu Tanesco
- Joseph Masikitiko - alikuwa mkurugenzi mkuu TBS
- Prof Sospeter muhongo - alikuwa waziri wa nishati na madini
- Ernest Mangu - alikuwa IGP
- Dickson maimu - alikuwa mkurugenzi mkuu NIDA
- Dr. Irene Isaka - alikuwa mkurugenzi mkuu SSRA
- Sam Kamanga - alikuwa mkurugenzi mkuu shirika la bima
Hao ni baadhi tu ya watu waliokuwa kwenye taasisi kubwa za serikali na wapo kwenye hiyo dini nyingine lakini magu aliwatumbua.
So suala la kutumbuliwa wala sio dini
Unaongea kujifurahisha alafu ukale kitimoto, jiulize enzi hizo kwanini ulibadilishwa mfumo wa mitihani kutoka jina kwenda kwenye namba? Jiulize ile tume iliyoundwa na jk kipindi kile kupima ufaulu wa wanafunzi katika dini ya kiisalm walikuja na majibu gani?

Na ndio silaha yenu eti waislam hawajasoma ndio maana hawateuliwi, hakuna uthibitisho juu ya hili angalia msomi kama prof assad alivyovuliwa cheo chake unadhani kisa nini? Kumbuka Ramadhani dau alikuwa anashambuliwa nini?
 
Ndugu zetu hawawezi kuwa sawa na sisi. Tatizo lao kubwa, wanawafundisha zaidi vijana wao Elimu Ahera zaidi ya Elimu Dunia. Si Jambo baya, lakin wanakosa ujuzi kutokana na kuwa na Elimu ndogo. Nakubali kuwa, wengi wao waliobahatika kutoboa, wako vizuri kichwani and their good leaders japo itikadi huwa zinawazidi.

Chukulia mfano, Kati ya wanafunzi mia mbili wa Udaktari wanaodahiliwa kila Mwaka na Chuo Kama Muhimbili, Hawa ndugu zetu huwa hawazidi ishirini...
vicious cycle
 
Hii hoja haina msingi wowote.

Hivi kama unavyosema ndivyo ilivyo basi si tungeona Wenzetu kule Zenji ambapo 90% ni Dini moja wakitusua sana na kutoa hiyo pcha kuwa wanabaniwa?

Hivi kama ajira zina upendeleo, serikali inaajiri sehemu gani wa Watanzania wote?
 
Unaongea kujifurahisha alafu ukale kitimoto, jiulize enzi hizo kwanini ulibadilishwa mfumo wa mitihani kutoka jina kwenda kwenye namba? Jiulize ile tume iliyoundwa na jk kipindi kile kupima ufaulu wa wanafunzi katika dini ya kiisalm walikuja na majibu gani?

Na ndio silaha yenu eti waislam hawajasoma ndio maana hawateuliwi, hakuna uthibitisho juu ya hili angalia msomi kama prof assad alivyovuliwa cheo chake unadhani kisa nini? Kumbuka Ramadhani dau alikuwa anashambuliwa nini?
Siongei kujifurahisha, nawashauri tuu ndugu zangu. Japo ni mla Kitimoto lakini ushauri wangu Kama ukiweka hisia pembeni una maana, baniani mbaya kiatu chake dawa. Ni kweli ulibadilishwa mfumo toka kutumia majina mpaka namba,na Mwenyekiti wa NECTA akapewa mtu wa dini yenu Safi.

Lakini jiulize, huu mwaka wa ngapi hayo yamefanyika? Na jee kuna lolote limebadilika kwenye ufaulu hasa shule zinazomilikiwa na taasisi za dini yenu? Ninakupa assignment, nenda DUCE leo, chukua sampuli ya darasa moja la first year, hesabu watu wa dini yako ulinganishe na watu wa dini zingine. Watu wa dini yako hawawezi kufikia hata idadi ya dhehebu moja tuu la RC. Ndalichako mlimuonea bure. Mpaka Sasa shule zenu zinaongoza kwa kuburuza mkia.

Huwezi kuta seminary ya kikatoliki kwenye orodha ya shule kumi zilizofanya vibaya. Narudia Tena, wekezeni kwenye shule, waelimisheni watu wenu, waijue na Elimu Dunia Kama wanavyoijua Elimu Akhera. Hapo wataweza kushindana kwenye soko la ajira. Kinyume chake mtaendelea kulalamika na kamwe msitegemee kubebwa/kuonewa huruma kwa sababu ya dini yenu.

N.B Mimi nimezaliwa familia yenye mchanganyiko wa kiimani japo binafsi nimefuata dini ya Kristu. Niliwahi kumpeleka mwanangu Kirinjiko Islamic seminary akaharibu then Nikamleta UBUNGO seminary nako akawa anaharibu tuu, mazingira ya shule magumu. Nimeamua kumpeleka shule ya Kikristo, Sasa naona utofauti, walau Kuna matumaini ya mtoto kufaulu.
 
Wakijenga shule nzuri watasoma watoto wale wa kule pia kwani wazazi wao ndio wenye ajira, wenye teuzi na wanaohudhuria semina na workshops kila Mara hivyo wanaweza kulipa ada kwenye shule bora zisizoweza kushindana na zike za kata. Hivyo hutashangaa kuona wanaokwenda vyuo vikuu wengi wao Ni wale wanaotokakwenye zile shule bora na ghari. Hawa ndio watakaovijaza vyuo vikuu huko muhimbili unakosema. Tatizo sio watoto Bali wazazi wao na wazazi wao sio tatizo Bali waliotoa fursa bila kuzingatia
Sasa mkuu, ili kuvunja vicious circle hii nini kifanyike? Watu wa dini Ile Wana shule nyingi sana, tatizo ni sifa ya Elimu inayofundishwa hapo. Kwa mfano, kwa Dar tuu, karibu kila mtaa Wana Seminary. Lakini uliza wanafunzi wanaotoka hapo wanaenda wapi? Quality ya Elimu inayotolewa na shule hizo ikoje?

Fanya simple survey, nenda kwenye moja ya shule zao inayojitahidi, UBUNGO Islamic seminary inayomilikiwa na Islamic Propagation foundation, asses mazingira ya wanafunzi kujifunzia, sifa za walimu wanaofundisha, vifaa vya ufundishaji, njoo kwenye content za mitihani ya majaribio Kisha malizia kwa kupitia matokeo yao ya ndani, utaelewa kwa ninj ndugu zetu huwa wanafeli hata kwenye mitihani ya Taifa. Na Jambo hili linaathiri idadi ya watu wao wanaojiunga na Elimu ya juu.

Pia, punguzeni ada kwenye shule zenu, muwape kipaumbele wenzenu. Mbona sisi tumesoma Seminary kwa ada ya 250000/- enzi hizo tena tukiwa tunalipiwa na wazazi wakulima wa ufuta?

Tafuteni namna ya kuvunja mnyororo huu.
 
Hebu kula waziri aagize orodha za watu waliohudhuria kwenye semina, workshops nk zote zilizofanyika mwaka huu tu aone Ni akina Nani wamealikwa, kuhudhuria na kulipwa posho. Baada ya kulipwa posho si wanaenda kulipia ada za watoto wao? Kununua kiwanja? Kufuga kuku? Kupiga rangi nyumba zao?
Hivi Zanzibar ambako Serikali na wafanyakazi wake wote Ni Waislam, shule zake zina perform vipi zikilinganishwa na za Tanganyika?a Kama hujui, performance ya elimu Zanzibar Ni Duni sana!

Waislam Wana matatizo yao wenyewe yanatokana na hiyo dini yao
wasitake kusingizia mfumo Kristo, tangia enzi za Mwinyi wanalalamikia Hilo tu
 
Ushauri kwenu nyie wa hiyo dini
1) kuwekeza kwenye elimu ya mtoto wako sio lazima uwe umeajiriwa na kulipwa posho za semina kama ulivyosema hapo juu. Sasa ivi watu wengi wanajishughulisha na biashara pamoja na kilimo ambazo zinawaingizia pesa nyingi tu. So kuwekeza kwenye elimu ni wewe mwenyewe tu...
Tatizo la Uislam na Waislam Ni Ultra-conservatism,yaani uhafidhina uliopitiliza kiasi kwamba hata elimu na mifumo ya Dunia ya kisasa wanaoona inaendana kinyume na maagizo ya mtume wao kwa hiyo haifai.

Hawa ndio wanaoongoza kwa kupeana ajira kwa misingi ya Dini halafu ndio wanatoa shutuma kwa wengine,
Wanasema Muislam ni ndugu kwa Muislam mwingine, yaani mkienda kuomba kazi Wakristo 10 na Muislam 1 na anayewafanyia interview ni Muislam basi huyo anamchukulia yule Muislam mmoja kama ndugu yake na ndio atatoa upendeleo kwake kuliko Wakristu

Wakristo wapo diverse wapo wakatoliki, Wasababto,Walutheri n.k na wala hawna hizo bond za Waislam ila ndio wanaoonekana wanapeana ajira kwa misingi ya Dini
 
mada za hivi ndiyo mada pekee ambazo wapinzani wa Magufuli huungana naye kwa sababu ya udini
Hivi mkuu, kipindi Cha Kikwete Waislam walikuwa na afadhali gani ukilinganisha na kipindi cha Magufuli? Au kipindi Cha Mwinyi walikuwa na afadhali gani ambazo Sasa hazipo?
 
Sasa mkuu, ili kuvunja vicious circle hii nini kifanyike? Watu wa dini Ile Wana shule nyingi sana, tatizo ni sifa ya Elimu inayofundishwa hapo. Kwa mfano, kwa Dar tuu, karibu kila mtaa Wana Seminary. Lakini uliza wanafunzi wanaotoka hapo wanaenda wapi? Quality ya Elimu inayotolewa na shule hizo ikoje? Fanya simple survey,
expand...
Tatizo la Uislam na Waislam Ni Ultra-conservatism,yaani uhafidhina uliopitiliza kiasi kwamba hata elimu na mifumo ya Dunia ya kisasa wanaoona inaendana kinyume na maagizo ya mtume wao kwa hiyo haifai.

Hawa ndio wanaoongoza kwa kupeana ajira kwa misingi ya Dini halafu ndio wanatoa shutuma kwa wengine
 
Back
Top Bottom